Powered By Blogger

Tuesday, April 26, 2011

MREMBO MAHAKAMANI KWA KUMUIBIA AFISA WA TAKUKURU

MSICHANA Gatti Samweli (26), mkazi wa Kinondoni, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashtaka ya kumuiba Afisa wa Taasisi na Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).Mbele ya Hakimu Marko Mochiwa imedaiwa na Karani Fatma Khatibu kuwa Aprili 11, mwaka huu, mshitakiwa aliiba vitu mbalimbali vikiwemo simu za mkononi, nyaraka mbalimbali ambazo ni mali ya mlalamikaji Alex Tungombe.

Mshitakiwa amekana mashtaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 20, mwaka huu.

Pia, Abdul Hoza (30), mkazi wa jijini hapa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashtaka ya wizi.

Mbele ya Hakimu Suzan Makabwa ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Benedict Nyagabona Februari 22, mwaka huu, mshitakiwa aliiba vitu vya aina mbalimbali vyenye thamani ya sh. 128,000 mali ya mlalamikaji Siwema Mkwayu.

Mshitakiwa amekana mashtaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 21, mwaka huu.

Wakati huo huo, Ramadhani Hamis (18), mkazi wa Mburahati amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashtaka ya wizi.

Mbele ya Hakimu Hilda Lyatuu imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Benedict Nyagabona Aprili 6, mwaka huu, mshitakiwa aliiba vitu vya aina mbalimbali vyenye thamani ya sh. 208,000 mali ya mlalamikaji Polycalp Mwingiba.Mshitakiwa amekana mashtaka na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 20, mwaka huu. source. Darleo

No comments: