Powered By Blogger

Thursday, April 28, 2011

Fujo Ndani ya ndege zamfikisha rumande.

Bwana Ally Ngenyiki, ambae ni mkazi wa sinza amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka ya kufanya fujo ndani ya kwenye ndege. wakili wa serikali ndugu, Nassoro katunga alidai mbele ya Hakimu mfawidhi joyce minde kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe April 23, katika uwanja wa Ndege ya Julius kambarage Nyerere.

Aidha wakili huyo wa serikali alieleza Mahakama hiyo kwamba, mshitakiwa kwa makusudi akiwa ndani ya Ndege alifanya fujo na kuleta usumbufu  kwa muudumu wa ndege hiyo bi. Viviano Shine. Mshtakiwa alikana shitaka linalomkabili, na kurudishwa rumande mpaka mwezi mei, mwaka huu pale kesi itakapotajwa tena.

Wednesday, April 27, 2011

Kashfa na athari zake katika sheria."Defamation"


SHERIA kwa ujumla wake inazingatia na kutegemea kwamba kila mtu ana haki ya kuwa salama na kwamba mawazo ya watu wengine yatolewe kwa kuzingatia taratibu na sheria ili kwamba mawazo au mtazamo wa watu hao usimuumize mlengwa.

Hivyo basi kutoa maneno yenye lengo la kumdhalilisha, kumuumiza au kumfanya mtu aonekane kwamba hafai mbele ya watu wanaomheshimu na jamii nzima kwa ujumla (kashfa) ni kosa katika sheria.
Kashfa hapa nchini inazungumziwa katika Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, hususan kifungu cha 38 mpaka cha 47. Kwa tafsiri, kashfa ni tamko la maneno ya mdomo au maandishi lililo na lengo la kujeruhi kuvunja hadhi ya mtu fulani katika jamii kwa minajili ya kumfanya achukiwe au kudharauliwa.
Zaidi ya hapo, mahakama katika maamuzi mbalimbali imetafsiri kashfa kwa namna tofauti lakini ikiwa na msingi mmoja. Kwa mfano, katika shauri la Hamisi dhidi ya Akilimali, (1971) HCD, 111 mahakama ilitamka kwamba kashfa ni kuwasilisha akilini mwa mtu mwingine masuala ambayo si ya kweli na yakiwa na uwezekano wa kusababisha kuharibika hadhi ya mtu au watu.

Hivyo basi ndugu msomaji, kuna mambo kadhaa yanayohitajika kuthibitika ili tamko litafsiriwe kama kashfa, mojawapo ni kwamba tamko hilo liwe la kashfa maana yake, mahakama itatakiwa kutafsiri maneno hayo kwa kuzingatia usawa na maana halisi ya neno lenyewe kama mtu mwenye uelewa wa kawaida anavyoweza kulitafsiri neno au tamko hilo.

Kwa hiyo, kiwango cha kupima neno au tamko kama ni kashfa au la ni kwa kumuangalia mtu wa kawaida angelichukuliaje neno au tamko hilo.Hili ni suala la msingi kwa kuwa maneno mengine yakichukuliwa katika mazingira yalipo tamkwa au kuandikwa hayawezi kuhesabika kama ni kashfa ingawa wakati mwingine maneno hayohayo yakitamkwa au yakiandikwa yanaweza kuhesabika kama kashfa.

Kitu kingine ambacho kinatakiwa kuthibitishwa ili neno au maneno yahesabike kwamba ni kashfa ni kwamba maneno hayo yalilengwa kwa mdai na siyo mtu mwingine. Hapa ndugu msomaji, sheria inahitaji mdai awe ametajwa moja kwa moja katika maneno hayo ya kashfa.

Ikiwa vinginevyo mahakama haitahesabu kwamba mdaiwa alikusudia kumtaja mtuhumiwa. Katika shauri la P.M Jonathan dhidi ya Athuman Khalfan, (1975)LRT,65 ambapo mdaiwa aliandika barua kwa Jaji Mkuu na kutoa tamko la mdomo katika tume ya uchunguzi na kwa Ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) wa mkoa wa Dodoma akimshtumu mdaiwa ambaye alikuwa Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi ya mdaiwa na mtu mwingine kwamba amependelea upande mmoja,mla rushwa na asiyefuata maadili.Wakati kesi ikiendelea, swali lilikuwa kama barua ya mdaiwa kwenda kwa Jaji Mkuu na tamko la mdomo kwa RCO ilikuwa ni kashfa. Mdaiwa katika utetezi wake mahakamani, alidai kwamba hakutaja jina lolote Katika tume na kwamba kwa RCO, ushahidi ulionesha kwamba ilikua baada ya kualikwa na mdai mwenyewe.

Katika maamuzi yake mahakama iliamua miongoni mwa mengineyo kwamba pale mdai akitoa taarifa moja kwa moja au kupitia mtu au kitu kingine na taarifa hiyo ikawa ni kashfa basi tamko hilo halitahesabika kuwa ni kashfa kwa kuwa mdai amefanya hivyo kwa kutaka mwenyewe au kwa maneno ya kisheria volent non fit injuria.

Hivyo kwa kuangalia jinsi taarifa inavyotolewa kuna aina mbili za kashfa. Aina ya kwanza ni kashfa inayotolewa kwa njia ya maneno ya mdomo au kwa lugha ya kisheria "slander." Katika aina hii, mdaiwa anatamka maneno yenye lengo la kumchafua na kumdhihaki mdaiwa akitumia maneno ya mdomo.Hii ni aina ya kashfa ambayo kitu kilichotumika kusambaza maneno hayo ya kashfa ni cha muda mfupi na kinasikika kwa masikio. Aina ya pili ni kashfa inayotolewa kwa njia ya maandishi au kwa lugha ya kisheria "libel 
Maandishi hayo yanaweza kuwa katika machapisho, kuchora, mwanasesere au kuchapa maneno yoyote yakiwa na lengo la kumkashifu mtu mwingine. Hivyo aina hii ya kashfa ni ile inayokuwa katika chombo cha kudumu (kama gazeti, jarida, kaseti) na maneno hayo yanaonekana kwa macho sio kusikika kwa masikio.
Hata hivyo kashfa ya maneno ya mdomo itahesabika pale tu itakapothibitika kuna madhara ya kipekee (ya kifedha) ambayo mdaiwa amepata kutokana na maneno hayo ya kashfa. Maneno hayo yanatakiwa yatambuliwe na kuthaminishwa na mdai mwenyewe.

Hata hivyo ndugu msomaji unatakiwa kujua kwamba kashfa ya maneno ya mdomo haitahesabika ikiwa tu maneno yaliyotamkwa yatahesabika ni kosa la jinai linaloadhibiwa kwa kifungo au inahusiana na maneno ya magonjwa ya kuambukizwa kwa lengo la watu wengine wasijihusishe na mdaiwa au kama maneno hayo ni yale yanayozungumzia ushoga, usagaji, uzinifu au kama ni kuhusiana na ushirikina.

Wakati mwingine kuna kashfa kwa kutumia katuni, picha au maneno ambayo ukiyaangalia yenyewe hayana madhara kwa hadhi ya mtu lakini yakiwa na uwezo wa kumkashfu mdai kwa mfano, katika kesi ya Thanker dhidi ya B.G Chipungahelo,[1965],EA,82 ambapo gazeti liliripoti ajali ya gari iliyomhusisha mtuhumiwa na kwamba katika gari hilo kwa mujibu wa gazeti kulikuwa na chupa ya pombe ya Brandy kitu ambacho kilikuwa na lengo la kumuonyesha mdai kama mtu mlevi.

Kwa upande wa adhabu dhidi ya kashfa, sheria imetoa adhabu kadhaa kwa mtu atakayethibitika kuwa ametoa maneno ya kashfa mojawapo ni kwa mdaiwa kutakiwa kumlipa fidia mdai au mhanga wa kashfa.Hapa mahakama itazingatia nakala ngapi za taarifa hiyo ya kashfa zilichapishwa eneo ambalo taarifa hiyo ya kashfa ilizunguka (ukubwa wa eneo, je ni mkoa, nchi au nje ya mipaka ya nchi).Adhabu nyingine kwa mdaiwa ni kukatazwa kuchapishwa tena kwa taarifa hizo katika gazeti, jarida au runinga. Adhabu nyingine inaweza kuwa kwa mdaiwa kuamriwa na mahakama kumuomba radhi mdaiwa katika njia ileile aliyoitumia kumkashfu.

Mara nyingi kama ni jarida au gazeti, mdaiwa atatakiwa kuandika taarifa tena ya kuomba radhi ukurasa wa kwanza na kwa maandishi makubwa. Na Allan Kajembe.

COURTROOM PROCEDURES AND PROTOCOL

  • Arrive at the Hall of Justice 15 minutes early so that you can locate the proper Courtroom. If you see your name on the white bulletin board outside the courtroom or on the docket attached to the cork bulletin board, then by all means go into the courtroom indicated. If you still do not know where your case will be heard, then go into the Clerk's office he will help you.
         
  • Dress appropriately. Dress slacks, shirt, skirt or blouse show respect for the Court. Clean jeans and dress shirt would also be acceptable. Hats are not allowed.
  • Food or drinks are not allowed in the courtroom.
  • Weapons of any kind are not allowed in the Hall of Justice.    
  • The courtroom is not an appropriate place for children. Please arrange for someone to watch them while you are in court. Even if you plan on leaving your children in the lobby, if they are too noisy, it disturbs court proceedings and security may have you remove them from the building.
  • Review your paperwork before your hearing. Stick to the FACTS. Try not to ramble when offering your side of the situation as your time is limited.     
  • Remember to address the Judge or magistrate when speaking, not the other party or their attorney. Don't interrupt the Judge or the other party/lawyer. Wait until it is your turn to speak. Remember to stand when addressing the Judicial officer.     
  • The Judge will ask you questions. If you don't understand the question, say so. Be direct. If you don't know an answer, say so. Take time when answering questions to make sure you answer thoroughly.
  • Be respectful and courteous at all times with the Court. Always address the Judge as "Your lord" or “Your Honour’ for magistrates. Do not interrupt If something needs to be clarified, wait until it is your turn to speak or ask to speak again.
  • Be sincere. Don't be sarcastic or argue with the Court or the other party. Stay calm. 
  • If you are stating dates, times, places, etc., be exact. If you cannot be exact, make it understood that you are only estimating.    
  • Speak clearly and distinctly, using words, phrases, and terminology that you can understand.
  • Remain courteous to the Judge after the ruling. Approach the bench where the Judge and clerk are seated only when told to do so by the Judge.  
  • You may bring a friend or family member for moral support. That person must remain silent, however, and must remain seated in the audience. He or she cannot approach the Judge with you.  
  • Avoid laughing or talking about the case in the hallway or restrooms of the Hall of Justice in such a way that the other party, counsel or witnesses for the other party may see or hear you.   
  • After the Judge /        Magistrate has made a ruling on the issues brought before him, make sure he signs your written order. When that order is filed with the Clerk's Office the decision becomes official. If the order is submitted later, the Judge will require both sides to sign it. If the other party won't sign it, you will have to schedule a hearing on the docket to ask the Judge to enter the order. The other side must be properly served notice of the hearing date and time you have scheduled to present the order.

These are the rules that apply to attorneys regarding Courtroom procedure and etiquette, and must be followed by people who are "pro se" (representing themselves) also.
Provided by:

·         Roni A. Booth, Cowlitz County Clerk

Tuesday, April 26, 2011

'Siasa' mahakamani zamkera Hakimu, ajitoa

HAKIMU Wilberforce Luhwago wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam aliyekuwa akisikiliza kesi ya kukaidi amri ya Mahakama inayomkabili Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, amejitoa katika kesi hiyo huku akionya siasa itaimaliza nchi.

Luhwago amesema, siasa ikiingia mahakamani nchi itayumba na watoto wa shule hawatowaelewa walimu wao kuwa Tanzania kila mtu yuko sawa mbele ya sheria, “wakati hati za kukamatwa na zile za miito mahakamani zinawalenga wauza vitumbua tu na wa misokoto ya bangi.”

Kutokana na uamuzi huo, aliwataka mawakili waliokuja kusikiliza kesi hiyo katika mahakama hiyo kupata habari zote za shauri hilo kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joyce Minde na si yeye tena.

Awali jalada halisi la kesi hiyo lilipelekwa katika Mahakama Kuu kwa mapitio, hali iliyozua mjadala wa kisheria katika mahakama hiyo.

Mmoja wa wanasheria wanaomtetea Fuime, alihoji kwanini mahakama hiyo inaendelea na kesi ambayo jalada lake lipo Mahakama Kuu.

Hakimu Luhwago, alimjibu wakili huyo kuwa kama alitambua katika mahakama hiyo hakukuwa na kesi hiyo, alifika mahakamni hapo kufanya nini na kumtaka aende ilipo kesi hiyo. Hata hivyo wakili huyo alikaa kimya.

“Kwa maneno ya wakili naamini hakuna kesi mbele ya Mahakama hii, basi sasa niamuriwe nikae au niondoke katika meza kuu na nikae kama wasikilizaji wengine waliopo katika chumba hiki cha kusikilizia kesi,” alisema Luhwago.

Awali mahakama hiyo ilitoa hati ya kumuita Faume mahakamani ambayo ilidharauliwa hivyo mahakama ikatoa amri ya kukamatwa kwa mkurugenzi huyo lakini haikutekelezwa.

Faume alitakiwa kufika mahakamani hapo kusikiliza shauri linalohusu mgogoro kati yake na kampuni ya usafi ya TECA uliotokea mwaka 2009.

Mgogoro huo ulianza baada ya Mkurugenzi huyo kutoa hati ya kusimamishwa kwa kazi ya uzoaji taka iliyokuwa ikifanywa na kampuni hiyo, kampuni hiyo ikaenda mahakamani.

TAMKO LA TLS KWENYE MUSWADA WA SHERIA YA MAPITIO YA KATIBA 2011

  1. 1.          TLS: TAARIFA YA DHARURA juu ya Muswada wa Katiba
Tarehe 9 Aprili, 2011
DAR ES SALAAM

Uundwaji wa Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara na Majukumu yake

Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (“TLS”) ni Taasisi ya Wanasheria wa Tanzania Bara iliyoanzishwa kwa Sheria ya Chama cha Wanasheria cha Tanganyika, Sura ya 307 Toleo la 2002. Kwa mujibu wa Sheria hii, Chama kina, pamoja na mambo mengine, jukumu la kuisaidia Serikali katika mashauri yanayohusu utungaji wa sheria na utekelezaji na matumizi ya sheria, na pia kulinda na kusaidia umma katika masuala yote yanayohusika na kadhia za sheria.

Chama cha Wanasheria kinatoa taarifa hii kwa mujibu wa mamlaka mahsusi ya sheria.
Mazingira ya Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, 2011

Tarehe 11 Machi, Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, 2011 (kwa kifupi “Muswada”) ulitangazwa katika Gazeti la Serikali la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Toleo Namba 1 Jarida Na.2. Chama kilipata nakala ya Muswada huo Jumanne, tarehe 30 Machi, na kilisambaza hizo taarifa kwa wanachama wake siku ya Alhamisi tarehe 31 Machi ili kupata maoni yao. Siku ya Jumamosi tarehe 2 Aprili, Chama cha Wakufunzi wa Chuo cha Dar es Salaam (UDASA) waliendesha mjadala wazi kuhusu Muswada, mjadala ambao uliripotiwa kwa mapana katika vyombo vya habari. Siku ya Jumanne, tarehe 5 Aprili, Chama chetu kilialikwa kupitia Kurugenzi ya Kamati za Bunge (“Kurugenzi”) kushiriki katika mjadala juu ya Muswada ambao ulipangwa kujadiliwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge (kwa kifupi “Kamati”) tarehe 7 Aprili Dodoma, kama ilivyopangwa awali. Mnamo mwisho wa siku hiyo Chama chetu kiliulizia maendeleo kuhusu mijadala bayana, na kikahabarishwa kwamba sasa sehemu mpya tatu (3)zimetajwa kwa ajili ya mijadala bayana, yaani Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar; aidha taarifa tulizopata ni kwamba mijadala itafanyika tarehe 7 na 8 Aprili, na ikibidi tarehe 9 Aprili. Kutokana na uthibitisho huu,Chama chetu kikaahidi kushiriki kikao cha Dar es Salaam.

Jumanne tarehe 5 Aprili Muswada uliwakilishwa Bungeni kwa Hati ya Dharura isomwemara ya kwanza. Tarehe 7 Aprili, Rais wa Chama chetu aliipelekea Kamati - kwa maandishi - maoni na mapendekezo ya wanachama wa Chama cha TLS kuhusu Muswada. Tarehe 8 Aprili, Rais wa Chama cha TLS alitoa mapendekezo kwa mdomo.

Baada ya kushiriki katika mijadala ya umma, Chama kilitiisha mdahalo kuhusu Muswada kwa wanachama ili kuhakikisha mawazo ya wanachama wengi iwezekanavyo yanakusanywa kuthibitisha msimamo wa wengi katika Chama.

Hoja na Maoni
UTANGULIZI

Kwa kuwa Chama cha TLS kimejizatiti kwa dhati kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria nchini Tanzania, kwa kujua kwamba sheria inapozingatiwa ipasavyo, utawala wa sheria huwalinda wananchi dhidi ya matumizi ya kibabe ya mamlaka ya Serikali; kwa kuwa tunaafiki dhana kwamba sheria zote lazima zitungwe kwa shabaha ya kuenzi Utawala wa Sheria, utawala bora na nyanja ya demokrasia ambayo imejengewa misingi imara katika falsafa ya haki ya nchi yetu na ambayo inashabihiana na viwango vya kimataifa na vyenye ubora maridhawa; kwa kuwa Chama kinaamini kwa dhati kwamba hatima na mchakato mzima kuhusu marejeo na utungaji wa Katiba mpya unapaswa kupata uhalali muafaka kwa njia ya ushirikishwaji wa wananchi; na kwa kusisitiza kwamba haki haitakiwi tu ifanyike, bali pia ionekane kwamba inafanyika, Chama kinaeleza msimamo wake mintarafu ya Muswada kama ifuatavyo:

1. Kuhusu lugha ya Muswada: Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba Muswada utangazwe katika lugha ya Kiswahili, kwa kuzingatia dhana ya haki kupatikana (jambo ambalo linamaanisha mtu wa kawaida kupata nakala na uelewa) kwa Watanzania wote (wanaoishi vijijini na mijini, wananchi wa kawaida, wenye mapato ya kati na wa matabaka ya juu), ikiwa ni sambamba na lugha inayotambulika ya toleo rasmi la Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977 (kwa kifupi “Katiba”);

2. Kuhusu jina la Muswada: Chama kinashauri kwa dhati kwamba jina la Muswada lisomeke ‘Muswada wa Kutunga Katiba Mpya, 2011’ ili kuonyesha dhahiri nia ya wananchi (kwamba wanataka Katiba mpya, siyo marekebisho yake) katika mchakato mzima;

3. Kuhusu maelezo ya awali la Muswada: Chama kinapendekeza kwamba tamko la awali lirekebishwe na lioneshe wazi madhumuni: MUSWADA wa Sheria itakayoweka mfumo wa kutunga/kuweka Katiba mpya inayokidhi vigezo vinavyokubalika kimataifa vya demokrasia na utawala bora’;
4. Kuhusu ukomo wa Katiba na utungaji wa rasimu ya Katiba mpya: Chama kinatoa tahadhari kwamba Katiba ya sasa haisemi lolote kuhusu ukomo wa Katiba na utungaji wa katiba mpya; kwa mujibu wa Ibara ya 98, ni utaratibu pekee unaotajwa wa kufanya marekebisho.

Kutokuwepo kwa vipengele vya suala hili kutafanya michakato yoyote ya kuunda Katiba mpya kuwa batili.

Hivyo basi kama jambo la lazima, Chama kinapendekeza kwa dhati yafanywe marekebisho ya Katiba, kuwekwe vipengele vitakavyoruhusu utaratibu wa ukomo wa Katiba iliyopo na utungaji wa Katiba mpya.

5. Kuhusu kifungu cha 5 cha Muswada - Uundwaji wa Tume: Chama kinashauri kwa dhati kwamba Tume iundwe moja kwa moja na Sheria hii. Lugha inayotumika katika Muswada inakasimu kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania mamlaka ya kuunda Tume ambapo Rais atakuwa na uhuru wa utendaji. Aidha Rais analazimika kuunda Tume hiyo baada ya tarehe 1 Juni 2011 (tarehe ambapo sheria hii itaanza kutumika), lakini hakuna kikomo kinachotajwa cha jukumu hili.

Ili kurekebisha kasoro hizi, kifungu hiki kisomeke, “Tume ya Katiba inaundwa kwa Sheria hii.”

6. Kuhusu kifungu cha 6 cha Muswada - Uteuzi wa wajumbe wa Tume: Chama kinatoa maoni na mapendekezo yafuatayo:
  • Uwakilishi katika Tume: Muswada unapendekeza Tume iwe na uwakilishi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa idadi sawa. Lakini kifungu hiki hakizingatii hata kidogo tofauti ya ukubwa wa idadi ya watu na kwamba Katiba ya Muungano inahusika na Zanzibar pale tu masuala ya Muungano yanapotajwa. Hivyo basi, ili kuhakikisha kuna uwiano stahikikatika Tume (yaani unaozingatia sura halisi ya mambo), idadi ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na kutoka Visiwani izingatie idadi ya watu.
  • Muundo wa Tume: Tume iwe Jopo la Wataalamu watakaoteuliwa kutoka mchanganyiko wa kada za taaluma, mashirika na jumuiya mbalimbali kwa kuzingatia jinsia, dini na ngazi za utaalamu. Aidha kif. 6(2)(e) kinampa Rais mamlaka ya kuteua kwa hiari yake wajumbe wa Tume wasiokuwa katika makundi ya watu waliotajwa katika fasili (a) hadi (d)- jambo ambalo linaweka mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka.
7. Kuhusu Kifungu cha 8 cha Muswada - Hadidu za Rejea (kwa kifupi “hadidu”) za Tume: Kwa ajili ya uwazi na uwajibikaji, Chama kinapendekeza kwamba hadidu ziandikwe na chombo huru na ziidhinishwe na Bunge la Tanzania
, badala ya Rais.
8. Kuhusu Kifungu cha 14 cha Muswada – Gharama za Tume: Muswada unadhihirisha dhamira ya Serikali kwamba matumizi ya Tume yatalipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali. Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba kuwe na mfumo wazi, bayana na wa uwajibikaji katika kuidhinisha na kutoa taarifa za matumizi.

9. Kuhusu Kifungu cha 16 cha Muswada – Kutoa taarifa kwa Rais: Ili pawe na mfumo wazi na bayana, Chama kinapendekeza kwamba Taarifa ya Tume iweze kupatikana kwa umma, yaani wananchi waione na waruhusiwe kutoa maoni yao juu yake, hata kama taarifa inapelekwa kwa Rais.

10. Utekelezaji: Ili kuhakikisha kwamba Watanzania hawaachwi nje ya mchakato huu, Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba shughuli ya Tume – kwa mtizamo wa kawaida – zifanyike mikoa yote 26 ya Tanzania, na siyo katika baadhi tu ya mikoa, kama msimamo ulivyojitokeza kwenye mijadala bayana iliyoendeshwa na Kamati ya Bunge.

11. Kuhusu vipengele visivyoruhusiwa kuguswa – Kifungu cha 9 (2) na 20 (1):
Muswada unafanya vipengele vya msingi vinavyohusu ibara za msingi za Katiba visiguswe. Kwa mfano, kif. 9 (2) kinataka mambo ya Muungano na suala la ofisi ya Rais, mambo yote mawili ambayo yaliyowekwa na Katiba, yasiguswe. Kif. 20 (1) kinakinzana na Ibara 26(2) ya Katiba ambayo inalinda haki ya mwananchi kupinga uhalali wa kikatiba wa sheria za nchi. Kuviacha vifungu vibaki pia ni kukiuka utekelezaji wa Utawala wa Sheria.

12. Kuhusu kasoro za uchapishaji zimebainika, lazima ziepukwe kwa uangalifu: Usahihi wa Muswada unategemea uandishi na rejea sahihi. Kwa mfano, kif. 19 kinatakiwa kurejea kif. 18 na siyo kif.19; na kif. 20 (3) kirejee kif. 20(2) na siyo kif. 20 (1). Athari ya hili la pili, kwa mfano, ni kumtwika tuhuma ya jinai mtu yeyote anayeamua kufungua shauri mahakamani kupinga Sheria hii – jambo ambalo ni kinyume na Katiba, na ni ukiukwaji wa haki na wajibu wa msingi.

13. Kuhusu Kifungu cha 21 cha Muswada - Kutangazwa Baraza la Kutunga Katiba: Muswada unatamka kwamba Rais ana mamlaka ya kuunda Baraza la Kutunga Katiba na kwamba anaweza kutamka Bunge lijigeuze kuwa Baraza la Kutunga Katiba.

Chama kinapendekeza kwamba Rais asiwe na mamlaka ya kuligeuza Bunge kuwa Baraza la Kutunga Katiba, na kwamba muundo wa Baraza uamuliwe na wananchi watakaoteuliwa kutoka kada mbalimbali (yaani taaluma na uzoefu, mashirika, taasisi za kidini na makundi mbalimbali).

14. Kuhusu Kifungu 26 cha Muswada – Kusimamia kura ya maoni (referendum): Inaonekana kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi si mahala pake kuratibu suala la uhalalishaji wa Katiba. Chama kinapendekeza kwamba taasisi za jamii, vyama vya siasa na watu binafsi na makundi mengine waruhusiwe kushiriki kwa uhuru uelimishaji wa umma kuhusu upigaji wa kura ya maoni.

Hatimaye Tume ya Katiba idhibiti uenendeshaji wa upigaji kura ya maoni.

15. Kuhusu sehemu ya VI – Uhalalishaji wa Katiba: Chama kinapendekeza kwamba mchakato wa uhalalishaji uendeshwe na Tume, siyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kuwa imeundwa na Katiba.

Mpango wa Chama wa Hitimisho:

a) Chama kinashauri kwa dhati kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, aiondoe Hati ya Dharura iliyoambatanishwa na Muswada uliowasilishwa Bungeni. Kwa ushauri wa Chama Muswada ufuate utaratibu wa kawaida ili Wabunge na umma wote upate fursa ya kutosha kujadili na kutoa maoni kuhusu Muswada.

Hali halisi, Halmashauri ya Chama cha Wanasheria kimeamua kumtembelea Mtukufu Rais ili kumfikishia yeye binafsi ujumbe huu.

b) Chama kinaisihi Serikali isitafute kugundua upya gurudumu katika mchakato huu – kwa kadiri inavyowezekana, Serikali ijifunze kutoka uzoefu wa nchi nyingine, kama vile Kenya na Uganda.

c) Chama chetu kiko mbioni kuunda Kamati ya Katiba, ambayo- pamoja na mambo mengine- itaishauri Halmashauri yetu juu ya maendeleo ya mchakato unaoendeshwa na Serikali, itatoa msaada wa kitaalamu na utatoa mapendekezo stahiki kwa Halmashauri yetu, umma na vyombo vinavyohusika na mchakato wa kutunga Katiba.

Kama hapana budi, Halmashauri ya Chama itapanua majukumu ya Kamati hii ili iweze kuwa
msemaji kwa niaba yake kuhusu mijadala, ambayo yaweza kuhitaji hatua zaidi.

Imewakilishwa kwa niaba ya Chama cha Mawakili Tanzania Bara
Francis K. Stolla
RAIS

UTAFITI WA HALI YA HAKI ZA BINADAMU KWA BABU LOLIONDO



                                                Umati nyumbani kwa babu

Baada ya kuona maelfu ya watanzania wanakwenda kwa wingi katika kijiji  cha Samunge mjini loliondo kwa lengo la kupata kikombe cha dawa  kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T)  Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Sonjo Mtaa wa Samunge, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilituma watafiti wake mjini Loliondo kuangalia hali ya haki za binadamu katika eneo hilo.

Lengo la ufuatiliaji huu ni  kubaini  ukiukwaji wa haki za binadamu unaotokea katika kijiji hicho kutokana na maelefu ya watanzania  na raia wa kigeni kumiminika kwa wingi katika kijiji cha Samunge.Ufuatiliaji huu ulilenga  kuangalia  jinsi serikali ilivyo lishughulikia  suala hili la huduma  ya tiba mbadala maarufu kama kikombe cha Babu wa Loliondo.Pia ufuatiliaji huu ulilenga kuangalia ubora hasa usalama wa dawa yenyewe, madhara ya msongamano wa watu na magari, huduma za jamii na matukio mengine ya kibinadamu. Habari hii chanzo chake ni kituo cha haki za binadamu.

MREMBO MAHAKAMANI KWA KUMUIBIA AFISA WA TAKUKURU

MSICHANA Gatti Samweli (26), mkazi wa Kinondoni, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashtaka ya kumuiba Afisa wa Taasisi na Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).Mbele ya Hakimu Marko Mochiwa imedaiwa na Karani Fatma Khatibu kuwa Aprili 11, mwaka huu, mshitakiwa aliiba vitu mbalimbali vikiwemo simu za mkononi, nyaraka mbalimbali ambazo ni mali ya mlalamikaji Alex Tungombe.

Mshitakiwa amekana mashtaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 20, mwaka huu.

Pia, Abdul Hoza (30), mkazi wa jijini hapa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashtaka ya wizi.

Mbele ya Hakimu Suzan Makabwa ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Benedict Nyagabona Februari 22, mwaka huu, mshitakiwa aliiba vitu vya aina mbalimbali vyenye thamani ya sh. 128,000 mali ya mlalamikaji Siwema Mkwayu.

Mshitakiwa amekana mashtaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 21, mwaka huu.

Wakati huo huo, Ramadhani Hamis (18), mkazi wa Mburahati amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashtaka ya wizi.

Mbele ya Hakimu Hilda Lyatuu imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Benedict Nyagabona Aprili 6, mwaka huu, mshitakiwa aliiba vitu vya aina mbalimbali vyenye thamani ya sh. 208,000 mali ya mlalamikaji Polycalp Mwingiba.Mshitakiwa amekana mashtaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 20, mwaka huu. source. Darleo

JK AONGOZA SHEREHE ZA MUUNGANO ZANZIBAR

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa tanzania leo; akiwaongoza maelfu ya watanzania huko Zanzibar; katika sherehe za miaka 47 ya Muungano. Muungano huo hata hivyo bado unalalamikiawa  kuwa na mapungufu fulani ya kimuundo na kisheria. Huenda Matatizo haya yatatatuliwa na katiba mpya.

Msaada kwa mdau.....

Learned friends,there's this lawyer (firm) who is representing me in a case that is still pending in court. Now I have been sued in another case and when I appeared in court to my surprise,the same lawyer who's acting for me in the other case is representing the Applicant.In short the counsel is representing me in one case,and accepts instructions to act against me in another case.How ethical is that?  From Mdau Veronica: Facebook Attorneys.