Powered By Blogger

Thursday, June 30, 2011

Msaada Kizimbani: Nitafanyaje kutengana na Mke wangu aliyeko Tanzania mie Marekani?

Ndugu Mwanasheria, naomba Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa makamu, ninayeishi nchini marekani, katika mji wa Newfoundland jimbo la Wayne.  Sasa nimekua na matatizo fulani fulani na mke wangu ambaye anaishi Tanzania. Na nimeona njia muafaka ya mimi kuendelea na maisha yangu ni kuachana naye. Tatizo langu kubwa sijui ni taratibu gani za kufanya(legal procedures), ili niweze kudivorce na huyu mama? Tafadhali naomba Mnipe ushauri wa kisheria juu ya taratibu za kufuatwa  ili niweze kutengana kisheria na mke wangu huyo wa ndoa. Ikizingatiwa kwamba mie naishi marekani nayeye anaishi Tanzania.Asante.

Wednesday, June 29, 2011

Posho kumfukuza Shibuda Chadema"Viongozi wasema"

Mh.Shibuda
Gazeti la mwanachi rimeripoti kwamba kitendo cha Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kupingana na sera ya chama chake kuhusu suala la posho za vikao (sitting allowance), kimeichefua Chadema ambayo imemuita msaliti ikisema, "adhabu yake ni kufukuzwa."Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliliambia gazeti hilo mjini Dodoma jana kuwa, alikerwa na kauli iliyotolewa na Shibuda ya kwenda kinyume na msimamo kambi hiyo kupinga posho za vikao kwa wabunge na wafanyakazi wengine wa umma.

Mbowe alisema kwamba kwa kauli yake ya juzi ya kuunga mkono posho ilidhihirisha kwamba mbunge huyo ni msaliti wa kambi hiyo, hivyo sheria zitafuata mkondo wake.

"Kutokana na tukio la jana (juzi) bungeni, Shibuda kutusaliti katika suala la posho za vikao, taratibu za kisheria zitafuata mkondo wake kwani utovu wa nidhamu haukubaliki katika kambi yetu, hata katika chama chetu,"alisema Mbowe na kuongeza:

"Suala la posho si la mtu binafsi, lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chetu na kama kuna kiongozi hafahamu hili basi hakustahili kugombea ubunge kwa sababu naamini Ilani ya Uchaguzi, Shibuda anayo."

"Posho zilijadiliwa na kupitishwa katika vikao maalumu vya chama, kwa hiyo kama Katiba yetu ya chama inavyotuongoza, Shibuda alitakiwa kulipinga katika vikao hivyo sio kutoka nje ya kikao na kuanza kupingana na maamuzi yake,"alisema Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.


Akinukuu kifungu katika Katiba ya chama chake kinachoeleza maadili ya viongozi, Mbowe alisema, "Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye kanuni."

Kauli ya Zitto
Kwa upande wake, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge kupingana na sera ya chama chake, ni kutokiamini chama hicho.

"Maana yake hakiamini chama, hivyo hafai kuendelea kuwa mwanachama na mbunge wa chama hicho,"alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.

Aliendelea, "Hapa kuna mambo mawili; masuala ya kisera na masuala ya utaratibu. Mbunge anayepingana na taratibu adhabu yake ni kumwita na kumpa onyo, lakini mbunge anayepingana na sera, huyo hakiamini chama na dhabu yake ni kufukuzwa."

Kwa mujibu wa Zitto, suala la kupinga posho kwa Chadema ni sera kwa kuwa limo kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2010."Hili (suala la posho), lipo kisera. Kwenye Ilani yetu ya uchaguzi tulisema, tutapunguza mishahara ya wabunge na posho zao. Sasa kama mbunge anachaguliwa kwa sera hiyo halafu anaipinga haradhani, huyo hakiamini chama na chama hakipaswi kumwamini."

Aliendelea,"Sasa, adhabu ya juu kabisa ya mbunge asiyekiamini chama, ni kufukuzwa. Huu ni usaliti. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mwenyekiti wa chama ameshalitolea tamko suala hilo halafu mbunge anakuja kumpinga hadharani maana yake nini,?" alihoji.

Tundu Lissu je?
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema kitendo cha Shibuda kupingana na sera ya chama chake, "ni uasi usiovumilika".

"Sasa nikiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni nadhani ninahitaji kukaa naye. Nitamwita anieleze kulikoni. Aseme kulikoni ameamua kukiasi chama na upinzani kwa ujumla?"

Aliendelea, "Lakini kwa bahati mbaya sana, adhabu kubwa inayoweza kutolewa na kambi ya upinzani ni kumtenga na kambi. Lakini kwa mtu kama Shibuda ambaye tayari anaijua adhabu hiyo na kuitafuta kwa makusudi, inaonekana haitamtosha."

"Kwa sababu hiyo basi, kambi ya upinzani itaenda mbali zaidi baada ya kumtenga. Tutakiandikia chama barua kukijulisha usaliti huo wa mbunge wake halafu chenyewe kina taratibu zake za kinidhamu."

Kauli ya Shibuda
Juzi alipokuwa akichangia Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2011/2012, Shibuda alitoa mpya pale alipopingana na misimamo wa Chadema kuhusu malipo ya posho kwa wabunge na watumishi wengine wa umma.

Akitumia lugha yake ya mashairi, Shibuda aliliambia Bunge kuwa utata uligubika posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, unatokana na tafsiri potofu ya neno hilo ambalo asili yake ni Ujira wa Mwia.

"Ujira wa Mwia (sasa posho) yalikuwa malipo anayopewa mtu kwa kazi anayoifanya ili kumwongezea hamasa ya kuendelea kuifanya kazi hiyo. Kwa bahati mbaya sasa neno hilo linaitwa posho na ndiyo sababu linaleta mjadala bungeni,"alisema Shibuda huko akishangiliwa na wabunge wa CCM.

Kwa mujibu Shibuda, kama maana ya posho ni Ujira wa Mwia kama ilivyokuwa ikitumika na wakoloni, haina sababu kuifuta kwa kuwa ndiyo hamasa kwa wabunge na watumishi wengine wa umma kuendelea kufanya kazi yao.

Shibuda alilitahadharisha Bunge kuwa mjadala wa posho umetokana na Bunge kuwa na aina mbili ya wabunge; wabunge maslahi jamii na wabunge maslahi binafsi.

"Wabunge maslahi binafsi hawashiriki misiba, hawatembelei hospitali wakasaidia dawa, hawaendi kwenye sherehe na hawana msaada wowote kwa jamii. Sasa aina hiyo ya wabunge hatutegemei kwa nini watake posho,"alisema

Aliendelea,"tabia ya choyo ndiyo inayowasumbua wabunge hao. Lakini pia tujue kwamba kuna wabunge wafanyabiashara na wabunge maslahi, mbunge maskini hawezi kuacha kuchukua posho, sasa ni vema tukatambua tofauti hizo ili tumalize mjadala huo."

Shibuda alipendekeza posho ziendelee kutolewa tena kwa haraka zaidi na nyongeza kubwa badala ya kuendelea kuvutana kuhusu uhalali wake nje na ndani ya Bunge.

"Mheshimiwa Spika, posho haitoshi, inafaa kuongezwa hadi Sh500,000. Mimi nasema na kazi ya kutafsiri ninachosema inategemea busara ya mtu, lakini posho ziongezwe ili zisaidie wabunge maskini, shughuli mbalimbali za kijamii."

Wakati Shibuda akiwa anaeleza hayo, Mbowe, alionekana akitikisa kichwa kwenye kiti chake.

Msimamo wake
Lakini Shibuda alilimbia gazeti hili jana atashangaa kama atatuhumiwa kwa maoni yake binafsi aliyoyatoa bungeni juzi juu ya kutaka wabunge waendelee kulipwa posho za vikao vya Bunge.

"Nitashangaa kama nitaitwa na kiongozi yoyote wa kambi yetu ya upinzani au Chadema kwa tuhuma za kutoa maoni yangu huru niliyoyatoa bungeni jana (juzi), hata nilipokuwa CCM nilipenda kusahihisha palipokuwa na makosa".

"Sitarajii Chadema kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama mimi sitakiwi kutoa maoni huru basi hakuna maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".

 
"Tusitafute hila na visa kwa maslahi binafsi, tutambue kwamba mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".

Alisema kwamba hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho ya vikao vya Bunge.

Shibuda akifafanua zaidi suala hilo la posho japo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chake ilitaka kupunguza posho hizo za vikao pamoja na mshahara wa mbunge, alisema, "Ilani ya Uchaguzi ni mpango kazi wa kuendeleza programu ya chama kilichopo madarakani, kwa hiyo hivi sasa hapa bungeni bila kujali itikadi zetu wabunge tunaunganishwa na programu ya kuendeleza nchi, utawala bora na uongozi wa kuongoza fikra za Watanzania".Chanz gazeti la mwananchi.

Afungwa kumuua rafikiyake: Kisa kaambiwa alipe bili ya bia.


Mshtakiwa Juma Mwita ameshtakiwa na kuhukumiwa na Mahakama kuu kanda ya Mwanza katika shitaka la jinai No. 10 la mwaka 2007 kwa kosa la kusababisha bila kukusudia mauaji ya rafikiye kalyankozie mujuni kinyume na kifungu cha 195 cha Sheria ya makosa ya jinai, ya mwaka 2002. Karani wa mahakama Kuu bi Shida liieleza mahakama hiyo tukio hilo lilitokea huko katika visiwa vya maisome Sengerema.

Akiiieleza mahakama hiyo wakili msomi wa serikali Ndugu; Obadia alisema kwamba mnamo tarehe 22/06/2007 mshtakiwa akiwa na rafiki zake walikua wanakunywa katika baa ya marehemu (kalyankozile mujini).

Baada ya kunywa kwao, rafiki wa mshtakiwa ndugu kalyankozile ambae pia alikua mmiliki wa grocery aliamua  kumuandikia Mtuhumiwa bili ya bia zote alizokunywa marehemu ili mshitakiwa azilipe. Mshtakiwa alikataa kulipa ndio mzozo ulipozuka baina yao. Mshtakiwa aliamua kumsukuma marehemu hivyo kumsababishia maumivu makali.

Aidha wakili huyo wa serikali aliiambia mahakama kwamba siku moja baadaye, marehemu kutokana na maumivu hayo alishindwa kwenda kazini hali hiyo iliendelea  mpaka tarehe 1/7/2007 mauti ilipomfika.


Mshtakiwa alikiri kosa lake hivyo kumlazimu Mh.Jaji G.K. Mwakipesile kumtia hatiani na kumfunga kifungo cha miaka 5 nje kwa mujibu wa kifungu cha 326(1) cha Sheria ya mwenendo wa Mashtaka kama ilivyofanyiwa marekemisho Mwaka 2002; ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Tuesday, June 28, 2011

Mh.Shibuda awageuka Wabunge wa Chadema: Adai Posho hazitoshi ziongezwe

Mh. John Shibuda
MBUNGE wa Maswa Magharibi John Shibuda (Chadema) amewaugeuka wabunge wa chama hicho kwa kuitaka Serikali kuongeza posho za wabunge badala ya kuziondoa.Amesema kuwa kwa majukumu ambayo yanafanywa na wabunge hasa wa aina yake ambaye ni mbunge kwa ajili ya maslahi ya jamii na si binafsi ni vema posho zikaendelea kutolewa na kutaka ziitwe malipo ya mwia.

Shibuda alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambapo alisema ni bora akawa mkweli na wakatofautiana kifikra lakini awakawa amesema kile ambacho anakiamini.

Alisema alisema kuwa kwa mbunge ambaye anashiki katika misiba, anachangia sherehe, anachangia mambo ya jamii na kushirikiana kikamilifu na wananchi atakuwa anahitaji fedha hizo za posho anazoziita ujira wa mwia.“Naomba Serikali ihakikishe inalipa mwai hizi za wabunge kwa haraka, tena ikwezekana iwe hata laki tano, najua wapo ambao wanaweza kunitafsiri vibaya lakini nachoweza kusema kwa wale ambao wananipenda wataninatafsiri vizurina wasionipenda watanitafsiri vibaya.

“Tunahitaji kupewa fedha hizi kwasababu tunataka kuwatumikia wananchi wetu kikamilifu. Hawa wabunge ambao wanafanya kazi kwa ajili ya maslahi binafsi watakuwa na mitazamo yao,” alisema Shibuda na kuongeza kuwa lazima ujiwa wa Mwia uongezwe kwa wabunge.

Kutokana na kauli hiyo ya Shibuda ni wazi amewageuka wabunge wa CHADEMA ambao walikuwa wametoa msimamo kuwa wamekubaliana kuwa wapo tayari kukata posho hizo lakini kitendo cha Shibuda kuja na msimamo tofauti wakata posho hizo ziendelee kulipwa.

Shibuda katika kuzungumzia hilo alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha wabunge wanaendelea kupewa haki zao kwa maslahi ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa fedha ambazo wanazipata kutokana na majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Pia alisema kuwa hataopenda kuona Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakiufa lakini anataka kuona wanajirekebisha kwa kuondoa ufisadi uliopo ndani ya chama hicho na kwa watumishi wa Serikali na kuongeza kujivua gamba haitoshi.Alisema kuwa umefika wakati kwa Serikali kuhakikisha inaondokana na ufisadi lakini akatumia nafasi hiyo kusema amejifunza mambo mengi kwenye siasa hasa kutokana na kuwa ndani ya chama tawala na sasa amejiunga na upinzani lakini kibaya zaidi ukiwa upinzani unaonekana si mwenzao.

Alisema kwa mazingira ambayo yanafanywa na watumishi wa umma kwa wapinzani yanasikitisha lakini akatumia nafasi hiyo ufike wakati wa kuondokana na dhana ya kuwachukia wapinzani. Chanzo The Habari.

Mchungaji Mbaroni kwa kumuua Mkewe.

MCHUNGAJI wa Kanisa la World Missionery Fellowship of Tanzania (WMF) katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Bw. Gaspar Joseph (52) anashikilizwa na polisi kwa kumuua mke wake baada ya kumpiga kwa fimbo katika ugomvi baina yao.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Bw. Henry Salewi alimtaja mwanamke huyo aliyeuawa kuwa ni Godeliver Gaspar (48) mkazi wa Migera katika Manispaa ya Bukoba, na kuwa alifariki dunia Juni 26, mwaka huu katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera.

Bw. Salewi alisema kuwa mchungaji huyo alikuwa akimpiga mke wake kwa muda mrefu, ambapo Juni 22 baada ya kumpa kipigo kikali, mchungaji huyo alimpeleka hospitali bila kutoa taarifa zozote, ambapo Juni 26 alifariki dunia wakati akipatiwa dawa.Alisema jeshi la polisi linamshikilia mchungaji huyo kwa ajili ya mahojiano zaidi na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya taratibu muhimu kukamilika.

Kamanda Salewi alisema kabla ya kifo cha mwanamke huyo, polisi walipokea taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu kuwa Bi. Gaspar hali yake ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera kutokana na kipigo cha mme wake.
 
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa na kuwa chanzo cha ugomvi huo uliosababisha kifo hicho bado hakijafahamika, ingawa taarifa kutoka eneo la tukio zinadai kuwa ugomvi huo ulitokana na binti yao wa kike kupata mimba.

Taarifa hizo zinasema kuwa mchunguji huyo alikuwa akimshtumu mke wake kusababisha mtoto wao wa kidato cha kwanza kupata mimba kwa madai ya kutomlea katika maadili, pia akimtuhumu kwa kuficha siri za binti huyo juu ya ujauzito aliokuwa nao.

Taarifa hizo zinadai wiki mbili kabla ya mwanamke huyo kuzidiwa na kupelekwa hospitali kila mara alikuwa akimpiga, hali inayodaiwa kusababisha maumivu na hatimaye kifo chake. Chanz gazeti la majira.

Vigogo 7 Wizara ya Ardhi kortini.

Baadhi ya watuhumiwa wakiwasili Mahakamani Kinondoni
VIGOGO saba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wa Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, wakidaiwa kutoa viwanja kinyume cha utaratibu.

Wakisoma jana mashitaka mbele ya Hakimu Yohana Yongolo wa Mahakama hiyo, waendesha mashitaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Leonard Swai na Pendo Temu, walidai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Juni na Oktoba 2008.

Waliopandishwa kizimbani ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilongawima, Josephat Woiso, Diwani wa Kunduchi, Patrick Makoyola, Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kilongawima Mbezi, Wanura Maranda na Mpima Ardhi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Hamidu Mgaya.

Wengine ni Ofisa Mipango Miji wa Wizara hiyo, Anna Macha, Ofisa Mipango Miji Msaidizi wa Wizara, Mapambano Baseka na Ofisa Ardhi Msaidizi wa Manispaa ya Kinondoni, Saidi Maligwah. Mshitakiwa mwingine, Patrick Makoyola hakuwa mahakamani hapo.

Waendesha mashitaka hao walidai kuwa washitakiwa walitoa taarifa za uongo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, kuhusu viwanja na kusababisha aviidhinishe na kutoa hati halali.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kukiuka Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kwa kutumia madaraka yao vibaya na kusababisha watu kupata viwanja kinyume na utaratibu. Wote walikana mashitaka na wapo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyowataka kuwa na wadhamini wawili wa kusaini dhamana ya Sh milioni moja kwa pamoja. Pia walitakiwa kutosafiri nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya Mahakama.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa maelezo ya awali Julai 26 na Hakimu alitaka mtuhumiwa mwingine aliyesalia kufikishwa mahakamani pamoja na wenzake siku hiyo.

Monday, June 27, 2011

LHRC yaomba Hati ya kuwakamata Viongozi wa Dowans:

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimewasilisha ombi chini ya hati ya dharura Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuomba itoe hati kukamatwa kwa Wakurugenzi wa Kampuni za Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited kwa kudharau amri ya Mahakama.

Maombi hayo yaliwasilishwa baada ya taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari Mei 21 mwaka huu, kuwa mitambo ya Dowans imeuzwa kwa Kampuni ya Symbion Power ya Marekani kwa thamani ya Dola milioni 120.Maombi hayo yaliwasilishwa na wakili wao LHRC Dkt. Sengondo Mvungi, kupitia hati ya dharura.

Jaji anayesikiliza kesi ya kuomba kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans, Bi. Emilian Mushi, Machi 3, mwaka huu alitoa amri kutaka pande zote mbili katika kesi hiyo kutogusa lolote linalohusiana na kampuni hizo.

Katika amri hiyo ya Mahakama iwapo upande wowowte ungehitaji kufanya lolote ni lazima kwanza waombe kibali cha mahakama.Kituo hicho ni miongoni mwa wanaopinga Mahakama Kuu ya Tanzania kusajiliwa kwa Tuzo ya Dowans ya sh. bilioni 94 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).

Kituo hicho kinaomba pia mahakama itoe amri ya kuwataka wadaiwa hao waweke Dola za Marekani milioni 120 kama dhamana na kulipa gharama za kesi hiyo.

Mbali na LHRC Mwandishi wa Habari Mwandamizi Bw.Timoth Kahoho, naye amewasilisha maombi kama hayo.Bw.Kahoho naye ni miongoni mwa wanaopinga tuzo ya Dowans isisajiliwe pamoja na Shirika la Umeme (Tanesco).

Januari 25 mwaka huu Dowans iliwasilisha ombi la kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania isajili tuzo waliyopewa na ICC na siku chache baadaye Tanesco, LHCR na Bw.Kahoho waliwasilisha hati ya nia ya kupinga ombi hilo la kutaka tuzo hiyo isajiliwe.

ICC ilitoa hukumu ya kesi ya Dowans dhidi ya Tanesco, Novemba 15, mwaka jana, na kutaika  iilipe fidia ya fedha ambazo kwa tahamani ya fedha za kitanzania ni takriban bilioni 94.Chanzo gazeti la Majira.

Hati ya kumkamata Gadaffi yatolewa.

Kanali Mohamed Gaddafi

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.Mahakama imemtuhumu kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuamuru mashambulio kwa raia baada ya machafuko dhidi yake kuanza kati kati ya mwezi Februari.

Mahakama hiyo iliyopo the Hague pia imetoa hati ya kukamatwa kwa washirika wake wakuu Kanali Gaddafi- mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa kijasusi Abdullah al-Sanussi. Maelfu ya watu wanaaminiwa kufariki dunia kwenye ghasia hizo.

Hati hizo ziliombwa na mkuu wa mahakama hiyo ya ICC Luis Moreno-Ocampo mwezi Mei, aliyesema watu hao watatu walihusika na "mashambulio yaliyopangwa na yaliyosambaa" kwa raia.Bw Moreno-Ocampo alisema mahakama hiyo ina ushahidi kuwa Kanali Gaddafi "aliamuru binafsi mashambulio kwa raia wa Libya wasio na silaha na alihusika kwa kukamatwa na kunyanyaswa kwa wapinzani wake wa kisiasa.

Serikali ya Libya hivi karibuni ilisema haitambui mahakama hiyo na tishio la hati hiyo haiwashughulishi.

Katiba Mpya kuzinduliwa April,2014

Mh.Mizengo Pinda
KATIBA MPYA ambayo mchakato wake umeanza inatarajiwa iwe imekamilika na kuzinduliwa rasmi Aprili 26, 2014 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mjini hapa.

Akifungua Semina Elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, alisema hayo ndiyo matarajio ya Serikali. "Ni matarajio ya Serikali kuwa Katiba Mpya itakuwa imekamilika na kuzinduliwa ifikapo tarehe 26 Aprili, 2014 katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kwamba kama mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa, Muswada wa Sheria kuhusu Mapitio ya Marekebisho ya Katiba utawasilisha bungeni mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge unaoendelea hivi sasa au mwanzoni mwa Mkutano wa Tano Oktoba mwaka huu.

Aliwataka Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni itakayoundwa ili kuwezesha mikutano ya hadhara ya kukusanya maoni  kufanyika kama ilivyokusudiwa kwa kuhamasisha wananchi kuhudhuria na kutoa maoni yao.

“Katika suala hili kubwa na la kitaifa, ni vyema viongozi wasiingize siasa na wajiepushe kuwashawishi wananchi katika kutoa maoni yao, bali wawaache watoe maoni kwa uhuru au pasipo shinikizo lolote,” alisema. Mchakato huo wa kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya, umekwishaanza na katika hatua ya awali, Serikali imeandaa rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011. 
Wakati huohuo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amesema haitoshi kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuweka ukomo wa kukamilika kwa katiba mpya ifikapo mwaka 2014 ,bila kuweka ratiba ya mchakato wa kupata katiba hiyo.Amesema  wananchi wanapaswa kupokea kwa tahadhari taarifa ya Pinda kwa kuwa alipaswa kuitoa bungeni na si  katika mkutano nje ya Bunge.

Mnyika alisema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kufuatia kauli ya Waziri Mkuu kwamba katiba mpya itazinduliwa Aprili 26 mwaka  2014.

Rufani ya Mahita yatupiliwa mbali.

MKUU wa zamani wa Jeshi la Polisi Nchini, Omar Mahita, ameumbuka kwa mara nyingine baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kuhusu sakata la mtoto anayemkataa.

Rufaa hiyo ya Mahita ilitupiliwa mbali jana na Jaji Dk Fauz Twaib, baada ya kuridhika na hukumu ya mahakama ya chini kuwa ilikuwa sahihi na kumwamuru Mahita kulipa gharama za kesi hiyo.Hata hivyo wakati hukumu hiyo ikitolewa, Mahita hakuwapo mahakamani na wakili wake Semgalawe, alifika wakati tayari jajiakiwa ameshamaliza kusoma hukumu.
 Septemba mwaka 2009 Mahakama ya Kinondoni  ilimwamuru Mahita kutoa kiasi cha Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya kumhudumia mtoto  na kulipa malimbikizo ya gharama za matunzo kuanzia mwaka 2003 hadi siku ya hukumu.

Hukumu hiyo ilitokana na kesi ya msingi iliyofunguliwa katika mahakama hiyo na aliyekuwa mfanyakazi wa Mahita, Rehema Shabani, kupitia kwa Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamau (LHRC).Katika kesi hiyo, Rehema alikuwa anadai matunzo ya mtoto Juma Omar Mahita, baada ya kumtelekeza na baadaye mahakama ilifikia uamuzi wa kumtaka Mahita kulipa gharama hizo.Mahakama pia iliamuru Mahita akachukuliwe vipimo vya vinasaba (DNA) lakini Mahita akakataa.

Hata hivyo Mkuu huyo wa zamani wa Polisi, kupitia kwa wakili wake Charles Semgalawe aliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, akipinga hukumu na adhabu hiyo.Katika rufaa hiyo, Mahita aliwasilisha sababu nne za kupinga hukumu na adhabu hiyo.Alidai kuwa pamoja na mambo mengine,mahakama ya chini ilikosea kisheria kuamua kwa kuwa shauri la matunzo ya mtoto halikufunguliwa nje ya wakati, kinyume cha Sheria ya Kuasili Watoto.

Pia alidai kuwa mahakama ya chini ilikosea kusema kuwa mrufani ni baba halali wa mtoto kwa kuegemea katika ushahidi wa mjibu rufani kwa madai kuwa mrufani alikataa kuchukua vipimo vya DNA wakati si kweli.

Mahita pia alihoji uhalali wa amri ya mahakama ya chini kumwamuru kumlipa mjibu rufani kiasi Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto wakati sheria inataja kiasi cha Sh100.

Hali kadhalika, alilalamikia amri ya mahakama ya chini ya kumtaka kulipa fidia kuanzia mwaka 2003  hadi siku ya hukumu.Hata hivyo katika hukumu yake jana Jaji DK Twaib alitupilia mbali sabababu hizo  baada ya kuziona kuwa hazina msingi na kuungana na baadhi ya hoja za wakili wa mlalamikaji, Fredrick Mkatambo kutoka LHRC.


Wakili huyo alizipinga vikali sababu hizo wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo.Jaji Dk Twaib alichambua sababu moja baada ya nyingine na kuzitolea maelezo ya kisheria ya sababu za kuzitupila mbali.

Thursday, June 23, 2011

Sheria ya Gharama za Uchaguzi kufanyiwa marekebisho.

Mh.William Lukuvi
Serikali imekubali kufanyia marekebisho Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa kuzingatia maoni mbalimbali ya wadau wakiwemo Wabunge.Hayo yalisemwa Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkanyageni, Habib Juma Mnyaa (CUF).

Awali, Mnyaa, alisema sheria hiyo haikushirikisha upande wa pili wa muungano (Zanzibar), kwasababu hakuna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).Alihoji serikali ina mpango gani wa kufanyia marekebisho sheria hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuondoa mapungufu yaliyoonekana.

Akijibu swali hilo , Lukuvi, alisema serikali itaendelea kuifanyia tathimini sheria hiyo kwa kukusanya maoni ya wadau mbalimbali.Katika swali lake la msingi, Mnyaa, alitaka kufahamu kama sheria hiyo ilisaidia kuondoa rushwa wakati wa uchaguzi au iliwakinga baadhi ya wagombea na kuwatisha wengine.

Pia alitaka kujua serikali imepata uzoefu gani katika kutekeleza sheria hiyo.Lukuvi, alisema sheria hiyo ilitungwa na Bunge si kwa lengo la kumkinga mtu yeyote, bali kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakuwa huru na wa haki.

Alisema sheria hiyo kwa kiasi kikubwa ilisaidia kupunguza vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mh.Jaji aangua kilio akijitetea.

JAJI Atuganile Flora Ngwale wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kitengo cha Ardhi, janaalishindwa kujitetea kuhusu kushindwa kwake kujaza fomu zinazohusu mali na madeni yake, kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Jaji huyo alishindwa kufanya hivyo  mbele ya Baraza la Maadili ambako aliangua kilio na hivyo kusababisha wanasheria kushindwa kumhoji.Hali hiyo ililazimisha baraza kusitisha usikilizaji wa shauri hilo.Wakati akiangua kilio, jaji huyo alilieleza baraza kwamba alishindwa kujaza fomu hizo na kuomba msamaha.Wakati akiangua kilio, jaji huo alisema "sina mali yoyote, kazi ndio maisha yangu, watoto wangu wanategemea kazi hii siwezi kudharau mtu, naomba mnisamehe, nimejifunza Mungu wangu,"alisema jaji huyo.

Jaji Ngwale alisimama katika baraza hilo ili kuanza kujitetea, lakini ghafla aliangua kilio kwa sauti ya juu huku akiomba baraza hilo limuonee huruma kwa kutojaza fomu."Ni kweli sijajaza fomu na kama kuna mtu aliniona nimejaza fomu hizi ajitokeze ndani ya baraza hili la maadili," alisema.

"Kazi hii ndio maisha yangu, kazi hii ndio faraja ya watoto wangu hivyo naitegemea sana  sina mali zozote za kunitesa na kuniita katika Baraza la Maadili,"alisema Ngwale huku akimwaga machozi.


Baada ya Barazakuona Jaji Ngwale ameshindwa kujitetea kwa njia ya mdomo, lilimtaka atoe  utetezi wake kwa njia ya maandishi na kulazimika kusitisha kuendelea na shauri hilo.Mbali na baraza hilo kusitisha kuendelea kusikiliza shauri hilo, pia wanasheria wa sekretarieti ya maadili na hawakupata nafasi ya kumhoji Jaji Ngwale kutoka na hali hiyo.Baada ya baraza hilo kusitisha kuendelea kusikiliza shauri hilo walimuomba jaji huyo aondoke mbele yabaraza hilo, lakini jaji huyo alikaidi agizo la wanasheria hao na badala yake aliendelea kulia mpaka baraza hilo lilipomuomba mmoja wa wanasheria ambembeleze na baada ya kubembelezwa alikubali kwenda kutoa maelezo yake kwa njia ya maandishi na baadaye aliruhusiwa kuondoka.


Baraza hilo litaendelea leo kwa ajili ya kuhoji watu wanne ambao hawakujaza fomu hizo za maadili ya umma mwaka jana, miongoni mwa watu hao watakaohojiwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Kanazi Mathias Bisoma Mgatta, Mkurugenzi wa  Shirika la Hifadhi ya Jamii la Taifa (NSSF), Crecencius  Magori.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kikosi cha Usalama Barabarani,  Tafiki Mwanza, Francis Bayona Katunzi na Diwani wa Mpanda mjini Ally Juma Nsokolo.Chanzo gazeti la mwananchi.

Wananchi wapambana na polisi kuwaokoa wenzao.

MABOMU ya machozi, risasi zilirindima jana kwa saa mbili huku wakazi wa Mji wa Bunda wakifunga maduka na kukimbia ovyo kwa hofu wakati polisi wa Kituo cha Bunda mkoani Mara walipokuwa wakipambana na wananchi wenye hasira kali waliotaka kuvamia kituo hicho.

Askari hao wakiwa na silaha hizo walionekana wametanda kuzunguka kituo hicho wakiwa na magari na kusababisha barabara kubwa ya Mwanza-Sirari kufungwa kwa muda wakati wa mapambano hayo.Milio ya risasi ilisikika mfululizo kuanzia saa 2:30 hadi saa 4:30 asubuhi jana ililenga kutawanya mamia ya wakazi wa Kijiji cha Tairo waliojichanganya na wenyeji wa mji huo huku na silaha za jadi na mawe kwa ajili ya kutaka kuvamia kituo hicho na  kuwaokoa watu wawili ambao walidai wanashkiliwa na jeshi hilo bila hatia.

Kabla ya kuvamia kituo hicho, wananchi hao walichoma moto na kuteketea nyumba 10 za familia nne tofauti kijijini hapo ambao waliwatuhumu kuhusika katika matukio matatu ya kuvamia zahanati na Ofisi ya Shule ya Tairo na kupora viti vitatu, magunia mawili ya pamba ya mwalimu mmoja wa shule hiyo aliyetajwa kwa jina la moja la Bw. Marekera na duka moja la Bw. Kikore Magwega.

Watu hao Bw. Jekonia Abiero ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Tairo katika miaka ya hivi karibuni na Bw. Kikore Magwega ambaye ni mfanyabiashara aliyeporwa bidhaa zake katika tukio hilo la ujambazi katika kijiji hicho wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano huku wananchi wakishinikiza waachiwe huru.

Hata hivyo, bila madhara makubwa polisi hao walifanikiwakuwatawanya wananchi hao ambapo walisema kwa sasa jeshi hilo limepewa mbinu mpya ya kupambana na wananchi wanaoshikilia sheria mikononi bila madhara na kuwataka wazingatie haki ya sheria.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi wilayani Bunda watuhumiwa wawili wa ujambazi wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo wamekamatwa  baada ya kujeruhiwa vibaya na wananchi wenye hasira na wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda chini ya ulinzi wa polisi na kwamba juhudi za kuwakamata wengine zaidi bado zinafanywa na jeshi hilo.

Akithibitisha tukio hilo, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Tairo, Bw. Raimond Misana aliwataja watuhumiwa wa ujambazi katika matukio hayo kuwa ni Bw. Amos Machele, Bw. Marwa Ghati ambao wameshikiliwa na polisi.

Alitaja watuhumiwa waliokimbia kwa kuwatoroka wananchi kuwani Bw. Nyango Mgore na Bw. Bhoke Nyitambe na kwamba wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuhusika katika matukio hayo ya ujambazi.

Bw. Misana alitaja baadhi ya nyumba za watuhumiwa zilizochomwa moto na wananchi wenye hasira ni pamoja na nyumba 4 za Bw. Nyango Mgore, nyumba 3 za Bw. Bhoke Nyitambe, nyumba 2 za Bw. Amos Machela zilizochomwa pamoja na kibanda 1 cha biashara cha Bw. Amos Machela.

matukio ya wananchi wanaojidai kuwa na hasira kali imeendelea mkoani Mara ambapo hivi karibuni baadhi ya wananchi wa Nyamongo wilayani Tarime walipambana na polisi katika migodi wa North Mara na kusababisha vifo vya watu watano siku chache kabla wananchi wengine kuvamia Kituo cha Polisi mjini Mugumu, Serengeti kwa lengo la kutaka polisi kuachia baadhi ya watuhumiwa wa mauaji.Chanzo gazeti la majira

Wednesday, June 22, 2011

Mh.Hakimu afa Chumbani kimyakimya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke
HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo ya Pangani iliyopo Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Jaffar Mselem (62), amekutwa amekufa katika nyumba anayoishi na mwili wake kukaa ndani kwa zaidi ya siku mbili bila kujulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, amesema, kifo cha Hakimu huyo, kinasadikiwa kutokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu nyumbani kwake eneo la Kwa Azizi Ali wilayani Temeke.

Misime amesema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa kifo cha hakimu huyo mstaafu anayefanya kazi kwa mkataba, kilisababishwa na umeme alipokuwa akiwasha kifaa cha kuchemshia maji ya kuoga.

“Kwa mujibu wa majirani zake na mtoto wake, Jumapili Mselem alishinda kwa mtoto wake anayeishi eneo hilo hilo hadi aliporejea nyumbani kwake jioni,” amesema Misime.

Amesema, baada ya kurejea katika nyumba hiyo ambayo anaishi peke yake upande mmoja huku upande mwingine ukikaliwa na wapangaji wake, Mselem hakuonekana tena hadi mwili wake ulipokutwa juzi sakafu chumbani mwake.

Kamanda Misime amesema, kugundulika kwa kifo, kulitokana na mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama anakofanyia kazi Mselem, kufika katika nyumba hiyo juzi kwa lengo la kumwangalia baada ya kutoonekana kazini Jumatatu na kukuta mlango wa nyumba yake umefungwa.

Alisema baadaye walitoa taarifa Polisi ambao walifika na kuvunja mlango, wakamkuta Hakimu huyo tayari amekufa na mwili umeanza kuharibika, suala ambalo majirani walidai kuhisi harufu kwa muda bila kujua ilikokuwa ikitokea.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa uchunguzi huku upelelezi wa tukio hilo ukiendendelea.Chanzo gazeti la habari leo.

Mh.Jaji werema azusha Malumbano Bungeni.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema jana alijikuta kwenye mgogoro na wabunge baada ya kueleza bungeni kuwa baadhi yao wanazungumza bila kufikiri ili waonekane kwenye luninga.Tukio hilo lilitokea jana wakati Bunge limekaa kama kamati kupitisha Muswada wa Fedha wa mwaka 2011 ulioletwa bungeni kwa mara ya pili na Naibu wa Waziri wa Fedha na Uchumi, Pereira Silima .

Chanzo cha mgogoro huo ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuleta mapendekezo katika kifungo cha tano cha Muswada huo kutaka Kamishna na watendaji wa Serikali kuondolewa madaraka ya kusamehe kodi.Lissu alilieleza Bunge kuwa tabia hiyo ndiyo mwanzo wa rushwa na ufisadi nchini kwani baadhi ya watendaji hao wamekuwa wakitumia vibaya mamlaka hizo. Lissu alitaka anayekosea katika suala la kodi akutane na adhabu.

Baada ya mapendekezo hayo, Mwenyekiti Anne Makinda alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutolea ufafanuzi suala hilo na Jaji Werema alisimama na kusema:"Sina nia ya kutukana mtu, lakini niseme tu hilo liko wazi, kwamba mtu anayeweza kuchelewa kulipa kodi, lakini ana sababu na sasa tunasema ikitokea ana sababu za maana, asamehewe, hatuwezi kusema kwa sababu amekosea basi aadhibiwe, tunaishi na jamii ambayo  watu wana matatizo,"

Aliendelea,"Nisema tu kwamba watu tusizungumze tu ili tuonekane kwenye luninga, nadhani ni vema tukafikiri kwa mapana na vizuri zaidi."

Kauli hiyo ilimwibua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye alisimama na kuomba mwongozo wa spika kisha akasema,"Mheshimiwa Spika humo ndani sisi ni viongozi na tuko kwenye legislation process. Sasa kuna kauli za kuudhi zinazotolewa na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambazo hazivumiliki"

Aliendelea,"Mimi namheshimu sana Jaji Werema, lakini siamini kwamba kauli hizo ni zake, labda awe ameumwa siku hizi mbili tatu. Kusema wabunge hatufikiri sawa sawa anatutukana wabunge, namwomba awaheshimu wabunge na afutee kauli yake kwamba wabunge wanazungumza ili waoanekane kwenye TV."

Akitolea mwongozo suala hilo, Makinda alisema "Nashukuru kwamba sasa kadiri siku zinazoendelea wabunge tunajua kuwa kuna maneno ya kauudhi maana wengine maneno hayo mnayatoa hata kwenye vyombo vya habari. Ni kweli kauli hiyo ya (Werema) inaudhi na tunamwomba aifute."

Baada ya agizo hilo, Jaji Werema alisimama na kusema kuwa "Mimi sijaumwa, ni mzima kabisa."

Baadaye Zitto alisimama na kusema "Nakubali Jaji Werema hajaumwa na nafuta kauli yangu."

"Sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali simama na ufute kauli yako," aliagiza Makinda

"Naitoa kauli yangu," alisema Jaji Werema.

Hoja ya posho yatikisa Bunge

Hali iliendelea kuchafuka bungeni baada ya hoja ya posho kurejeshwa tena kinyemela na kuzua mjadala mkali kati ya wabunge wa CCM ambao waliendelea kutetea posho hizo na wabunge wa upinzani ambao wanaipinga.

Kauli ya Lissu kwamba mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono anaokoteza maneno kwa kutetea posho za wabunge akisema zipo hata kwa madiwani, ilizua balaa nyingine baada ya wabunge wengi wa CCM kusikika wakipiga kelele,"afute kauli hiyo afute!

Hata hivyo, Mwenyekiti Makinda alipuuza kauli hizo na kuendelea  kuongoza mkutano huo huku wabunge wakiendelea kupigana vijembe chinichini.

Lissu alipinga pendekezo la Serikali kufuta kodi ya posho akisema sio sahihi kwani baadhi ya watumishi wa umma wakiwamo wabunge wanapewa posho kubwa inayostahli hata kukatwa posho.

Baadaye Waziri katika Ofisi ya Rais, (Sera na Utaratibu), William Lukuvi alisimama na kueleza kuwa hoja ya upinzani ni ya msingi, lakini inahitaji muda kufanya marekebisho hayo.

"Hoja hii ni sahihi, wabunge ni kweli tuna mishahara mikubwa kuliko watumishi wetu mimi napata responsibility allowance ya 200,000 na kiongozi wa upinzani anapata Sh2  milioni, ni vizuri, lakini tunahitaji kutumia kanuni kujadili hilo,"alisema

Lissu alieleza kuwa hoja yake sio kufuta posho bali kuondoa kodi ya posho wakati sheria iliyopo inataka wanaopata posho kuanzia Sh200,000 watozwe kodi.Wakati hao yakiendelea katika Ukumbi wa Bunge ulikuwa ukijaa kelele kwa wabunge kushangilia.

DIWANI CCM JELA KWA KUTOA RUSHWA

DIWANI wa Viti Maalumu wa Tarafa ya mlingoti Wilayani Tunduru kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Atingala Mohamed amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya sh milioni 6 baada ya kupatikana na hatia ya kutoa rushwa.

Katika shauri hilo namba 13/2011, Diwani huyo alituhumiwa kutoa khanga na vitenge kwa wajumbe 15 wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Tunduru ambapo alifanikiwa kuibuka mshindi wa nafasi hiyo. Mashtaka hayo yalifafanua kuwa kutokana na hali hiyo, diwani huyo alikiuka kifungu Namba 13 (1) (A) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Namtumbo, Bw. Sprian Semwija alisema kuwa mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na inaamini kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia hiyo.Katika mashtaka hayo, Bi. Atingala alitiwa hatiani katika Makosa 9 kati ya 15 aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya. Katika kosa la kwanza, mahakama hiyo ilimhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili Jela au kulipa faini ya sh. milioni mbili na makosa manane yaliyobakia mahakama hiyo ikamhukumu adhabu ya mwaka mmoja mmoja au kulipa faini ya sh. 500,000/ kwa kila kosa.

Wakizungumzia adhabu hiyo Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Bi. Monica Mtili mbali na kuonesha kushtushwa na taarfa za tukio hilo awliwataka viongozi Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoani Ruvuma kushughulikia na kuhakikisha kuwa watuhumiwa wote wa makosa ya Uchaguzi Mkuu wanafikishwa Mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake vingivyo wananchi watakosa imani na chombo hicho.

Nao Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bw. Mustafa Bora na kaimu katibu wa CCM Wilaya ya Tunduru Bw. Hasan Kindamba walisema kuwa adhabu hiyo ni salamu kwa wanasiasa ambao hutumia njia za panya kupata madaraka na kuongeza kuwa ingawa makosa ya Rushwa yako wazi sana lakini kesi ya Diwani Atingala ilikuwa na mambo mengi yaliyojificha ingawa hawakufafanua.

Wakizungumzia nafasi ya udiwani viongozi hao walisema kuwa wanasubiri maelekezo kutoka Makao Makuu ya CCM taifa ili waweze kuteua Diwani mwingine kujaza nafasi hiyo.

Kamanda wa Taasisis ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Daud Masiko alisema kuwa huo ni mwanzo tu na kwamba watuhumiwa wote wa makosa ya uchaguzi watafikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.Chanzo gazeti la majira.

WACHINA WAMPIGA MKUU WA KITUO CHA POLISI

Imeripotiwa katika gazeti la Mwananchi  kwamba juzi kwenye kituo cha Polisi Babati Mjini mkoani Manyara baada ya wafanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Chico, raia wa China walimpiga mkuu wa kituo hicho, ASP Shaaban Minginye na mkuu wa polisi jamii mkoani humo, ASP Morris Okinda.

Tukio hilo lililodumu kwa saa mbili kati ya saa 12:30 jioni hadi saa 2:30 usiku liliwalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto zilizorushwa hewani ambazo hata hivyo zilijibiwa na Wachina hao wakitumiia bastola nao, hali iliyoweka rehani amani  mjini  Babati.

Wachina hao wanadaiwa kufanya vurugu hizo na kuwashambulia ASP Mingiye na Okinda kwa madai kuwa polisi walimwachia dereva wa basi la abiria aliyelikwaruza gari lao na kusababisha ajali. Kitendo hicho cha kuwapiga makonde viongozi hao wa polisi mkoani humo kiliamsha hasira za wananchi ambao walianza kumshambulia mmoja wa raia hao wa China.

Gazeti hilo ilishuhudia raia huyo wa China, Chang Charles akipigwa na wananchi hao waliochukizwa na kitendo chao cha kuwapiga polisi ambapo alijaribu kutumia mtindo wa kujihami 'kung fu' huku akitoa sauti za, 'huu, haa', lakini alipigwa ngumi iliyomjeruhi usoni

Katika tukio hilo, ASP Minginye alipigwa vibao na ngumi na raia mmoja wa China ambapo raia watatu wa China walijeruhiwa vibaya na wananchi na kulazwa kwenye Hospitali ya Mrara mjini Babati na hali zao zilielezwa kuendelea vizuri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Liberatus Sabas alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kwamba raia 10 wa China wanashikiliwa kwa kuhusika na vurugu hizo.Alisema chanzo cha vurugu hizo ni raia mmoja wa China, (Chang Charles) kumpiga mkuu wa kituo cha polisi Babati, baada ya kuliachia basi la abiria lililogonga lori linalomilikiwa na kampuni hiyo (Chico), kitendo kilichofanya  wananchi kumpiga Mchina huyo.

"Hali hiyo ilijitokeza baada ya basi la abiria aina ya Scania, mali ya Kampuni ya NBS lililokuwa likitokea Kahama kwenda Arusha kukwaruzana na gari la kampuni hiyo ya Kichina lililokuwa linatumika katika ujenzi  wa barabara ya Babati-Singida,"alisema.

Alisema baada dereva wa basi hilo kulikwaruza gari la kampuni ya Chico aina ya Ford, tukio hilo liliripotiwa kituo cha polisi Babati na dereva wa basi kutakiwa kuwapeleka abiria Arusha ili kesho yake arudi kituoni hapo.


“Baada ya dereva wa basi kuruhusiwa na kuondoka raia mmoja wa China alianza kurusha mawe kwenye basi hilo na kuvunja taa na kioo cha mbele na kumpiga mkuu wa kituo, ndipo abiria waliposhuka na kuanza kumshambulia Mchina huyo,” alisema Kamanda Sabas.


Alisema baada ya vurugu hizo lilizuka kundi lingine la raia wa China lilijitokeza na  kuanza mapambano na wananchi na ndipo katika vurugu hizo askari polisi wakapiga risasi hewani na mabomu ya machozi ili kuwatawanya na kujaribu kusitisha vurugu hizo.


“Hadi hivi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia raia 10 wa China wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na tunatarajia kuwafikisha mahakamani leo (jana), ili wakajibu mashtaka ya uaribifu wa mali na kufanya vurugu,” alisema Kamanda Sabas.

Kamanda Sabas aliwataja Wachina hao wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Chang Charles, Luan Hiten(23), Wang Sheng(23), Sing Yun(24), Sing Jin (23), Lin Jun (37), Whang Puong(23) Lu Gang (23) na Sio Jing (23).Alisema katika vurugu hizo, askari polisi mmoja ambaye hakumtaja jina alijeruhiwa jichoni na Wachina hao na raia watatu wa China walijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mrara wakipatiwa matibabu.

Aliwataja raia hao wa China waliojeruhiwa kuwa ni Young Gris, Luan Hiten  na Chang Charles ambao alisema hali zao zinaendelea vizuri, baada ya kupatiwa matibabu.

Tuesday, June 21, 2011

Mbunge na Hakimu wabanwa kwa kutokuwasilisha tamko la mali.

Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma jana liliwafikisha kwenye baraza hilo, Mbunge wa Korogwe Mjini (CCM), Yusuph Nassir, na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Usevya iliyopo Wilayani Mpanda, Vultan Kundy, kwa kushindwa kurejesha fomu za mali zao.

Akijitetea mbele ya baraza hilo chini ya Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Nassir alikana mashitaka hayo na kujitetea kuwa alitimiza wajibu wake wa kuchukua fomu na kuirejesha katika ofisi za maadili za mkoani Dodoma.Alisema hata hivyo alishangaa kuona anaitwa katika baraza hilo wakati alikuwa ni miongoni mwa wale waliojaza na kurejesha fomu hizo na kukiri kwamba Desemba 22, mwaka jana ndipo aliporejesha.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, nakili kwamba mimi si kiongozi mzembe, kwa sababu nilitekeleza agizo la kujaza fomu iliyonitaka kuorodhesha mali zangu na nilifanikiwa kurejesha Desemba 22, mwaka jana hivyo kosa si langu bali ni tatizo la kimasijala,” alisema.

Aidha, aliliambia baraza hilo kuwa tatizo la malalamiko ya kushindwa kurejesha fomu, amelisikia kwa baadhi ya wabunge ambao wengi wao wanalilalamikia kwa kuwaita katika baraza japokuwa walirejesha fomu hizo.
Kwa upande wake, Vultan Kundy alisema tangu alipoajiriwa kuwa hakimu katika mahakama ya mwanzo ya Isevya wilayani Mpanda mwaka 2008, hajawahi kujaza fomu hizo kutokana na kushindwa kuzipata kwa wakati.

Hata hivyo, baraza liliwaachia watuhumiwa kuendelea na shughuli zao kwa lengo la kusubiri maamuzi yatakayotolewa baadaye dhidi yao

Monday, June 20, 2011

Jalada la ajali ya Jaji Lugazia kutua mahakamani

 Imeripotiwa katika gazeti la majira kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Eliezer Fereshi, amesema upelelezi wa tukio la ajali ya gari iliyokuwa ikiendeshwa Jaji Projestus Rugazia, umekamilika najalada la shauri hilo litafikishwa mahakamani wakati wowote.Katika ajali hiyo iliyotokea jijini Dar es Salaam, Oktoba 3, mwaka jana mtu mmoja, Salehe Omary wa Msasani Dar es Salaam, alikufa na wengine watatu kujeruhiwa.
Bw. Fereshi alitoa kauli hiyo alipozungumza na gazeti la majira  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja yanapofanyika Maonesho ya Wiki ya  Utumishi wa Umma.Bw. Fereshi alisema ofisi yake ilikuwa ikisubiri kukamilika kwa  upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamani.Alisema jalada lake hiyo litafikishwa mahakamani siku yoyote kama inavyofanyika kwa wengine.

"Kulikuwa na upelelezi, sasa umeshakamilika na tutapeleka mahakamani jalada hilo," alisema Bw. Fereshi

Jaji Rugazia (56) mkazi wa Ada Estate Kinondoni Oktoba 3, mwaka jana alipata ajali iliyosababisa gari lake kugonga magari matatu, ambapo mtu mmoja alikufa na wengine wanne kujeruhiwa.Waliojeruhiwa ni Issa Idd (30) mkazi wa Kinondoni, Nasibu Hassan (28), mkazi wa Kitunda na mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), aliyejulikana kwa jina moja la Rahma.

Jaji Rugazia ambaye naye aliumia katika ajali hiyo, alikuwa akiendesha gari namba T.780 ACB aina ya Toyota Land Cruiser Prado.

Magari aliyogongwa ni T.776 AZK Mitsubishi Pajero, T.213 AZR Toyota Spacio, T.104 BHY Daihatsu Teriors, T.395 AKU Toyota Corolla na T.312 ACB Suzuki Escudo.

Aliyekua Raisi wa Tunisia:atiwa hatia, ahukumiwa miaka 35 jela(kesi yamalizika siku1)


Aliyekua Rais wa Tunisia Ben Ali

Mahakama moja nchini Tunisia imemhukumu rais wa zamani Zine al-Abidine Ben Ali na mkewe Leila kifungo cha miaka 35 jela kwa ubadhirifu na utumiaji mbaya wa mali ya uma.Wawili hao, ambao walikimbilia Saudi Arabia mwezi Januari baada ya mapinduzi ya kiraia, pia wametakiwa kulipa faini ya dola milioni $66m.

Kesi hio iliyofanywa siku moja pekee na bila washtakiwa kuwepo mahakamani iliangazia pesa na vito vya thamani vinavyosemekana kuwa dola milioni $27m na ambazo zilipatikana katika moja ya kasri zao.

Jaji anayesililiza kesi hio alisema uamuzi juu ya mashtaka mengine, kuhusiana na mali haramu ya madawa ya kulevya na silaha, utatamkwa Juni 30.Ben Ali walikimbilia Saudi Arabia Januari 14 katika uso wa mapigano maarufu dhidi ya utawala wake wa miaka 23 .
Mahakama ambayo kesi dhidi ya Ben ali ilisikilizw
Wakili wa Ben Ali Akram Azoury amesema kuwa hukumu hiyo ilitolewa kwa misingi ya kisiasa na "ni mzaha alisema awali kwamba mteja wake "mteja wake anakanusha kwa nguvu  madai yote yanayelekezwa kwake na kwamba yeye si mwenda wazimu kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kinachodaiwa kupatikana katika ofisi yake".

Mchakato wa kusililiza kesi hiyo pia ulikosolewa na wadau mbalimbali , "Mchakato haukuwa wa kuridhisha, alisema " Zied Cherni, mwanasheria wa Tunisia,.""Unaweza kukaa na kuuliza, kwa nini adhabu yake ije sasa hivi?" alisema, akibainisha muktadha mpana wa kisiasa katika nchi ya Afrika Kaskazini. "Kuna serikali kivuli, ambayo ni haki ya sasa kujaribu kuendesha na fitna watu Tunisia." 

TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA NA SILAHA 

Ben Ali, kiongozi wa kwanza kuangusha katika wimbi la machafuko ya Kiarabu, anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na wizi wa madawa ya kulevya na silaha, kufuatia ugunduzi taarifa ya karibu $ 27m katika vyombo vya dhahabu na fedha pamoja na madawa ya kulevya na silaha katika majumba mawili nje Tunis.Kati ya kesi 93 zinazomkabili Ben Alia, 35 ya kesi hizo zitasikilizwa katika mahakama wa kijeshi.


 BEN ALI ANAJIBU NINI?
Sheria za Tunisia inakataza mwanasheria kutoka nchi ya kigeni  kutetea mteja kama hayupo, maafisa wa mahakama wamesema hayo hivyo kumnyima nafasi Mwanasheria wa Ben Ali kutoka ufaransa Jean-Yves Le Borgne, kushiriki katika kesi hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na Le Borgne, Ben Ali " kwa nguvu anakanusha" shutuma dhidi yake, kwa madai kwamba  silaha zilizopatikana ilikuwa ni zawadi kutoka kwa  wakuu mbalimbaliwa nchi.

"Taarifa ya kypatikana na madawa ya kulevya ni uongo na fedheha... Ni suala la kusikitisha na kukashifu,'' Mwanasheria huyo ilisema .Saudi Arabia haijajibu maombi extradition, na baadhi  ya watunisia walionyesha kuchanganyikiwa kwamba Ben Ali bila kuwepo kwa hukumu yake.

Kituo cha sheria kutetea waliouawa kinyama Selous


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimejitosa katika sakata la mauaji ya wanakijiji wawili wa Cholesamvula ambayo yanadaiwa kufanywa na  askari wa wanyamapori katika Hifadhi ya Selous mkoani Pwani Februari mwaka huu.Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtafiti msaidizi wa kituo hicho, Pasience Mlowe alisema hivi sasa polisi Pwani inawasiliana na ofisi za hifadhi hiyo zilizopo Morogoro ili kuweza kuwatia mbaroni watuhumiwa.

Alisema wameanza kulishughulikia suala hilo ili kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa mbele ya sheria ili haki itendeke na wiki iliyopita walikuwa Kijiji cha Kwala kupata ukweli kuhusiana na sakata hilo ambako walizungumza na Kigwiso Mfanyeje ambaye alinusurika katika tukio hilo.“Tulienda kijijini walipokuwa wanaishi marehemu na kuzungumza na watu wengine na tumefanya mawasiliano na mkuu wa upelelezi wa wilaya pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani ambao wametoa ushirikiano mkubwa”alisema Mlowe.

Alisema wamewasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema na barua imepatikana kutoka ofisi hiyo kwenda ya wanyamapori ambayo ipo Morogoro na wakati wowote watuhumiwa watatiwa mbaroni ili manusura wa tukio hilo, Mfanyeje aweze kwenda kuwatambua.“Unajua polisi wana namna zao za utendaji kazi na ilipofikia ni kuwa barua kutoka kwa IGP kwenda Ofisi ya wanyamapori ililiyopo Morogoro imekwenda na watakuwa wameipata hivyo, wakati wowote watuhumiwa watatiwa mbaroni” alisema.

Mlowe alisema ni kweli tukio hilo lilitokea na linasikitisha na alilipongeza gazeti la Mwananchi kwa kufuatilia tukio hilo ambalo kama lisingeripotiwa pengine lingepita bila kufahamika kutokana na wakazi wa eneo hilo kudai kuwa kuna visa vingi vya watu kuuawa au kutoweka mara wanapoingia katika eneo hilo la Selous.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absolom Mwakyoma hakuweza kupatikana kuweza kuzungumzia zaidi suala hilo na simu yake muda mwingi ilipopigwa iliita bila kupokelewa. Tukio la mauaji hayo lilitokea Februari 2 mwaka huu na katika tukio hilo watu wawili  wanadauwa kuawa askari hao.

Waliouawa ni pamoja na Hamisi Feruzi ‘Boy’na Mohamed Sutta wakati Mfanyeje Kigwiso alijeruhiwa na hadi hivi sasa ana kilema kutokana na mkono wake wa kushoto uliopigwa risasi kupoteza uwezo wa kufanyakazi.

Tukio hilo liliripotiwa Polisi Kisarawe ambao walienda hadi eneo la tukio na kukuta mabaki ya mafuvu moja likiwa limechomwa moto, viungo vingine na mabaki ya nguo ambazo ndugu wa marehemu waliokuwa katika msafara huo wa polisi waliweza kuzitambua kuwa ni za ndugu zao. Chanzo gazeti la Mwananchi.

Muasia aliyeficha maiti sandukuni ahukumiwa kunyongwa hadi kufa.


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania,Kanda ya Dar es salaam imemhukumu mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia, Vinoth Plavin Nadhesan, kunyongwa kwa kamba hadi kufa, baada ya kupatikana na hatia ya kumwua mwenzake kwa kumchoma visu na mishale. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Faudh Twaibu, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka.

Jaji Twaibu alisema mazingira ya kesi yanaonesha kuwa mshitakiwa alimwua Abdulbassit Abdallah, mkazi wa Dar es Salaam, kwa kukusudia na si kwa kujitetea kama anavyodai. “Mshitakiwa amepatikana na hatia ya mauaji na hukumu yake ni kunyongwa kwa kamba hadi kufa, kama hajaridhika na uamuzi huu ana haki ya kukata rufaa,” alisema

Alisema Mahakama inaamini taarifa za Polisi kuliko ushahidi wa upande wa utetezi uliotolewa mahakamani hapo, kuwa Abdallah ndiye aliyeanzisha ugomvi kwa kumpiga Nadhesan kwa fimbo, kwani ushahidi huo kwa mujibu wa Jaji Twaibu, ni wa kujitetea. Kwa mujibu wa taarifa za Polisi zilizotolewa mahakamani hapo kwa ajili ya ushahidi, mshitakiwa alikiri kuua katika kituo cha Polisi na mbele ya shahidi na wakati akikiri, alimtaka askari asipeleke shahidi wakati akitoa maelezo yake.

Kwa mujibu wa ushahidi huo wa Polisi, Nadhesan alisema hahitaji shahidi wakati wa kutoa maelezo yake Polisi, kwa kuwa wakati anaua, alikuwa peke yake na aliamua kumweleza ukweli askari huyo kwa kuwa alimjali.

Awali ilidaiwa mahakamani kuwa Februari 6 katika eneo la Kariakoo mtaa wa Kipata, Nadhesan alimwua Abdallah kwa kumchoma na visu vya jikoni.

Mbali na kumchoma visu hivyo, Nadhesan pia alimchoma Abdallah na mshale mgogoni, tumboni, shingoni na mdomoni na kuuweka mwili wake kwenye begi na kulitelekeza ndani ya gari katika maegesho ya magari ya jengo la JM Mall (Habour View).

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, chanzo cha ugomvi huo ni fedha na ulianza Abdallah alipomkopesha mshitakiwa dola 20,000 za Marekani, kwa makubaliano ya kumlipa baada ya mwaka mmoja. Katika utetezi wake, Nadhesan alidai kwamba Abdallah ndiye aliyeanzisha ugomvi kwa kumpiga fimbo na ngumi na katika kujitetea, alichukua kisu na kumchoma nacho.

Nadhesan alijitetea kwamba alipoona Abdallah anapiga kelele, alimchoma mshale kwa kuhofia kwamba kama angenyanyuka, yeye angekuwa hatarini. Ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulionesha kuwa mwili wa marehemu ulikutwa na vipande vya mishale mdomoni. Kwa Mujibu wa vifungu vya 196 na  197 vya Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 16 kama ilivyofayiwa marekebisho mwaka 2002, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuua au kusababisha mauji wa mtu mwingine. Mtu yoyote anayetiwa hatiani na kosa la mauaji adhabu yake ni kuhukumiwa kunyongwa mpaka Kufa. Hata hivyo hukumu hiyo ya kifo japokua kwa miaka ya hivi karibuni haijaekelezwa kwa muuaji yeyote inapingwa kwa kiasi kikubwa na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu nchini na duniani kwa ujumla, kwamba inakinzana na kifungu cha 14 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inyobainisha ya kwamba Kila mtu anay haki ya kuishi.

Nadhesan alikamatwa na Polisi katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Februari 7 akijiandaa kutoroka kwenda India.

Saturday, June 18, 2011

Kambi ya upinzani kumshtaki Mh. Makinda


KAMBI ya Upinzani Bungeni imemshtaki Spika, Anne Makinda katika Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ikimtuhumu kumkingia kifua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda asiwajibishwe na Bunge.Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Spika Makinda kuzuia kujibiwa kwa swali la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kuhusu sababu za Serikali kutowafikisha mahakamani askari polisi waliohusika katika mauaji ya raia 72 yaliyofanyika katika kipindi cha kati ya mwaka 2008 na mwaka huu.

Mbali ya Lissu, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Esther Matiko naye alitaka kupata maelezo kutoka kwa Waziri Mkuu ya sababu za kutofikishwa mahakamani kwa askari waliohusika na mauaji ya raia katika eneo la Nyamongo, wilayani Tarime.

Wabunge hao walifanya hivyo wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, yanayoulizwa kila Alhamisi wakati Bunge linapokutana.

Spika Makinda alizuia kujibiwa kwa maswali hayo kwa maelezo kuwa masuala hayo yako mahakamani na kwamba kuyajibu kutakuwa ni kuingilia uhuru wa Mahakama ambayo mara kadhaa, imelilalamikia Bunge kuwa limekuwa likiingilia huru wake.

Maelezo hayo yalionekana kutoiridhisha Kambi ya Upinzani ambayo iliamua kumshtaki Spika katika Kamati hiyo ili ichunguze uamuzi wake na baadaye kutoa uamuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye pia Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chadema, alisema tayari kambi yake imeshakamilisha maandalizi ya hati ya malalamiko ya wabunge hao na kwamba ingewasilishwa kwa Katibu wa Bunge jana jioni.

“Tusingependa kufanya hayo maana vinginevyo tunaonekana kama tunahoji uwezo wa Mheshimiwa Spika, lakini hatuna jinsi imebidi. Tumempeleka katika Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge kwa sababu kuacha uamuzi potofu wa Spika wa Bunge usimame, itakuwa ni ‘precedent’ (kitangulizi cha jambo) ya hatari kwa Bunge letu kwa sababu uamuzi huo kuachwa bila kupingwa, unaweza kutumiwa katika mijadala mingine katika siku zijazo,” alisema Lissu.

Alisema vitendo hivyo vya Makinda ni vya ukiukwaji wa kanuni za kudumu za Bunge na kwamba katu Kambi ya Upinzani haitakuwa tayari kumwacha aendeshe Bunge kama anavyoona binafsi.

“Spika wa Bunge ana mamlaka makubwa sana kiuamuzi, lakini anatakiwa kufuata kanuni na kanuni kuu muda wote ni ya nane inayomtaka kuendesha shughuli za Bunge na kutoa uamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba, sheria na kanuni,” alisema Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria.

Lissu alisema Spika Makinda pia anapaswa kufuata uamuzi wa maspika waliomtangulia na kuzingatia uzoefu, mila na desturi za mabunge mengine yanayofuata utaratibu unaofafana na kufuatwa na Bunge la Tanzania.

Mbunge huyo alidai kwamba hiyo si mara ya kwanza kwa Spika Makinda kutoa uamuzi ulioonekana kumkingia kifua Waziri Mkuu wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

“Itakumbukwa kwamba wakati wa Mkutano wa Pili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliofanyika Februari mwaka huu, Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika kutokana na kauli ya uongo iliyotolewa na Waziri Mkuu kuhusu mauaji ya Arusha. Baada ya kutoa mwongozo alioombwa, Spika wa Bunge alimkemea Mheshimiwa Lema na kumtaka athibitishe kauli yake juu ya uongo wa Waziri Mkuu,” alisema Lissu.

Alisema hata hivyo, Lema alipotoa uthibitisho wake, Spika Makinda alizima mjadala kwa kukalia uthibitisho wa Lema... “Hadi leo Watanzania hawajaambia chochote juu ya jambo hilo, lakini kuna siku tutakumbushia hilo ili wananchi wajue ukweli.”

Mbunge huyo alidai kwamba uamuzi wa Spika kuhusu swali lake, aliufanya bila kuuliza au kupewa taarifa sahihi kuhusu mauaji ya Tarime na kesi dhidi yake na wenzake.

“Hii ni hatari sana kwa uendeshaji bora wa Bunge, kama Spika ambaye pia ni kiongozi wa Bunge atakuwa anatoa uamuzi ambao hana taarifa sahihi juu yake… hadhi na heshima ya Bunge itashuka kwa sababu wananchi wataona Spika anatoa uamuzi kwa lengo la kuwakingia kifua mawaziri na Serikali ili wasiwajibishwe bungeni. Hii ikitokea ni hatari kwa demokrasia yetu kibunge,” alisema.

Alisema yeye na wenzake saba wanakabiliwa na mashtaka ya kuingia kijinai katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, kufanya mkusanyiko haramu katika eneo hilo na kuwazuia Mganga wa Hospitali ya Wilaya na askari polisi kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu waliouawa katika Mgodi wa Nyamongo na kwamba mashtaka hayo si ya mauaji na kwamba haikuwa sahihi kwa Spika kuzuia maswali yake.

Alipoulizwa juu ya imani yake kwa Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Lissu alisema hana sababu za kuamini kwamba pamoja na kuwa ina idadi kubwa ya wabunge wa CCM, itaacha uadilifu wake na kupindisha haki.

Mbunge huyo alisema kwa mujibu wa kanuni, wakati kamati hiyo yenye wajumbe 15 itakapoketi kuchunguza malalamiko hayo, Spika ambaye pia ndiye wake na naibu wake, watapaswa wasikalie kiti hicho na badala yake, wajumbe watamchagua mmoja wao kuendesha kikao cha uchunguzi.

Alipotakiwa kuzungumzia hatua hiyo, Makinda ambaye jana asubuhi hakuendesha Kikao cha Bunge alijibu kwa simu: “Niko kwenye kikao." Alipotafutwa tena, simu yake ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alisisitiza kuwa bado alikuwa katika kikao. Chanzo gazeti la Mwananchi.

Wanafunzi waliolawiti wahukumiwa.

NAFUNZI wawili wa darasa la saba katika shule ya msingi Kidugalo wilayani Morogoro, wamehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko sita kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi mwenzao.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Jafari Mzonge wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa  mahakamani hapo. Wanafunzi hao, Salama Said (14) na Shaaban Kefa (14), walimlawiti mwanafunzi mwenzao wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 12 na kumsababishaia maumivu. 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mzonge alisema ametoa adhabu hiyo kali kwa watoto hao baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka.Hakimu Mzonge pia alisema amefikia uamuzi huo wa kutoa adhabu ya viboko kwa kuzingatia kwamba wanafunzi hao bado watoto na ni kosa lao la kwanza.

Awali, akisoma maelezo ya kosa, Mwendesha Mashitaka Salehe Kalulu, alidai kuwa washitakiwa walitenda kosa Novemba 26, mwaka jana, saa 12.30 jioni, katika kijiji cha Kidugalo, Ngerengere.Hata hivyo, alidai kuwa adhabu iliyotolewa kwa wanafunzi hao ni ya kuridhisha kutokana na umri mdogo walionao na hivyo si vyema kuhukumiwa kifungo ikizingatiwa ni kosa lao la kwanza.

Alidai pia hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa wanafunzi wengine wenye tabia kama hiyo na kuwaonya kutoendelea na vitendo hivyo.

Ajinyonga kwa kukatazwa kuoa Mke wa Pili.

MKAZI wa kijiji cha Ubinga kata ya Mhugi, Tabora, Bundala Mwandu (26) amejinyonga baada ya walezi wake kumkataza kuoa mke wa pili. Akithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nzega, Issa Muguha, alisema Mwandu alikutwa amejinyonga Juni 13 saa nne asubuhi katika kijiji hicho.

Muguha alisema, kabla ya kujinyonga, Mwandu alikuwa na mke mmoja na alitaka kuoa wa pili, lakini alipopeleka taarifa hiyo kwa walezi wake, hawakukubaliana na uamuzi huo. Baada ya taarifa hiyo kukataliwa, Mwandu alifikia uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya gome la mti.

Akizungumza na gazeti hili, babu wa Mwandu, Bulabo Kinimba, alisema alipopata taarifa ya mjukuu wake kutaka kuoa mke wa pili, alimshauri asubiri mpaka baadaye. Kinimba alisema alimshauri kwamba kwa sasa umri wake hauruhusu kubeba majukumu makubwa ya familia mbili.

“Nilimwambia asubiri baadaye ndipo angeze mke wa pili, kwani bado ana umri mdogo, nashangaa kijana wangu amefikia uamuzi huu,” alisema babu huyo.

Jaji Mkuu awaonya wanasisa.

Mh. Jaji Mkuu(Mwenye suti nyeusi)akionyesha Vitabu akiwa na IGP Mwema.
VIONGOZI wa siasa nchini wametakiwa kupanda mbegu za maadili mema kwa wafuasi wao, huku wao wenyewe wakionesha mfano wa kuwa mstari wa mbele kutii sheria za nchi. Aidha, wametakiwa kuelewa, kwamba tafsiri ya kupenda nchi si kufanya harakati za kuchochea ukiukwaji wa sheria.

Hayo yalisemwa jana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, katika hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu utii wa sheria bila shuruti uliofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

Alisema uzinduzi wa kampeni hizo umekuja kwa wakati mwafaka, hasa katika kipindi ambacho nchi imekumbwa na matukio ya wananchi kujifanya wanadai haki, lakini bila kuzingatia wajibu walionao kisheria.

Katika hotuba yake, aliyoitoa mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwamo makamanda wa Polisi wa mikoa yote nchini, wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na wa asasi za kiraia, alisisitiza juu ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa vitendo, kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Jaji Mkuu pia aliwataka viongozi wa dini kuelewa kwamba wana wajibu mkubwa wa kuongoza dhamira za wafuasi wao kutenda mema, kuhimiza na kulinda maadili ya jamii kwa ajili ya kujenga amani na umoja wa kitaifa.

Kwa upande wa asasi za kiraia, alisema nazo zina jukumu kubwa kwa umma wa Watanzania wanaopaswa kupewa elimu chanya ya uraia na uzalendo, huku wakitimiza maadili mema ya kitanzania.

“Wananchi wetu wakitii sheria bila kushurutishwa, watavisaidia vyombo vyenye mamlaka ya utoaji haki kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi zaidi.

“Aidha, kutaiwezesha jamii kuishi kwa amani, usalama na utulivu, kupunguza hali ya watu kuishi kwa mashaka na wasiwasi, kupunguza matumizi ya nguvu na kuimarika kwa uhusiano wa kiutendaji kati ya vyombo vya Dola na wananchi,” alisema Jaji Mkuu aliyeonesha kukerwa na tabia za baadhi ya wananchi kujichukulia madaraka ya vyombo vingine vya Dola kwa kuchukua uamuzi kinyume na utaratibu uliowekwa kisheria.

Akimkaribisha Jaji Mkuu kuzindua kampeni hiyo, IGP Mwema alisema kampeni hiyo itakayosambaa hadi ngazi za mashina, inalenga kuwaamsha na kuwapa hamasa Watanzania kuirejea misingi ya uwajibikaji katika harakati za kudumisha amani, usalama na utulivu, kama mtaji wa kujiletea maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini.Chanzo gazeti la Habari leo.

Thursday, June 16, 2011

Mtikila Kuishitaki Serikali Mahakama ya Afrika:Adai Mabilioni.

Mchungaji Christopher Mtikila,

MWENYEKITI wa Chama Cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ametangaza kesi mpya nne za kimataifa dhidi ya serikali ikiwemo madai ya fidia ya dola zamarekani milioni 150.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salama jana, Mchungaji Mtikila alisema amefungua kesi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na kwamba tayari aliziwasilisha Juni 10 mwaka huu na itaanza kusikilizwa muda wowote kuanzia sasa.

Alisema kesi hizo nne dhidi ya serikali pia ina kipengele alichodai kuwa ni kubatilishwa kwa uhuru wa Tanganyika na muungano pamoja na baadhi ya vipengele vya katiba.Alitaja vifungu vya katiba anavyopinga kuwa ni ibara ya 39, 67 na 77, kufungwa jela mwaka mmoja kwa kile 'bila kosa' na madai ya mke wake, Bi. Georgina Mtikila kudhulumiwa mamilioni ya fedha.

Alisema katika kesi hizo anatetewa na jopo la wanasheria waandamizi sita wa kimataifa ambao walikuwa wa Umoja wa Mataifa (UN).Aliwataja wanasheria hao wanaosimamia kesi zake kuwa ni Profesa. Setondji wa shirika la Etudes Vihode la Benini, Prof. Charles Adeogun wa shirika la Charles Antony LLP (Nigeria), Profesa Frscis Dako wa Benini wakisaidiwa na Bi. Mary Birdi, Profesa Deogratias Njau na Prof. Megan Thompson wote wa Benini.

Mchungaji Mtikila alidai kuwa kitendo cha uhuru wa Tanganyika kubatilishwa na kuungana na Wazanzibari hakikubaliki na kwamba kinakwenda kinyume cha matakwa ya wananchi.Alisema uhuru huo ndio haki kuu ya watu wote duniani ambao ilisababisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945 (The right to self Determination).

Alisema uhuru wa Watanganyika ni haki ya Watanganyika wenyewe hivyo wana wajibu wa kuutunza uhai wao katika mipaka ya ardhi kwa utaratibu wao wenyewe kwa kutumia maziwa na asili yao.Alidai kuwa Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere, anastahili kuhukumiwa hata kama ni marehemu kwa kuhusika katika kuwapunguzia Watanganyika ubinadamu na kulazimishwa kuwa 'watumwa wa Wazanzibari'.

Mchungaji Mtikila alitoa mpya pale alipodai kuwa katika orodha ya watuhumiwa hao, Hayati Nyerere yumo na atahukumiwa kama akipatikana na hatia kwa sababu alilazimisha watu kuwa 'watumwa wa nchi nyingine jirani' na kupunguza umuhimu wao na hatimaye kupoteza kabisa utambulisho wa nchi yao Tanganyika.

"Tunataka mahakama ya kimataifa itupatie haki ya uhuru wetu (The right to self determination of the people of the Republic of Tanganyika) kama binadamu wengine wote katika mipaka ya nchi zao, tunaiambia mahakama ya ulimwengu kwamba muungano ni kongwa la utumwa katika chingo la Tanganyika," alisema.

Kuhusu kufungwa mwaka mmoja jela alisema kuwa alifungwa kwa sababu ya kukemea na kukaripia kuhusu alichokiona juu ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Marehemu Horace Kolimba ambapo mahakama ya rufani ilimuhuku kutokana na kauli alizozitoa kama kiongozi wa dini.

Alidai amefungua kesi upya katika mahakama hiyo akitaka serikali kumlipa dola milioni 150 za kumfunga na kumdhalilisha bila kosa.

Alisema madai ya mke wake alifikishwa mahakamani mwaka 1984 na kuendeshwa kisiasa na hatimaye kutolewa hukumu mwaka 1994 kwa kuyatupilia mbali. Habari hii chanzo chake ni gazeti la Majira.

Mbaroni kwa kulawiti mtoto wake wa kambo

MKAZI wa Kahe Madukani, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, Idd Hashimu (25) anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka sita ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kahe.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Yusuph Ilembo, alisema tukio hilo lilitokea Juni 14 majira ya saa 6:00 mchana nyumbani kwa mtuhumiwa huyo Kahe Madukani wakati mama wa mtoto huyo alipokuwa shambani.Alisema siku hiyo mwanaume huyo alimwita mtoto huyo chumbani na kumziba mdomo kisha kumfanyia kitendo hicho.

Alisema kabla mama wa mtoto huyo hajaenda shambani asubuhi aliacha maagizo kwa mtoto huyo na wenzake wawili wafue nguo na aliporudi majira ya saa 12:00 jioni alikuta nguo hazijafuliwa na alipouliza sababu ya kutofuliwa alijibiwa na mtoto huyo kuwa yeye alikuwa chumbani na baba.Alisema majibu hayo yalimlazimu mama huyo kumchunguza zaidi mtoto wake ndipo mtoto huyo alipomweleza hali halisi na kumfanya mwanamke huyo kutoa taarifa polisi na baadaye mtoto huyo alipelekwa hospitali na kutibiwa kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Wednesday, June 15, 2011

Mbunge asimamishwa: Adai 15% ya wabunge wenzake ni Mashoga.

Mh.Mille Othiambo

Mbunge pichani hapo juu, jana jioni katika kikao cha kupitisha majina ya wateuliwa wa nafasi za juu za Mahakama nchini kenya aliibua mtafaruku mzito baada ya kudai asilimia 15% ya wahesimiwa wabunge wa Jumba hilo ni Mashoga. Madai hayo yalichafua hali ya hewa la Bunge hilo, na yalipingwa kupingwa vikali kutoka kwa wabunge wenzake. Hali hiyo ilimlazimu Naibu Spika wa bunge hilo  Farah Maalim kumuomba Bi Odhiambo kuondoa au kufuta  matamshi yake pamoja na kuomba msamaha.

Bi. Othiambo alitamka maneno hayo wakati wa majadiliano bungeni humo, kuhusiana na kupitishwa au kutokupitishwa kwa majina matatu yaliyopendekezwa kwa ajili, ya Jaji Mkuu wa kenya, Naibu wake pamoja na Mkurugenzi wa makosa ya jinai.

Bi Odhiambo alikataa kuomba radhi wala kufuta usemi wake kwani alisema madai anayoyasema yametokana na utafiti uliandikwa katika ripoti ya  mwanaharakati Betty Murungi wakati mwanaharakati huyo  alipohojiwa mbele ya Kamati ya Utekelezaji na Usimamizi wa katika,wakati wa zoezila uteuzi wa wagombea mbalimbali wa nafasi hizo za juu katika Mahakama. Mbunge huyo alinukuliwa akisema:  "I am merely reporting what was said to us before the committee. Mr Speaker if you want to get me out because of that I am happy; I will leave,". 

Hali hiyo ilimfanya Waziri wa Sheria Mutula Kilonzo kusema kwamba madai ya ripoti zilionyesha kuwa asilimia 15 ya Wakenya walikuwa mashoga na ripoti hio haikusema , hakufanya kumbukumbu yoyote maalum kwamba  asilimia hio ya wabunge ni Mashoga.

Kutokana na Mbunge huyo kukataa kukanusha usemi wake, Naibu spika akisoma Kanuni na 197 na 198 ya Bunge hilo, alimsimamisha Bi.Othiambo asihudhulie vikao viwili vya Bunge."Kwa mujibu wa masharti katika Kanuni ambazo nimezitaja ninamsimamisha Mheshimiwa Millie Odhiambo asihudhulie Bunge kwa siku mbili," alisema.Cha kustaajabisha kabla naibu spika, hajamaliza kutoa hukumu yake Mbunge huyo aliamua kutoka nje ya kikao vya Bunge.

Hata hivyo wabunge walionekana kutokuridhika na hawakua na furaha na adhabu hiyo didhi  ya Bi Odhiambo Ndipo Mh.Mbunge Bifwoli Wakoli kusema ahabu hio ni ndogo, ingefaa Mh.Othiambo asimamishwe kwa muda wa mwaka mmoja kutoingia Bungeni. 

Naibu Spika vilevile alikubaliana na Mbunge Mwingine,Asman Kamama aliyeomba  hotuba ya Bi Odhiambo ni kuondolewa kutoka Hansard ambapo taarifa zote rasmi hurekodiwa.

Kikao hicho cha kupitisha majina ya wagombea, kilimamlizika mida ya usiku kwa wabunge kupitisha majina ya walioteuliwa kuwa Jaji Mkuu,Makamu wake na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai wa Kenya.



Ashtakiwa kwa jaribio la wizi wa Senti 99(1500 Tsh).

Christopher Tisley

Jamaa hapo pichani ameshitakiwa kwa  jaribio la wizi kwa kutumiwa silaha, Baada ya kumtishia bastola  karani wa duka moja huko Marekani, ili ampe senti 99 za dola ya kimarekani alizokua nazo sawa na shilingi 1500 za kitanzania.

Kulingana na  taarifa  iliyotolewa Mahakama  hapo, Christopher Tisley, 34,  alitembelea maeneo ya Magharibi mwa  Lawrence Avenue huko  Marekani na kumdai karani huyo fedha, karani huyo alipokataa mtuhumiwa huyo alitoa bunduki na kuanza kumtisha nayo.

Tisley,ambae ni mkazi wa Morgan Street, aliamuatoka nje  ya duka hilo baada ya mteja kuingia katika duka hilo, hivyo kumpa mwanya karani huyo kufunga mlango kwa ndani. Japo mlango ulifungwa jamaa huyo aliendelea kugonga malango na madirisha akilazimisha apatiwe pesa. 

Polisi walipofahamishwa walikuja na kukamata  Tisley, japo silaha kwa wakati huo hakua na silaha inayodaiwa alitumia kutishia. Waendesha mashitaka wanasema jamaa huyo alipatikana na gramu 3 ya methamphetamine(unga wenye kemikali) katika milki yake.  

Jaji wa mahakama anayostakiwa jamaa huyo alisema dhamana ya njemba huyo ni Dola 50,0000 sawa na zaidi ya shillingi Millioni 65,000,000/= za kitanzania. Tishley anashitakiwa kwa jaribio la kujipatia mali kwa nguvu na  milki ya mali isiyoruhusiwa.