Powered By Blogger

Monday, May 28, 2012

WENGI WAMLILIA WAKILI MAARUFU, BONIFACE STANSLAUS.


MKURUGENZI Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) 'Jembe' amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia kutokea kwa kifo hicho.  Marehemu Boniface ameacha pengo kubwa sana kwa wanaasheria hasa waliojikita katika kesi za jinai, kwa weredi wake mkubwa sana wa kudadavua, na kuendesha mashauri mbalimbali ya jinai. Yumkini, weredi wake huo ndio umepelekea mamia ya wanasheria na wadau mbalimbali kutoa maoni yao katika kurasa mbalimbali za kijamii” social networks” kuonesha maoni yao kama ifuatavyo:

MAONI YA WADAU:

Dr. Eliezer Feleshi , DPP alisema bado ofisi yake na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji huyo wa uendeshaji wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa. 


Moses Masinga, wakili msomi wa kujitegemea aliandika facebook , so sad tuliokuwa wote Law School nadhani mnamkumbuka jamaa alivyokuwa JEMBE! Aisee duniani tunapita tu. It is not easy kuamini lakini habari ni hivyo.
Kheri Mbiro, wakili msomi wa kujitegemea aliandika katika ukurasa wake wa facebook, RIP Boniface Stanslaus Makulilo,Sr. State Attorney..your passing away couldn't have been any earlier...quite a crippling blow to the Attorney General's Chambers...indeed many of us never ceased to pick a trick or two up your sleeves whenever you stood up in court...."An authority"..for many..its saddening but the Lord's wishes are unquestionable...we pray for your soul....amen.
Innocent Mhina mwanasheria na wakili wa bank ya posta aliandika;jamaa alikua exta ordinary attorney principles nyingi sana zimetoka kwenye cases alizo argue yeye na zingine kwa kuomba muongozo wa mahakama ususani kwenye ishu ya inquiry at subordinate crts at wht tme iwe conducted and how,.cheki kesi ya seleman abdalah v/s republic you will appreciate him and not only that alikua mwalimu mzuri sana
 
Jerry Muro ambae bwana Boniface aliwahi kuendesha kesi yake alisema, R.I.P boniface stanslaus,naibu mkurugenzi wa mashtaka alikuwa mwendesha mashtaka wa serikali kny kesi yangu,japo nilishinda kesi ila alitoa changamoto kny kesi yangu haswa.
WASIFU WAKE:

Boniface alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahaha ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.

Nyadhifa ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka 2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.Kati ya Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mwanza.Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri ilipofika Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma.


                                       KESI KUBWA ALIZOZIMAMIA;

Miongoni mwa kesi kubwa ambazo mwandishi wa habari hizi amekuwa akimshuhudia akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa nchini

  • sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka jana, iliwahukumu kwenda jela miaka mitano.
  • kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka jana.
  •  kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara Jayankumar Patel "Jeetu Patel' na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.
  • Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja. 

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Boniface mahali pema peponi.Amin.

MAAMUZI YA KESI YA LULU KUSIKILIZWA JUNI 16.


Lulu akiwa Mahakamani
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba Lulu akiwa mahakamani hapo.Lulu akiwasili Mahakamani hapo.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.

Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.

Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.

Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.

Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.Baada ya kusikiliza mabishano hayo
ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.

 
kwani Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 Pamoja na Sheria ya watoto ya mwaka 2009,  suala la umri lina mantiki kubwa sana ya kisheria, kwani mfumo wa kusikilizwa kwa kesi za watoto wenye makosa mbalimbali ya jinai” Children in conflicting with the Laws” pamoja na adhabu zao ni tofauti na ule wa kesi za watu wazima. Chanzo Michuzi Blog.

Wednesday, May 23, 2012

Daktari aliyefanikisha kuuawa kwa Osama, ahukumiwa miaka 33 kwa Uhaini.


Dr. Afridi Shakeel
 
Daktari wa Pakistani ambae aliisaidia Marekani kubaini uwepo wa   Osama bin Laden nchini Pakistani amehukumiwa kifungo cha miaka 33 jela      kwa   kosa la       uhaini.

Dokta Afridi Shakeel alishitakiwa kwa kufanya kampeni bandia ya chanjo ya kusaidia CIA kupata sampuli ya DNA ya kiongozi wa al-Qaida na watu wa familia yake ili kuthibitisha uwepo wake katika katika mji huo wa Abbottabad, Pakistan.



Vikosi vya maalum vya Marekani vilimuua bin Laden wakati wa uvamizi uliyofanyika mwaka mwezi wa mei.

Maafisa wa serikali walisema kuwa mahakama ya kikabila iliyopo  kaskazini magharibi ya Pakistan Khyber ilimtia hatia Afridi kwa kosa la  uhaini. Mbali na kutumikia kifungo hicho cha  jela, daktari huyo pia atalazimika kulifaini ya $3,500.Maafisa wanasema kuwa chini ya mfumo wa kikabila, Afridi hakupewa haki ya kujitetea, au kupata mwanasheria.

Mapema mwaka huu, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta alisema Afridi alitoa msaada mkubwa sana katika kufuatilia uwepo wa bin Laden  nchini Pakistani hivyo kutoa wito kwa mamlaka ya Pakistan ya kumwachilia. Alisema Afridi angeweza kutoroka Pakistan kabla ya kukamatwa, lakini alichagua kukaa kwa sababu alikuwa na uzalendo.

Alipoulizwa kuhusu hukumu ya  Afridi wa, Msemaji wa Pentagon  George Little aliwaambia waandishi wa habari: " mtu yeyote ambaye amesaidia au kutiamkono Marekani katika kumtafuta Osama bin Laden hastaili kua na kosa kwa kua haikuwa kazi dhidi ya Pakistan bali Walikuwa wakifanya kazi dhidi ya al-Qaida.

Kifo cha Osama bin laden kwa namna moja au nyingine kimefifisha mahusiano ya kidemokrasia kati ya Marekani na Pakistani.

Tuesday, May 22, 2012

RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI WA RUFANI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama yaRufani.

Walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012.

Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000.

Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004

Saturday, May 19, 2012

SERIKALI YAANZA MCHAKATO WA KUANDAA MFUMO WA WASAIDIZI WA SHERIA (PARALEGALS)


Mh. Naibu waziri wa Katiba na Sheria  Kulia akiteta jambo nje ya ukumbi wa Bunge( Picha ya Maktaba)
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki, wakati alipokutana na Wanaharakati wa Kisheria wa Asasi zisizo za Kiserikali ofisini kwake jijini Dar-Es-Salaam. Mhe. Kairuki amesema kuwa mchakato huo utakapokamilika utawezesha  Wasaidizi wa Sheria kutambuliwa na sheria husika na hivyo kupanua wigo kwa wananchi wa mijini na vijijini kuwa na msaada wa kisheria wanapopatwa na matatizo.“Natambua umuhimu wa uundwaji wa Sheria hii ya Paralegals ndio maana tumeanza mchakato huu kwa kuufanyia marekebisho na kueleza dhana nzima ya Palalegals,” Alisema.

Amewataka Wanaharakati hao kuendelea kuwasisitiza Wasaidizi wa sheria  kuhakikisha kuwa wanatoa Huduma zao kwa uwazi zaidi ili wananchi waweze kufaidika hiyo.Amesema Serikali itahakikisha kuwa inaweka mazingira bora yatakayowawezesha   Wasaidizi wa Sheria kufanya kazi zao vizuri lakini kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Haki za Binadamu.

Wanaharakati hao wamesema kuwa mpaka sasa Wasaidizi wa Sheria (Paralegals) bado hawajatambulika kisheria na kwamba sheria haitoi nafasi kwa Mawakili wa Serikali au wa kujitegemea kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo na Mabaraza ya Kikata maeneo ambayo ndiyo yenye matatizo makubwa ya kisheria kwa wananchi wa kawaida.

Akizungumza kwenye mkutano huo Wakili wa Kujitegemea Bw. Alphonse Katemi amesema wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu mfumo wa kisheria hauruhusu kwa Mawakili kutoa huduma za kisheria katika Mahakama za mwanzo na Mabaraza ya Kata. “Kwa hiyo ni suala ambalo kwa kweli wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu ni mfumo wa kisheria mawakili kwenye mabaraza haya ya ardhi    hawaruhusiwi,” Alisema Katemi na kuongeza kuwa huko ndiko kwenye maeneo ambayo yanawatesa sana na kuwaumiza wananchi wa nchi hii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasadizi wa Sheria Bi. Flora Masoy amesema kuwa endapo hao Wasaidizi wa Sheria watawezeshwa kutambulika ni wazi kuwa ata kazi zao wanazozifanya nazo zitatambulika kisheria.Wamesema iwapo Wasaidizi hao watatambulika kisheria itawasaidia kutoa huduma za kisheria hasa kwa wananchi waliopo vijijini ambao ndio wengi wanaokabiliwa na uelewa mdogo wa haki zao.“Wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini wanashindwa kupata huduma za kisheria vizuri kutokana na kutokuwepo na watoaji wa kutosha wa huduma za kisheria,” Alisema mmoja wa Wanaharakati.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph Ndunguru, amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Paralegals Serikali imeandaa Waraka wa Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutunga sheria ambayo lengo kuu kuwatambua Wanasheria Wasaidizi.  Amesema katika mchakato huo wa kuandikwa kwa sheria hiyo Serikali itahakikisha kuwa inawashirikisha wadau mbalimbali katika kupata mawazo mapya yatayowezesha wananchi kupata msaada wa kisheria. Chanzo Michuzi blog.

Monday, May 7, 2012

UMRI WA LULU WALETA MVUTANO KORTINI

Mojawapo ya Picha za Lulu, akipelekwa Kotini

UMRI wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba jana ulizua utata katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mawakili wanaomtetea kutaka kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo ili akashtakiwe kwenye Mahakama ya Watoto.

Kesi hiyo ilitajwa jana huku mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Keneth Fungamtama, wakiwasilisha maombi kuhusu suala hilo la umri wa mteja wao wakitaka asishtakiwe mahakamani hapo kama ilivyo sasa. Fungamtama ambaye alikuwa akisaidiana na Mawakili Peter Kibatala na Fulgence Masawe, alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 17 hivyo, kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Watoto. “Mshtakiwa ana umri wa miaka 17 na tuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa,” alidai Fungamtama.

Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18. Wakili huyo aliendelea kunukuu vifungu mbalimbali vya Sheria ya Mtoto kama 98 (i) na 114 (ii), ambavyo alidai kuwa vyote vinawapa nguvu ya kuwasilisha maombi yao hayo ya kuihamisha kesi hiyo. “Hata katika suala la Mahakama, vifungu vyote vya sheria hii vimefafanua, hivyo tunawasilisha maombi yetu kwamba mteja wetu ana umri wa miaka 17 na shauri hili lingepaswa kusikilizwa Mahakama ya Watoto,” alidai.

 Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliomba wapewe muda zaidi kwa sababu bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo. “Kesi hii imekuja mahakamani hapa kama ya mauaji na upelelezi bado haujakamilika. Tunaposema haujakamilika, tunapeleleza kila kitu, likiwamo suala la umri,” alieleza Kaganda. Alisema hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa kilichowasilishwa mahakamani hapo, linasomeka Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo, kwa jina la Elizabeth Michael. “Tunaomba muda tuweze kuchunguza kuhusu umri wa mshtakiwa kwa sababu aliwaeleza polisi kwamba ana umri wa miaka 18 halafu mawakili wake wanakuja kueleza hapa mahakamani kwamba ana umri wa miaka 17,” alidai Kaganda. Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kutokana na mvuto wa kesi hiyo katika jamii, wanaomba wapewe muda zaidi kufanya upelelezi ili kumtendea haki mshtakiwa huyo.

 Kuhusu cheti hicho kusomeka Diana Elizabeth, Wakili Fungamtama alikiri na kudai kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili. Fungamtama alidai kuwa hawana pingamizi na maombi ya upande wa mashtaka kwamba wapewe muda zaidi wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa, ingawa alidai kuwa suala hilo halina ugumu. Akitoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mkazi Augustina Mbando alisema: “Mahakama imesikiliza maombi yaliyoletwa na Fungamtama na Kaganda na imeona kesi iliyopo hapa ni ya mauaji na jinsi kesi hii ilivyo, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika.”

“Kama defence (upande wa utetezi) wana maombi yoyote wanaweza kufanya hivyo kupitia Mahakama Kuu,”.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapotajwa tena. Inadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam msanii huyo wa kike, alimuua Kanumba. Jana Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 2:50 asubuhi akiwa peke yake kwenye gari linalobeba mahabusu, huku akisindikizwa na magari mengine mawili.

Alipoingia mahakamani alikuwa amezingirwa na askari Magereza na Polisi zaidi ya 10 na kuufanya  umati mkubwa wa watu uliofurika mahakamani hapo kushindwa kumwona. Miongoni mwa watu waliofika mahakamani hapo jana ni baba mzazi wa msanii huyo, Michael Kimemeta na ndugu zake wengine kadhaa. chanzo Gazeti la Mwananchi.  

MTAZAMO WANGU KATIKA DHANA KWAMBA RAIS AMEVUNJA KATIBA KATIKA UTEUZI WAKE WA MAWAZIRI


Siku chache zilizopita Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliteua Baraza lake la mawaziri.Baraza hilo limekuja baadbaadhi ya mawaziri, kushutumiwa kwa utendaji mbovu wa shughuli zao na kila siku na kutumia mamlaka yao aidha kujinufaisha au kufisadi mali ya Umma. Kimsingi,lengo langu si kudadisi kwa kina sababu zilizopelekea Mh.Rais kufanya mabadiliko hayo. Nimehamasika kuandika suala hili baada ya vyombo mbalimbali vya habari, wanazuoni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kua namaoni tofauti, wengine wakienda mbali sana na kusema Rais amevunja kaika kwa kuwachagua baadhi ya Mawaziri kushika wadhifa huo wakati wao si wabunge. Niseme kwamba katika maoni yangu hayo nitarejerea Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(1977), kama "Katiba".

Kimsingi, nikiwa Mwanasheria nimeona si vibaya nikitoa mawazo yangu katika mkanganyiko huu ambapo jamii isiyo na uelewa wa kisheria” layman”, huweza kukumbwa na mkanganyiko usiostahili katika jambo hili. Mfano katika gazeti la mtanzania la leo Jumapili, lilimnukuu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) likiwa na kichwa cha habari” MBOWE AMSHUKIA JK, ADAI AMEVUNJA KATIBA UTEUZI WA MAWAZIRI”. Katika gazeti hilo lenye namba. ISSN 0856-5678 Toleo Na. 6049, gazeti hilo lilimnukuu Mh.Mbowe akisema mafuatayo,” inasikitisha Kuona Rais anaendesha nchi kihuni na kuvunja kwa makusudi Katiba,wakati akifahamu kuwa hawezi kumpa mtu uwaziri bila kuapishwa ubunge na kwamba kwa hatua hiyo Rais Kikwete ameridharau bunge.

Niaze kueleza kwamba Ibara ya 66(1) e kinatoa Mamlaka ya Kikatiba kwa Rais kuteua wabunge wasiozidi 10 wenye sifa atakazoona inafaa kuitumikia nafasi hiyo, sanjali na mamlaka hayo aliyopewa Rais aina nyingine ya mtu kuwa Mbunge pia zinaainishwa katika Ibara hiyo hiyo; na kwamba mtu anaweza kua mbunge kwa kuchaguliwa na wananchi au vilevile kupitia kwa viti maalum, ay nafasi aliyonayo kama ya Mwanzaasheria Mkuu wa Serikali.  Hivyo basi Uteuzi wa Rais kwa Prof. Sospether Muhongo na Bi.Jane kuwa wabunge na hatimaye uwaziri ni uteuzi wa kikatiba.

Watu wanaosema Raisi amevunja katiba, wanamaoni ya kwamba wabunge walioteuliwa na Rais kuwa mawaziri hawajaapa  kuwa wabunge kabla ya kushika na Kuteuliwa na Raisi kuwa Mawaziri. Nina wiwa kusema ya Kwamba huu ni upotoshwaji mkubwa  na pengine uelewa mdogo wa Katiba pamoja na Sheria za nchi yetu.

Kimsingi Swali la kutuongoza ni kwamba, ni wakati gani mtu anakua Mbunge? Je ni pale mtu anapotangazwa na Tume kuwa Mbunge ?AU Je ni Pale ambapo mtu anapoteuliwa na mtu mwenye mamlaka kuwa Mbunge? Au Je ni pale mtu anapokua kiapo cha Ubunge? Ni rai yangu kwamba Sura ya 343 iliyofanywa marekebisho mwaka 2002 na 2010 ,kifungu cha 98 kinasema mtu anakua mbunge pale baada ya kutangazwa na Tume ya uchaguzi kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuwa mbunge kupitia Jimbo husika, au pale mtu anapoteuliwa kwa mujibu wa Katiba kushika wadhifa huo(Kama ambavyo Rais amefanya katika Ibara ya 66(1)e). Suala la kwamba mtu huyo amekula kiapo cha kutumikia wadhifa huo wa ubunge au la! Hilo ni suala jingine. Na kuapa au kutokuapa kwa mtu huyo hakumuondolei ubunge wake( does neither disqualify him or her from holding that post nor invalidate the same). Ninachomaanisha ni kwamba Mtu anapotangazwa au kuteuliwa kuwa mbunge, mtu huyo atahesabika kuwa mbunge pale tu atakapotangazwa au kuteuliwa kushika wadhifa huo. Kwa Mfano. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni Mbunge Kikatiba kwa nafasi aliyonayo yeye kama Mwanasheria Mkuu katika Ibara ya 66(1)d na 55(5). Kama Rais akiingia Madarakani na Kumteua Mwanasheria Mkuu wa serikali, Mwanasheria huyo baada ya kuapa Kwa Rais anaanza majukumu yake kama Mwanasheria Mkuu, lakini hataanza majukumu yake kama mbunge mpaka pale atakapoanza kushiriki katika shughuli za Kibunge. Hii haina tofauti na uteuzi wa Mawaziri.

Pamoja na hayo ibara ya 68 ya Katiba inaeleza wazi kwamba, na nanukuu Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge. Kwa mantiki ya Ibara hii ni kwamba Mawaziri hao walioteuliwa na Rais ni wabunge isipokua hawawezi kushiriki katika shughuli za ubunge bila kula kiapo au pasipo kuapishwa na Bunge.  Swali la kujiuliza ni shughuli gani za bunge zinazozungumziwa na Ibara hii ya 68. Shughuli za bunge kama inavyoelezewa ni kutunga sheria pamoja na majukumu mingine ya waliyopewa Kikatiba.

Kwa upande wa Pili, Rais amepewa mamalaka ya Kikatiba katika Ibara ya 55 (1),(2),(3) kuteua Mawaziri na manaibu wao, hata hivyo mawaziri hao hawaruhusiwi kutekeleza majukumu yao ya kiuwaziri pasipo kutii masharti ya Ibara ya 56 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inayowataka Mawaziri hao kula kiapo kwa raisi kabla ya kuanza majukumu yao.  Ningekua na maoni tofauti kama, Mawaziri hao wangeanza kufanya shughuli zao za kiutendaji kama Mawaziri kabla ya kuapishwa na Rais..hapo ndipo tungesema wamekosa uhalali wa kiutendaji kama Mawaziri.

Kwa mantiki hii basi ya tafrisi ya Kikatiba ni Kwamba Mh. Rais hajafanya kosa lolote la kuwateua wabunge hao kua Mawaziri kabla ya kuapishwa na Bunge.
Ni rai yangu kwamba, Wanasiasa waache maneno ya uchochezi kupotasha raia ilikuepuka migogoro isiyokua na tija katika Taifa. Iwapo wadau wanaona ya kwamba kuna ulazima wa Mawaziri kuapishwa na Bunge kabla ya kuanza majukumu yao ya uwaziri, basi wapeleke maoni na mapendekezo yao kwenye Tume ya Mabadiliko ya Sheria kutoa maoni yao, pale Tume inapoanza kupokea maoni hayo.