Powered By Blogger

Tuesday, August 21, 2012

Sababu 7 zilizopelekea C.C.M kushindwa Igunga




Chama cha Mapinduzi jana kilioteza jimbo la Uchaguzi la igunga baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutengua matokea ya uchaguzi huo, yaliyompa ushingi Dk. Kafumu mapema oktoba mwaka jana.

Akiiongoza Mahakama hiyo Mheshimiwa Jaji Mary Shangali alitangaza kutengua Uchaguzi huo baada ya kurishika na hoja saba kama zifuatavyo:Akitoa hukumu hiyo, Jaji Mary Nsimbo Shangali alisema Mahakama ilipokea malalamiko 15 ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili, lakini baadaye yakaongezwa madai mengine mawili hivyo kufikia 17.“Madai yaliyopokewa na Mahakama ni 17 na kati yake imethibitisha madai saba,” alisema Jaji Shangali katika hukumu hiyo.

1.   Kwamba Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alitumia nafasi yake ya uwaziri kutoa ahadi ya ujenzi wa Daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni moja ya kero kubwa kwa wananchi wa Jimbo la Igunga. 

2.   Kwamba Dk Magufuli akiwa katika moja ya kampeni za uchaguzi huo, alitumia nafasi ya uwaziri kwa kuwatisha wapigakura wa jimbo hilo kwa kusema kama hawatamchagua mgombea wa CCM, watawekwa ndani. 

3.   Kwamba Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage alitangaza kuwa mgombea wa Chadema alikuwa amejitoa katika uchaguzi huo, jambo ambalo Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliokuwa ukitolewa.

4.   Kwamba kitendo cha Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Rage kupanda na bastola jukwaani, kulipelekea wapiga kura kuhofia na kuleta dosari katika uchaguzi huo.

5.   Kwamba kauli ya Imamu Swaleh Mohamed wa Msikiti wa Ijumaa Igunga, kuwatangazia waumini wa msikiti huo kuwa wasikichague Chadema, kwa kuwa baadhi ya viongozi wake wamemdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario.

6.   Kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kudai kuwa Chadema kilileta makomandoo katika uchaguzi huo na kupanga kuuvuruga.
7.   Hoja nyingine ambayo Jaji Shangali aliikubali ni ugawaji wa mahindi ya kuwawezesha wakazi wa Igunga kukabiliana na njaa wakati wa uchaguzi huo kwamba ulitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kuwashawishi wananchi wawapigie kura. Jaji huyo alihoji iwapo wakazi wa Jimbo la Igunga walikuwa na njaa sana wakati wa uchaguzi huo kiasi cha viongozi wa Serikali kuona kuwa ulikuwa wakati mwafaka wa kugawa mahindi hayo.

Hata hivyo haijaeleweka mara moja iwapo chama cha mapinduzi kitakata rufaa Mahakama ya rufani au vipi. Ila kwa mujibu wa sheria wanayo nafasi hio.

JAMHURI LAANDIKA" MAJAJI MAJI SHINGONI"

http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/08/224.jpg

Mawakili kesi ya Hamad Yashid"wapinga uwezo wa Makama kuu"

Gazeti la Mwananchi limeandika, Kwamba Mawakili wa wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) katika kesi dhidi ya mbunge wa Wawi, Zanzibar, Hamad Rashidi na wenzake 10, wamedai kuwa Mahakama Kuu Tanzania haina uwezo wa kuwachukulia hatua kwa kumvua uanachama Rashid na wenzake.

Mawakili hao Taslima Law Chamber ( Advocates) na J C Kerariy& Co Advocates wametoa madai hayo wakati wa usikilizwaji wa maombi ya Rashid na wenzake wanaoiomba Mahakama Kuu Dar es Salaam kuwatia hatiani na kuwafunga wadhamini wa CUF.

Rashid na wenzake waliwasilisha maombi hayo mahakamani hapo  Januari 10 mwaka huu , wakidai kuwa Baraza la Taifa la Uongozi la CUF lilipuuza amri ya mahakama hiyo iliyolizuia kuwajadili wala kuwachukulia hatua zozote wakati wa mkutano wake wa Januari 4, 2012, mjini Zanzibar.Amri hiyo ya Mahakama kulizuia baraza hilo kuwachukuliwa hatua yoyote Rashid na wenzake ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari, 2012 kufuatia maombi waliyoyawasilisha mahakamani hapo Januari 3, 2012, chini ya hati ya dharura.

Katika maombi hayo (ya Januari 3) Rashid na wenzake walidai  kuna kesi ya madai namba 1 ya mwaka 2012  waliyoifungua mahakamani hapo wakihoji muundo wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho   na uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo.

Katika maombi hayo walidai kuwa licha ya baraza hilo kupata taarifa za kuwepo kwa amri hiyo ya mahakama saa tatu kabla, lakini baraza hilo liliendelea na azma yaka na hatimaye kuwafukuza uanachama.

Mbali na wadhamini hao, wengine ni wajumbe wa Baraza Taifa la Uongozi la chama hicho, Hivyo wanaiomba mahakama iwatie hatiani na kuwafunga jela wadhamini hao a pamoja na wajumbe wa Baraza la Taifa la Uongozi la chama hicho akiwemo Makamu wa kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika utetezi wao waliouwasilisha mahakamani hapo kwa njia ya maandishi wadhamini hao wa CUF kupitia kwa mawakili wao, wanadai wakati baraza hilo likitoa uamuzi wa kuwavua uanachama Rashid na wenzake, hapakuwa na amri halali ya Mahakama.

Mawakili hao wa CUF wanadai kuwa amri hiyo inayodaiwa na waombaji haikuwa  nakala halisi bali nakala iliyonakiliwa kwa njia ya kielektroniki [scanned] na kwamba hata hivyo hakuna ushahidi kwamba iliwafikia wadaiwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa mawakili hao, hata kama amri hiyo ingekuwa ni halali na hata kama kungekuwa na ushahidi kuwa iliwafikia wadaiwa kabla ya kutoa uamuzi wa kuwavua uanachama walalamikaji bado Mahakama Kuu haiwezi kuwachukulia hatua.

Wanadai kuwa utaratibu wa kuwasilisha taarifa na utekelezaji wa amri zinazotolewa na mahakama zote kwa jumla nchini Tanzania kama unavyoelezwa katika  Amri ya V Kanuni ya 22 (2) CPC haukufuatwa.

Mawakili hao wanadai kuwa kwa mujibu wa amri na kanuni hizo kama mlalamikiwa anaishi katika mamalaka ya Mahakama  Kuu ya Zanzibar , amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania Bara kwenda kwa malalamikiwa ambaye ni mkazi wa Zanzibar ilipaswa ipitie kwanza Mahakama Kuu ya Zanzibar.“Utaratibu huu haukufuatwa na mlalamikaji wa kwanza na kile mlalamikaji wa kwanza alichokuwa akijaribu kufanya hakiko katika matakwa ya kisheria inayotumika,” wanadai  mawakili hao.

Wanadai katika jedwali la kwanza la Katiba ya Tanzania, Mahakama Kuu si miongoni mwa mambo ya Muungano, isipokuwa Mahakam a ya Rufani tu, hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania haina mamlaka ya kisheria kwa mambo yanayofanyika Zanzibar.

Mbali na Hamad Rashid wengine waliofukuzwa uanachama CUF ni Doyo Hassan Doyo, Shoka Khamis Juma na Juma Saanane, wote wakiwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho. 

Thursday, August 16, 2012

DRC: MWANAMUZIKI KOFI OLOMIDE AFUNGWA MIEZI 3.



Koffi Olomide

Mwanzamuziki gwiji wa miondoko ya rumba amefungwa kifungo cha miezi 3 na Mahakama moja ya mjini kinshasa baada ya kukutwa na hatia kwa kuvuruga usalama wa umma. 
 
Mapema jana Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa na kufikishwa mahakamani. Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinshasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.

Kesi hiyo iliharishwa hadi leo(Alhamisi)asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10 lakini idadi hio ya mawakili iliongezeka na kufikia 14 .Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.

 Jopo la mawakili wanaomtetea mwanamuziki huyo, huenda ikakata rufaa baada ya kutoridhishwa na kifungo alichohukumiwa mteja wao.

Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo

TUNDU LISSU" AFICHUA MENGI" JUU YA MAJAJI KATIKA UTETEZI WAKE MBELE YA KAMATI YA MAADILI YA BUNGE.

Nimenunua nakala kutoka Gazeti la JAMHURI ambalo limeamua kutoa utetezi wa Lissu neno kwa neno ili wasomaji waweze kujua kilichomo ndani ya Mhimili wa Mahakama. Ninanukuu kilichoandikwa katika gazeti hilo.

Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, ametoa ushahidi mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kuthibitisha kile alichokisema bungeni Julai 13, mwaka huu kuhusu uteuzi wa majaji na sifa zao. Katika ushahidi wake ameweza kuonyesha ni kwa namna gani - kwa nyakati tofauti - marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakivunja Katiba kwa kuwaongeza muda na kuwateua majaji waliofikisha muda wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwenye orodha hiyo amewataja baadhi ya majaji wasiokuwa na sifa ya kuwa majaji katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa akiwamo mmoja aliyelazimisha kuingia darasani katika Chuo Kikuu Huria, ili aweze kupata shahada ya sheria kama kwa mujibu wa Katiba. Wamo majaji wengine walioteuliwa kushika nafasi hizo nyeti ilhali wakiwa wanakabiliwa na tuhuma nzito za rushwa na ukiukaji wa maadili ya kazi wakiwa mahakimu na wanasheria.

Aidha, kuna majaji amewataja wasiokuwa na uwezo wa kuandika hukumu, akitoa mfano wa jaji mmoja aliyeshindwa kuifanya kazi hiyo kwa miaka minne, akanyang’anywa. Aliyekabidhiwa baada yake aliifanya kazi hiyo ndani ya wiki tatu tu. Lissu amewataja majaji wengine wagonjwa ambao tangu wateuliwe hawajawahi kusikiliza kesi na kuzitolea hukumu.

UTANGULIZI
Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha Maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, Maoni ya Kambi yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa “kuidhalilisha” Mahakama na/au “kuwadhalilisha majaji” (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); “kuwavunjia heshima majaji” (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); “kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji” (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); “kufedhehesha Mahakama na majaji” (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

Aidha, Msemaji wa Kambi alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na “kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote” (Mangungu). Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba “... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na hii Tume ya Uajiri wa Mahakama.” Zaidi ya hayo, “... labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii.”

Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba. Msemaji wa Kambi alikataa kufuta kauli hiyo ambako Mwenyekiti wa Kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi. Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hili muhimu. Maelezo haya yana lengo la kutoa ufafanuzi huo.

Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya BUnge, Lissu alisema, “Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana ‘uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa Madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.”

TATIZO LA MUDA MREFU

Kuna ushahidi mkubwa kuthibitisha kwamba kuna watu wameteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu “... wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma (na) wanapewa ‘zawadi’ ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni.” Ni muhimu kuweka wazi hapa kwamba utamaduni huu haukuanza baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchaguliwa kuwa Rais, bali ni tatizo la muda mrefu. Kwa mfano, marehemu Jaji Kulwa Masaba na Jaji Madina Muro na majaji Stephen Ihema, Juxton Mlay, Augustine Shayo na Vincent Lyimo waliteuliwa majaji wa Mahakama Kuu baada ya utumishi wa muda mrefu kwingineko katika utumishi wa umma.

Majaji Masaba na Muro waliteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi na – kwa kadri ninavyofahamu - hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika! Jaji Lyimo aliteuliwa Machi 28, 2007 mwaka mmoja kabla ya muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, ilipofika Oktoba 26, 2007 Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo Phillemon Luhanjo alimtaarifu Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete “... ameamua kusogeza mbele muda wa kustaafu wa Mheshimiwa Jaji Vincent Kitubio Damian Lyimo kwa miaka mitatu  kuanzia Machi 28, 2008 siku ambayo angestaafu kwa lazima”!

Kwa upande wao, Majaji Ihema, Mlay na Shayo walijizolea umaarufu kwa kuwa majaji wasioandika hukumu na hivyo kuwa wacheleweshaji wakubwa wa kesi katika Mahakama Kuu. Jaji Ihema alitia fora kwenye jambo hili kiasi kwamba Juni 16, 2003 Mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Mzee Joram Allute, alilazimika kumwandikia Rais Benjamin Mkapa maombi ya kumwondoa Jaji Ihema kama Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania “kwa uzembe na kukosa maadili.”

Mzee Allute alikuwa na kesi kwa Jaji Ihema ambapo Jaji huyo ‘alikalia’ uamuzi kwa zaidi ya miaka minne hadi aliponyang’anywa faili la kesi hiyo na kukabidhiwa Jaji mwingine aliyeandika uamuzi ndani ya wiki tatu! Mwezi mmoja kabla ya barua ya Mzee Allute kwa Rais Mkapa, mawakili wake walikuwa wamemwandikia Jaji Mkuu Barnabas Samatta kulalamikia ucheleweshaji wa uamuzi wa kesi hiyo. Mawakili hao walidai: “Hadhi na heshima ya Mahakama inaporomoka vibaya kama inachukua zaidi ya miaka mitatu kwa Jaji kutafakari na kutoa uamuzi kwa jambo jepesi kama maombi ya pingamizi.” Licha ya malalamiko haya dhidi yake, Jaji Ihema alipatiwa mkataba wa ajira wa miaka miwili mara baada ya kustaafu mwaka 2005.

MAJAJI WA MIKATABA

Agosti 2, 2005 Jaji Kiongozi Hamisi Msumi alitoa taarifa kwa majaji wote wa Mahakama Kuu kwamba Jaji Ihema alikuwa amepewa mkataba mpya baada ya kustaafu kama Jaji wa Mahakama Kuu. Taarifa hiyo ilimfanya Jaji Bernard Luanda, wakati huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, kuhoji ‘Uhalali Kikatiba kwa Majaji Kufanya Kazi kwa Mkataba Baada ya Kustaafu.’ Katika taarifa yake kwa Jaji Kiongozi Msumi, Jaji Luanda alisema kwamba “... suala la majaji kupewa mikataba ... linaenda kinyume na Katiba.” Jaji Luanda alifafanua: “Kwa kuwa Jaji amestaafu, basi kiapo chake nacho kimeondoka. Kwa bahati mbaya hawaapishwi ili washike kazi hizo za ujaji.... Ni hoja yangu kwamba Majaji waliostaafu na kupewa mikataba si Majaji kwa mujibu wa Katiba.”

Msimamo wa Jaji Luanda uliungwa mkono mwaka mmoja baadaye na Jaji wa Rufaa, Augustino Ramadhani wakati huo akiwa Kaimu Jaji Mkuu. Katika ‘Mawazo Kuhusu Vifungu Vinavyohusu Mahakama na Majaji’ aliyomwandikia Jaji Mkuu Samatta na kunakiliwa kwa Majaji wa Rufaa wote, Jaji Ramadhani alisema kwamba “... sio sahihi kwa Jaji Mkuu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huo kupindukia umri wa miaka 65 (ambao ndio umri wa kustaafu kwa lazima kwa Jaji wa Rufaa na Jaji Mkuu).” Baadaye Jaji Luanda aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wakati Jaji Ramadhani alikuja kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Kauli ya Kambi kwamba kuna ukiukaji mkubwa wa Katiba kuhusiana na uteuzi wa majaji inaungwa mkono na nyaraka za ndani ya Serikali na hasa Ofisi ya Rais, Ikulu yenyewe. Desemba 6, 2007, mkutano kuhusu ajira ya majaji waliostaafu ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Kiongozi Luhanjo. Wajumbe wengine walikuwa pamoja na Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika na Naibu wake Sazi Salula, Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Sophia Wambura na Susan Mlawi wa Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa Kumbukumbu za Mkutano huo, “kwa utaratibu unaotumika sasa, baadhi ya Majaji wanaofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa Ibara ya 110(1) kwa Majaji wa Mahakama Kuu na Ibara ya 120(1) ya Katiba wanaongezewa muda wa kuendelea na utumishi wao kwa mkataba baada ya wao kuwasilisha maombi rasmi.” Baada ya mjadala juu ya jambo hili, wajumbe wa mkutano walikubaliana kwamba “utaratibu wa kuongeza muda kwa njia ya mkataba unakiuka masharti ya Katiba na kuleta mkanganyiko kama Majaji hao wanastahili kulipwa mshahara au pensheni au vyote kwa pamoja.”

Matokeo ya mkutano wa Ikulu ilikuwa ni kuundwa kwa ‘Kikundi Kazi kwa Ajili ya Kuchambua na Kushauri Kuhusu Ajira ya Majaji Baada ya Kustaafu’ chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kikundi Kazi kiliwasilisha Taarifa yake Machi 7, 2008. Katika Taarifa yake Kikundi Kazi kinakubaliana na msimamo wa kikatiba kwamba “kwa kuzingatia Ibara za 110 na 120 za Katiba inaonekana wazi kuwa suala la ajira za mikataba kwa Majaji ambao wamekuwa wakifanya kazi za Jaji baada ya kufikia umri wa kustaafu ni kinyume cha Katiba.” Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, hadi mwezi Machi 2008, “... walikuwepo Majaji wawili ... wa Mahakama ya Rufani na Majaji tisa ... wa Mahakama Kuu, ambao wapo katika ajira za mkataba, na Jaji mmoja ... wa Mahakama Kuu aliyeongezewa muda wa ajira kwa mujibu wa masharti ya Katiba....”

Hii ina maana kwamba, kulikuwa na Majaji kumi na moja ambao walikuwa wanafanya kazi kinyume cha Katiba na – kwa maneno ya Jaji wa Rufaa Luanda – hawakuwa Majaji kwa mujibu wa Katiba! Aidha, kwa mujibu wa ushahidi wa nyaraka hizi, kulikuwa na Jaji mmoja tu ambaye alikuwa ameongezewa muda wa ajira ya ujaji kwa mujibu wa Katiba. Katika mapendekezo yake, Kikundi Kazi hakikumung’unya maneno:

“Mikataba iliyopo hivi sasa iko kinyume cha Katiba.... Hii ina maana kwamba Majaji hao wanafanya kazi ya Jaji kinyume cha Katiba, hivyo kazi zote ambazo wamezifanya na wanaendelea kuzifanya wakiwa chini ya ajira mpya za mikataba hazina uhalali wowote kisheria. Kazi hizo ni sawa kama vile zimefanywa na mtumishi mwingine yeyote asiye na madaraka ya Jaji. Hivyo basi, Rais ashauriwe kuifuta mikataba hiyo mara moja kwa vile ina madhara makubwa kwa jamii na katika uteuzi wa Majaji wapya kuchukua nafasi zao. Majaji waliofutiwa mikataba waendelee na pensheni zao kama kawaida.”

Miaka minne imepita tangu Kikundi Kazi kiwasilishe mapendekezo yake Ikulu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kutekeleza mapendekezo hayo. Aidha, licha ya msimamo wa majaji Luanda na Ramadhani kuwa na umri wa takriban miaka saba, utaratibu wa uteuzi wa majaji wastaafu haujaachwa na mamlaka husika ya uteuzi. Ajira ya sasa ya Jaji Kiongozi Fakih Jundu iko katika kundi hili la watu wasiokuwa Majaji kwa mujibu wa Katiba.

JAJI KIONGOZI FAKIH JUNDU

Jaji Kiongozi Fakih Jundu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Rais Mkapa mwaka 2003. Julai 29, 2009, Jaji Jundu wakati huo akiwa Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Iringa, alitoa taarifa ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, mara baada ya kutoa taarifa hiyo, Jaji Jundu siyo tu alipewa mkataba wa ujaji kwa miaka mitatu, bali pia alipandishwa cheo na kufanywa Jaji Kiongozi.

Kama hiyo haitoshi, inasemekana sasa kwamba Jaji Kiongozi Jundu ameongezewa mkataba mwingine tena wa miaka miwili kuendelea kuwa Jaji Kiongozi kuanzia Julai 29, 2012! Huu ni ukiukaji wa Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Taarifa ya Kikundi Kazi, “... umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi ni miaka sitini.... Hivyo, iwapo Rais atamuongezea Jaji Kiongozi muda wa kufanya kazi, hatamuongezea kama Jaji Kiongozi.”

Kwa maana nyingine, kama ilikuwa makosa kikatiba kumpa Jaji Jundu mkataba wa ajira kama Jaji wa kawaida, ilikuwa makosa makubwa zaidi kikatiba kumpandisha cheo na kumfanya Jaji Kiongozi wakati alikwishafikisha umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi! Pili, kwa utamaduni uliozoeleka Tanzania, majaji wamekuwa wanaongezewa kipindi kimoja cha miaka miwili ili wamalizie kesi walizokuwa nazo hadi muda wao wa kustaafu unawadia. Kwa msimamo wa kikatiba ulioelezwa na Jaji wa Rufaa Luanda, Jaji Mkuu Ramadhani na Kikundi Kazi, siyo sahihi kwa Jaji Kiongozi Jundu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huo kupindukia muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba!

Nyongeza hii ya pili ya mkataba wa Jaji Kiongozi Jundu imewafanya watu wanaojiita ‘Watumishi wa Mhimili wa Mahakama’ kumwandikia Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kulalamikia jambo hilo. Kwa mujibu wa barua yao, ambayo pia ilinakiliwa kwa Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu, watu hao wamesema yafuatayo kuhusu Jaji Kiongozi Jundu: “Sisi watumishi wa Mahakama tunafahamu udhaifu mkubwa kiutendaji alionao Jaji Kiongozi wetu wa sasa. Kimsingi hamudu madaraka haya. Ipo mifano mingi ya udhaifu wa Jaji Jundu. Mfano alimhamisha hakimu kutoka kituo chake cha kazi kama adhabu kwa vile hakimu huyo alitoa maamuzi ambayo yeye hakuyafurahiya kwenye ile kesi maarufu ya kibaragashia. Ni busara za Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, ndizo zilizomsaidia hakimu huyo.”

JAJI THOMAS MIHAYO

Thomas Bashite Mihayo aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Oktoba 8, 2003. Januari 16, 2006 Jaji Mihayo alitoa notisi ya kustaafu kwa mujibu wa Katiba kuanzia Juni 8, 2006 atakapokuwa ametimiza umri wa miaka sitini. Hata hivyo, Machi 8 ya mwaka huo, Jaji Mihayo alitaarifiwa na Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete alikuwa amempa “... mkataba wa miaka miwili kuanzia Juni 9, 2006.” Mkataba huo ulifikia mwisho wake Juni 8, 2008. Hata hivyo, Jaji Mihayo alipatiwa mkataba mwingine tena wa mwaka mmoja ulioanzia Juni 9, 2008 hadi Juni 8, 2009 na baada ya hapo hakupatiwa mkataba mwingine.

Inaelekea Jaji Mkuu Ramadhani alisahau msimamo wake wa awali kuhusu ajira za mikataba kwani ndiye aliyependekeza Jaji Mihayo “... apewe mkataba mwingine wa mwaka mmoja...” Na wala si Jaji Mihayo pekee aliyepatiwa au kuongozewa mkataba katika mazingira tatanishi kama haya. Kwa mujibu wa nyaraka za Idara Kuu ya Utumishi, Jaji Donasian Mwita alipatiwa mkataba wa ujaji Juni 28, 2004. Mkataba huo wa miaka miwili ulianza kutumika Julai 1, 2004. Vile vile, Jaji Joseph Masanche alisaini mkataba wa aina hiyo hiyo na Idara Kuu ya Utumishi ulioanza kutumika kuanzia Machi 7, 2006.

MAADILI YENYE SHAKA

Msemaji wa Kambi hakuzungumzia masuala yanayohusu maadili ya majaji. Hata hivyo, kutokana na mjadala uliojitokeza ndani na nje ya Bunge kutokana na hotuba yake, ushahidi umepatikana unaoonyesha kwamba baadhi ya majaji wameteuliwa bila ya kwanza kuwafanyia uchunguzi juu ya maadili yao.

MAJAJI KASSIM NYANGARIKA NA ZAINAB G. MURUKE

Kassim Nyangarika alikuwa wakili wa kujitegemea na wakili mwenza wa Jaji Kiongozi Jundu kabla ya uteuzi wake kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2003. Kama wakili, Bwana Nyangarika aliwahi kumwakilisha mlalamikaji katika kesi ya Peter Muti dhidi ya CIELMAC Ltd., Kesi ya Madai Na. 314 ya 2003 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Katika kesi hiyo mteja wa wakili Nyangarika alishinda.

Hata hivyo, kufuatia rufaa dhidi ya uamuzi huo, Mahakama Kuu ilifutilia mbali mwenendo wa kesi hiyo baada ya kugundua kwamba Wakili Nyangarika alikuwa amefanya vitendo vyenye kuashiria uvunjifu mkubwa wa maadili. Kwa mfano, Mahakama Kuu iligundua kuwa Wakili Nyangarika alimwelekeza hakimu – kwa kutumia ‘kipande cha karatasi cha rafu na kilichoandikwa kirafiki’ - namna ya kuendesha kesi hiyo. Mahakama Kuu iligundua makosa makubwa zaidi ya hilo. Kwa mujibu wa Jaji Kalegeya, “... kulikuwa na mawasiliano yasiyokuwa rasmi kati ya Mahakama na Wakili.” Jaji Kalegeya alikuta ushahidi wa uwezekano mkubwa kwamba Wakili Nyangarika ndiye aliyeandaa uamuzi wa Mahakama katika kesi hiyo. Aidha, Mahakama Kuu iligundua kwamba Wakili Nyangarika “... aliielekeza Mahakama kutokutoa uamuzi kwa tarehe iliyopangwa badala yake aliielekeza itoe uamuzi huo tarehe nyingine.”

Kwa mujibu wa Jaji Kalegeya, kama kilichoonyeshwa katika mawasiliano ya Wakili Nyangarika na Mahakama ya Wilaya kilikuwa cha kweli basi “... utoaji haki katika Mahakama hiyo uko katika hatari kubwa kama sio jina la Mahakama yote, kitu kinachohitaji marekebisho ya haraka.” Kwa sababu hiyo, Jaji Kalegeya alielekeza kwamba “mamlaka husika zichukue hatua za kufichua ukweli kuhusu barua ya Wakili Nyangarika ya tarehe 18/03/2004.” Hukumu na maelekezo ya Jaji Kalegeya yalitolewa tarehe 22 Julai, 2005. Miezi saba baadaye, Wakili Nyangarika aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania!

Wakili mwingine mwenye maadili ya mashaka yanayofanana na ya Jaji Nyangarika ambaye pia ameteuliwa Jaji Mahakama Kuu ni Zainab Muruke. Kama wakili, Zainab Muruke alimwakilisha Stephen Hill Forwood ambaye alikuwa amepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili bila faini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu. Baadaye kampuni ya mawakili ya Z.G. Muruke & Co. Advocates iliwasilisha Hati ya Mapitio (Memorandum of Review) katika Mahakama hiyo hiyo ikiomba Bwana Forwood abadilishiwe hukumu.

Ombi hilo lilikubaliwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Kabuta na tarehe 26 Julai, 2004, Bwana Forwood akabadilishiwa adhabu kuwa faini ya shilingi 20,000 au kifungo cha miaka miwili. Jambo hili liliripotiwa kwa Jaji Kiongozi ambaye aliamuru uchunguzi ufanywe uliopelekea kushushwa cheo cha Hakimu Mkazi Kabuta. Jaji Kiongozi pia aliamuru Wakili Muruke atoe maelekezo ya ushiriki wake katika sakata hilo. Hiyo ilikuwa tarehe 14 Desemba, 2004. Mwaka mmoja na miezi miwili baadaye, Zainab Muruke aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

MAJAJI PELAGIA B. KHADAY NA PATRICIA FIKIRINI

Bi. Pelagia B. Khaday ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliyeteuliwa mwaka 2009. Kabla ya uteuzi huo Bi. Khaday alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kabla ya hapo alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu na Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Agosti 12, 2004, alipewa taarifa ya kusimamishwa kazi kama Msajili wa Wilaya na kuhamishiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na ‘uzito wa shutuma’ zilizotolewa dhidi yake kwa Jaji Mkuu.

Taarifa hiyo iliandikwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Edward Rutakangwa, kwa maelekezo ya Jaji Mkuu na ilieleza kwamba Bi. Khaday alikuwa anatuhumiwa kwa “kuwashinikiza au kuwashawishi baadhi ya mahakimu mkoani Arusha kushughulikia au kuamua kwa upendeleo mashauri yaliyowahusu ... jamaa au rafiki zake”; na “kuwaandalia sababu za rufaa baadhi ya washitakiwa waliotiwa hatiani na mahakama za mahakimu hapa mkoani.”

Kabla ya kumsimamisha Bi. Khaday kazi, Jaji Mfawidhi Rutakangwa alikuwa amemteua Mheshimiwa Jacob Somi, wakati huo akiwa Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, kuwa Afisa Uchunguzi (Enquiry Officer) ili kuchunguza tuhuma dhidi ya Bi. Khaday. Taarifa ya Uchunguzi wa Awali ya Afisa Uchunguzi Somi inasema kwamba Bi. Khaday alikuwa amelalamikiwa na mahakimu kwa kuwashinikiza ili watoe maamuzi ya kesi zilizokuwa zinawakabili jamaa au marafiki zake.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Hakimu Mkazi Elvin Mugeta “alikiri kuwa-approached na Bi. Khaday ili atoe hukumu ya upendeleo kwa mshtakiwa Richard Bareto ambaye inasadikiwa kuwa ni jamaa wa rafiki yake wa karibu.” Ijapokuwa Bi. Khaday alikanusha kufanya hivyo, Afisa wa Uchunguzi Somi aliridhika kwamba “Bi. Khaday alikuwa amejiwekea utaratibu, kama alivyodai mwenyewe, wa kuwasiliana na Mahakimu kwa lengo la kuwafahamisha pamoja na mambo mengine malalamiko yaliyokuwa yakimfikia dhidi yao ili kuwanusuru wasiharibikiwe.”

Hata hivyo, Afisa Uchunguzi Somi aliridhika kwamba “utaratibu huu ulikuwa kero kwa mahakimu pale alipoutumia kwa kushinikizwa na jamaa zake na/au rafiki zake kwa lengo la kupata maamuzi ya upendeleo. Kitendo cha kumtoa mahakamani Hakimu kwa lengo la kutaka kujua hatima ya mshtakiwa Bareto aliyekuwa asomewe hukumu siku hiyo, ni mfano wa matumizi mabaya ya utaratibu huo.”

Afisa Uchunguzi Somi hakupata uthibitisho wa madai ya Bi. Khaday kuwaandalia sababu za rufaa washtakiwa waliotiwa hatiani. Hata hivyo, kwa mujibu wa Taarifa yake, “... sikuridhishwa na utaratibu wake wa kupeleka nakala ya hukumu kwa Bi. Mushi na kumtaka aisome ili kuona kama kuna uwezekano wa mshtakiwa Hussein Ramadhani Kitema kukata rufaa Mahakama Kuu baada ya kufungwa jela na Bw. Mugeta.” Afisa Uchunguzi Somi alipendekeza kwamba Bi. Khaday – “ambaye ni mtumishi wa Mahakama kwa kipindi kisichopungua miaka 20...” - apewe nafasi ya kujirekebisha.

Baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi, Jaji Mfawidhi Rutakangwa alimteua Mh. Samuel Karua, Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, kuwa Investigation Officer. Tarehe 23 Februari 2007, Investigation Officer Karua aliwasilisha Taarifa ya Uchunguzi wake kwa Jaji Mkuu. Taarifa ya Investigation Officer Karua ilimkosha Bi. Khaday kwa tuhuma zote dhidi yake.

Hata hivyo, Taarifa ya Investigation Officer Karua ina maeneo mengi yanayoleta mashaka. Kwanza, kama Investigation Officer Karua mwenyewe alivyosema, shahidi muhimu katika uchunguzi wake alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mushi. Vile vile, shahidi huyu alikuwa ‘star witness’ katika uchunguzi wa awali mbele ya Afisa Uchunguzi Somi na ndiye aliyetoa ushahidi wa yeye na mahakimu wengine kuingiliwa katika kazi zao na Bi. Khaday.

Hata hivyo, mbele ya Investigation Officer Karua, shahidi huyu muhimu alikana kila kitu alichokisema mbele ya Afisa Uchunguzi Somi. Kwa kiasi kikubwa, Investigation Officer Karua aliitumia about turn hii kumkosha Bi. Khaday dhidi ya tuhuma zote zilizokuwa zinamkabili. Cha kushangaza ni kwamba Investigation Officer Karua hakujiuliza na hakumuuliza shahidi huyu sababu za kukana ushahidi wote alioutoa mbele ya Afisa Uchunguzi Somi.

Je, alirubuniwa au kutishwa ili amsaidie Hakimu na mtumishi mwenzake katika Mahakama ya Tanzania asifukuzwe kazi? Kama sio hivyo, je, ni sababu zipi zilizomfanya shahidi huyu muhimu kubadili ushahidi wake kwa kiasi hicho? Je, ushahidi alioutoa shahidi huyu mbele ya Afisa Uchunguzi Somi ulikuwa wa uongo? Na kama ulikuwa wa uongo, ushahidi wake wa pili kwa Investigation Officer Karua ni wa kweli kiasi gani mpaka kumfanya Investigation Officer Karua kutamka kuwa shahidi huyu ‘anaweza ... kuwa anasema ukweli.’

Inaelekea Investigation Officer Karua, Hakimu Mkuu Mkazi mwenye uzoefu wa miaka mingi katika Mahakama, alifanya kazi yake kwa mtazamo wa kimahakama zaidi badala ya kutumia mtazamo wa kiupelelezi na/au kiuchunguzi ambayo hasa ndiyo ilikuwa kazi yake katika uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Bi. Khaday. Kwa mtazamo wa kimahakama, ukweli kwamba shahidi muhimu kama Hakimu Mkazi Mfawidhi Mushi alikana ushahidi wake wa awali mbele ya Afisa Uchunguzi Somi ilikuwa inatosha kumfutia Bi. Khaday hatia yote. Kwa mtazamo wa kiupelelezi/kiuchunguzi, about turn ya shahidi huyu ingemfanya Investigation Officer Karua kuchunguza zaidi sababu za kigeugeu hicho.

Pili, Investigation Officer Karua hakuipa uzito wa kutosha Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi. Kwa mfano, Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi – yenye kurasa 14 zilizochapwa - imeelezewa katika Taarifa ya Investigation Officer Karua kwa aya moja tu! Kwa sababu hiyo, ni vigumu kukubaliana na Investigation Officer Karua kwamba Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi ‘ilikuwa muhimu sana’ wakati umuhimu huo haujafafanuliwa wala kuelezewa hata kidogo katika Taarifa yake.

Aidha, Investigation Officer Karua alitakiwa kueleza sababu za kutofautiana na Afisa Uchunguzi Somi kwamba Bi. Khaday alikuwa anakera mahakimu kwa kuwasiliana nao baada ya kushinikizwa na ndugu au rafiki zake ili wapatiwe upendeleo katika kesi zilizokuwa zinawakabili. Investigation Officer Karua hakufanya hivyo. Vile vile, Investigation Officer Karua hakuona ajabu wala kujiuliza kama ilikuwa ni kitu cha kawaida kwa Bi. Khaday kumleta Richard Bareto – mshtakiwa aliyehusishwa na shinikizo la Bi. Khaday kwa Hakimu Mkazi Mugeta – kama shahidi wake wa utetezi.

Tatu, Investigation Officer Karua hakutoa sababu za maana za kutochukua ushahidi wa mahakimu wengine waliodaiwa kushinikizwa na Bi. Khaday. Katika aya moja tu iliyowahusu mahakimu hao, Investigation Officer Karua alisema kwamba siku ya kutoa ushahidi wao kwake, watu hao “... walishikilia msimamo wa kauli walizotoa mbele ya Bwana Somi ... na baada ya tafakuri ya muda ... mashahidi hawa waliachiwa.”

Mbele ya Afisa Uchunguzi Somi, mashahidi hawa wawili, Hakimu Mkazi Msumi na Hakimu Mkuu wa Wilaya Mlay, walikuwa wamesema kwamba “... huko nyuma (Bwana Msumi) aliwahi kuitwa na mlalamikiwa baada ya wadhamini walioshindwa kukidhi masharti ya dhamana ... kumpelekea malalamiko ya kukataliwa dhamana, maelezo ambayo hayakuwa na ukweli wowote.” Aidha, kwa mujibu wa Afisa Uchunguzi Somi, “... katika hali isiyokuwa ya kawaida Bw. Mlay, PDM hakuwa tayari kueleza kilichomsibu hadi kujiengua katika usikilizaji wa kesi ambayo Bi. Mushi alidai ilikuwa inamkabili rafiki yake wa karibu na Bi. Khaday.” Investigation Officer Karua hakuona sababu yoyote ya kufuatilia ushahidi wa mahakimu hawa wawili!

Nne, Investigation Officer Karua anakubali kwamba hali ilikuwa tete katika Kituo cha Arusha: “Inaelekea mtuhumiwa alikuwa na mahusiano mabaya na baadhi ya mahakimu.” Kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, Investigation Officer Karua alikuwa na wajibu wa kuchunguza chanzo cha mahusiano hayo mabaya, hasa kwa vile kulikuwa sio tu na tuhuma bali pia ushahidi wa mahakimu husika kwamba Bi. Khaday alikuwa anawaingilia mahakimu katika kazi zao. Hakufanya hivyo. Badala yake Taarifa ya Investigation Officer Karua inaonekana kama jitihada za kumkosha Bi. Khaday dhidi ya tuhuma nzito za ukosefu wa maadili ya kimahakama. Jitihada hizi zilifanikiwa kwani miaka miwili baada ya Taarifa ya Investigation Officer Karua, Bi. Khaday aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Na wala siyo Bi. Khaday pekee aliyeneemeka na taarifa hiyo. Bi. Patricia Fikirini, ambaye Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi inamwelezea kama mmoja wa mahakimu waliosikiliza kesi ya mfanyabiashara maarufu wa Arusha, Justin Nyari iliyokuwa chanzo cha tuhuma dhidi ya Bi. Khaday – alihusishwa na tuhuma dhidi ya Bi. Khaday kwa maneno yafuatayo: “... Kama mtawala ... (Bi. Khaday) ... alisema aliwahi, tena kwa nia njema, kumweleza Bi. Fikirini ... kuhusu uvumi kwamba mume wake alikwenda gerezani na kuchukua mamilioni ya fedha kwa Bw. Nyari na hivyo kumshauri awe mwangalifu zaidi”! Katika uteuzi wa majaji uliofanywa na Rais Kikwete mwezi Juni mwaka huu, Bi. Patricia Fikirini naye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Wapo wanaoweza kusema kwamba Bi. Khaday hakupatikana na hatia yoyote na kwa hiyo haikuwa makosa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Aidha, inaweza kudaiwa kwamba Bi. Fikirini hajawahi kutuhumiwa kwa kosa lolote la maadili na kwamba ‘uvumi’ pekee hautoshi kumnyima mtu mwenye sifa haki ya kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kwa wenye hoja za aina hii jibu langu ni kwamba kiwango cha ‘sifa maalum’ kinachotakiwa na Katiba kwa mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ni mtu ambaye “... kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu....” Kiwango hiki ni cha juu kiasi kwamba kutokuwa na hatia pekee haitoshi kumfanya mhusika kuwa ‘kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.’ Kwa maoni yangu, mtu aliyeundiwa uchunguzi wa kimaadili au ambaye kuna uvumi unaomhusisha na rushwa ‘hafai kwa kila hali’ kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu. Majaji Khaday na Fikirini wapo kwenye kundi hili.

JAJI ALOYSIUS MUJULIZI

Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishirini walioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili ya Ishengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam. Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocates vile vile walikuwa mawakili wa Tangold Ltd.

Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishia mabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na 2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya Tangold Ltd. ililipwa dola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyaraka zilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana wa Benki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwamba Tangold Limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Haya yote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates.

‘SIFA MAALUM’ ZENYE SHAKA

JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK

Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba: “Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.”

Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984, “mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba.” Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba. Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.

Uteuzi wa Jaji Mbarouk kuwa Jaji wa Rufaa ulileta minong’ono mingi katika taaluma ya sheria kiasi kwamba marehemu Wakili Leopold Kalunga anasemekana kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka uteuzi huo utenguliwe. Hata hivyo, Wakili Kalunga alifariki kabla ya shauri lake kusikilizwa na kwa hiyo liliondolewa mahakamani. Aidha, monong’ono hiyo ilimfanya Jaji wa Rufaa Mbarouk kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambako bado ni mwanafunzi hadi ninapoandika Addendum hii.

MAJAJI ‘WALIOTOLEWA MITAANI’

Katika Maoni ya Kambi tulidai kwamba “... sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na - kwa sababu hiyo - hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba....” Ukiacha uteuzi wa Jaji wa Rufaa Mbarouk ambao haubanwi na masharti ya Ibara ya 109(1) na 113(1)(a) ya Katiba, majaji wengine waliotajwa kwenye Addendum hii hawakupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Majaji wengine ambao pia hawajawahi kupendekezwa na Tume hiyo ni pamoja Fatuma Massengi, Mary Sumari, Imani Mkwawa-Aboud na Sekela Mushi.

Friday, August 10, 2012

Papaa Msoffe ashitakiwa kwa mauaji.

Papaa musoffe akiingia Mahakamani
 
HATIMAYE mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe maarufu kwa jina la “Papa Msofe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi ya mauji.

Wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome alidai kuwa Msofe ambaye ni mkazi wa Mikocheni,anakabiliwa na kosa moja la mauji ambalo ni kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.


Papaa akiingizwa kwenye rejesta
Wakili Kweka alidai kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe anayetetewa na wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kitoli na kwamba upelelezi wa kesi ya hiyo bado haujakamilika.

Kwa upande wake hakimu Mchome alisema kesi hiyo ambayo ipo mbele yake ni mauaji na mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ni Mahakama Kuu hivyo akamtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote.

“Kwa sababu hiyo naiarisha kesi hii hadi Agosti 23 mwaka huu, kesi hii itakuja kwaajili ya kujatwa na kwa kuwa kesi hii haina dhamana naamuru mshitakiwa apelekwe gerezani”alisema Hakimu Mchome.

Msofe ambaye alifikishwa kwenye eneo la mahakama hii jana saa 3:30 asubuhi chini askari kanzu watatu ambao mmoja alikuwa amebeba silaha na kisha kumuingiza kwenye selo ya mahabusu hiyo kwaajili ya kumuifadhi hadi ilipofika saa tano saa asubuhi mshitakiwa huyo aliingizwa kwenye chumba namba tisa cha mahakamani hapo na kuanza kusomewa maelezo yake huku ndugu na jamaa zake walikuwa wamefika mahakamani hapo kwaajili kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao.

Msofe ambaye jina lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo zinazopigwa na Bendi za Miziki ya Dansi nchini ikiwemo Bendi ya FM Academia na Acudo Impact aliletwa na askari kanzu hao akitokea kwenye sero ya jeshi la polisi ambako kwa zaidi ya wiki moja sasa alikuwa akiishi ndani sero hiyo ya polisi kwaajili mahojiano na mshitakiwa huyo na hatimaye jana akafikishwa mahakamani hapo kwa kesi ya mauji.

Papaa akirudishwa Mahabusu
Itakumbukwa hivi karibuni mjane mmoja aishie Mbezi Beach alilalamika kupitia vyombo vya habari kuwa Papa Msofe anataka kumdhuru nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe wake kupitia vyombo vya habari, hali iliyosababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati sakata hilo na hatimaye mjane huyo akarudishiwa nyumba yake aliyokuwa akidai Msofe anataka kumdhurumu.

Aidha itakumbukwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Papa Msofe kufikishwa katika mahakama hiyo kwa makosa mbalim




Thursday, August 9, 2012

Malawi Kuishitaki Tanzania Mahakama ya Kimataifa.

Waziri wa MaMambo ya Ndani wa Malawi; Nd.Uladi Musa
 
MALAWI imesema imeondoa ndege zake zilizokuwa zikifanya utafiti wa mafuta katika Ziwa Nyasa kwa kuwa haitaki kuingia vitani, badala yake imeamua kupeleka mgogoro huo Mahakama ya Kimataifa,
Mgogoro baina ya Malawei na Tanzania hivi karibuni uliingia katika hatua nyingine, baada ya Serikali ya Tanzania kuiagiza Malawi kuondosha ndege zilizokua zinafanya utafiti wa mafuta katika eneo lake. Waziri wa Tanzania wa Mambo ya Nje Bernard Membe aliliambia Bunge huko Dodoma  kwamba lazima Malawi iache mipango yake ya kuchunguza mafuta katika ziwa nyasa na kukiita hicho ni  kitendo cha uchokozi.
            
Malawi iliingia mkataba na Kampuni ya Uingereza Surestream mwaka jana kufanya utafiti katika  maeneo ya ziwa  nyasa ambapo  inaaminika kuwa na mafuta na gesi kwa wingi.Hoja ya Tanzania katika mgogoro huu ni kwamba katika sheria za kimataifa  ni kwamba iwapo  nchi mbili zinatengwa  maji, mpaka ni katikati ya  maji hayo na kwamba, Tanzania inapinga umiliki wa Malawi kwa asilimia mia katika ziwa nyasa.

Waziri wa Usalama wa Ndani  wa Malawi Uladi Mussa anasemaje?

Waziri wa Malawi ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Ndani, Uladi Mussa, akizungumza na Zodiak Broadcasting Station (ZBS) siku ya Jumanne aliimiza watu katika wilaya mbili za Karonga na Chitipa zinazopakana na Tanzania kubakia shwari kwakua  hakuna kitu ambacho kingetokea.

"Mimi lazima kuwahakikishia watu wote katika nchi hii kubakia shwari. Sisi tuzungumza na serikali ya Tanzania na mambo yote tatakua  mazuri.  Ikishindikana  sisi tutalipeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa ya Haki, " alisema Waziri huyo.Waziri huyo alisisitizakwamba ziwa yote ni ya Malawi na kuongeza kwamba serikali ina ushahidi wa kuthibitisha hatua yake.

"Hakuna suala hapa. Sisi wote tunajua ziwa ni letu. Kwa kweli kama madai kama hayo yangekuja  kutoka Msumbiji angalau ingekuwa inaleta maana  kwa kiasi fulani lakini si Tanzania. Tuna ushahidi wa mikataba kuonesha kwamba Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi, "alisema Waziri wa Mambo ya Ndani.

Hoja ya Malawi.

Serikali  ya Malawi inasema kwamba hoja ya  kwa Tanzania-kwamba ziwa litakua la pamoja itatumika pale  tu ambapo hakuna  mkataba lakini katika hali hii mpaka ilikuwa wazi na hasa ilivyoainishwa katika Mkataba wa 1890 Heligoland.

Aidha,  alisema kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika 1963 Wakuu wa Nchi wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) alifanya azimio kwamba nchi wanachama wanapaswa kutambua na kukubali mipaka waliokuwa rithi wakati wa uhuru.

JK aapisha vigogo wa Mahakama leo.

Balozi sifue kushoto, Jk na Vigogo wa Mahakama

Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha, Mhe. Ignas Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, kabla ya uteuzi wake Mhe. Kitusi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhe. Rais akimuapisha Mhe. Panterine Kente kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.                                               caption

Mhe. J.K akimuapisha Mhe.Hussein Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, kabla ya uteuzi wake,Mhe. Kattanga alikuwa Katibu Mkuu TAMISEMI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Costa Mahalu ashinda kesi yake.

Aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Italia,Balozi Costa Mahalu ambaye alikua mshitakiwa namba moja kwenye kesi ya matumizi mabaya ya fedha za ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia, pamoja na mshitakiwa namba mbili Grace Martin (kushoto) wakiwa wamezungukwa na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kusomewa kesi yao ambayo wameshinda leo na kuonekana hawana hatia yeyote kutoka na kukosekana kwa ushahidi uliokamilika.
Mahalu akipongezwa na jamaa yake.

Bila Shaka akisema" haki imetendeka nimeshinda kesi......"
Hongera Professor