Powered By Blogger

Thursday, July 26, 2012

WAFANYAKAZI GGM WAGOMA: SABABU YA MAFAO YA KUJITOA.

Picha ya Maktaba: Wafanyakazi wakiwa kazini
 
Wafanyakazi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine(GGM) wamegoma kufanya kazi sababu kuu ikiwa kupinga sheria  ya mafao ya kujitoa inayowanyiwa wafanyakazi fursa ya kuchukua malipo hayo wanapoacha kazi hadi pale watakapofikisha umri wa kustaafu.  Hali hiyo ilimlazimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uzimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)Bwana Afrikanus Mushi kuzungumza na wafanyakazi hao kwa takriban masaa matatu na kuwaomba warejee kazini, mpaka mamlaka hiyo itakapotoa na kufanya upembuzi yakinifu baada ya mwezi mmoja.
Wafanyakazi kusubiri kama mzee huyu ili wapate mafao
Kauli hii ya Mkurugenzi Huyo wa inakuja baada ya Mamlaka hiyo kupitia katika kitengo chake cha mawasiliano na uhamasishaji kutoa taarifa kwa umma  kwamba “Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya  kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa wadau”. Haileweki kama kikao hicho cha Mkurugenzi Mkuu na Wafanyakazi wa GGM, kutabadilisha hali hiyo ndani ya kipindi kifupi cha Mwezi mmoja.

Wakati huo huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii(facebook, twitter na blogs mbalimbali) wadau wa mitandao hiyo wametoa maoni yao kama ifuatavyo:

Stanslaus Nyambea aliandika: Sheria Kandamizi ya Mafao ya kuacha kazi kabla ya kustaafu yapitishwa Tanzania.Sheria ina mapungufu makubwa ya kisheria:
1. Ina viashiria vya kibaguzi vya waziwazi, yaani mfuko wa hifadhi wa wabunge unasema wanapewa mafao soon after bunge likifa. Kwanini na wao wasiwekewe limit ya miaka 55?-Ubaguzi huu!

Pili, inalazamisha na kuamua matumizi ya mtu binafsi, eti mkopo wa nyumba kwa watu hawa utatolewe na mfuko, wakati hata ukiisha miaka 1000, hutaweza kulipa. Mosi, Kijamii hii sheria ni ya kupuuzi sana; mosi inashau sisi tulioko kwenye sekta binafsi ajira zetu ni za muda.wengi tunajiandaa kwenda kusoma kutumia hizo hela za mafao.

Kisiasa, tunajua kuwa serikali yetu ni mfilisi, haina fedha kwakuwa zinaibwa, hivyo njia pekee ni kuiba fedha zetu za mifuko ya hifadhi kujenga barabara, majengo na kutimiza ahadi za kipuuzi za rai.

Novatus Rukwago aliandika:Hapa kuna maswali machache makubwa ya msingi ya kujiuliza hat kama hatujaanza kutafuta tufanye nini. Hivi hii imepitishwa na nani? 2. Kama ni wabunge tunaowaita wawakilishi wetu, wamefanya hivyo kwa maslahi ya nani?. 3. Je Rais ameshaisain au la. Kama bado, je amesikia kilio cha wnanchi wake? Na kama tayari je alijua alichosain?. Tukipata majibu sahihi ndo tuulizane tufanye maamuzi kwaajili ya leo na kwaajili ya kesho. Mungu atunusuru na msiba huu

Mwingine alisema’ Hiyo Miongozo HATUITAKI.. Mtushirikishe kwenye Miongozo wakati wa KUTUNGA sheria ambayo inatuhusu sisi wenyewe wafanyakazi Hamkutushirikisha why NOW matake kutushirikisha kwenye MIONGOZO? Non Sense kabisa, Hivi wewe mtu amefanya kazi miezi mitatu na kibarua kikaisha na mtu alikuwa analipwa 120,000 Hiyo NSSF yake unajua ni how Much?mpka aisubirie kwa mpk afike miaka 60 na ajira zenyewe hizi za kubangaiza ambazo serikali inaangalia tu wanapewa wageni wazawa tunaachwa unategemea hizi siku zote anaishi vipi? hiyo sheria nafikiri inaweza fanayakazi serikalini ambako watu huwa hawafukuzwi kazi, Kazi inaisha siku anastaafu akiwa na hiyo miaka 60, sisi wa sekta Binafsi Mnatuonea tu, Vimishara venyewe ndo hivyo vya tia maji tia maji, leo hii nimeachishwa kazi nina Miaka 30 ndo ni wait tena 30 years nipewe Hifadhi yangu KWELI? Are you Serious?Please msiwe kama watoto. Hata hii Mamlaka kweli inawatu wenye HEKIMA na BUSARA kweli?Nahisi ni mradi tu wa Mtu, Hiyo mifuko ya jamii yenyewe inapiga Deal kinoma na Hela zetu lakini hatupewi Share kwenye hiyo Miradi wala Riba!Basi wangekuwa hata wanatudanganyishia kutuwekea mdhamana kwenye Mabenki tuwe twapata Mikopo ya Kununua Nyumba za NHC au hata Kupewa Mikopo, As I know kuwa Hii mifuko ya Jamii ina weka Hela zetu kwenye Mabenki kwa FIX deposit accounts..Tunajua yote wanayofanya tuka kaa Kimya NOW ndio mnataka hata hichi kidogo tusikipate,Please Kuweni Serious.


SAKATA LA FAO LA KUJITOA "MAMLAKA YA HIFADHI YA JAMII"YATOA TAMKO.



Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi  huu unakwenda sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari  na kuleta mkanganyiko  miongoni mwa Wanachama na Wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Kufuatia hali hiyo Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:

Marekebisho kuhusu  kusitisha fao la kujitoa  yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha uzeeni.

Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi kutoka  vyama vya wafanyakazi, Chama cha waajiri pamoja na Serikali. 

Kwa kutambua  tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya kazi, tofauti ya  sababu za ukomo wa ajira, na umuhimu wa Mwanachama  kunufaika na michango yake wakati angali katika  ajira, Mamlaka inaendelea na mchakato wa kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya  wanachama. Miongozo na  kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo  wafanyakazi, waajiri na Serikali kabla ya kuanza  kutumika.

Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo maombi mapya ya  kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa wadau. 

Tangazo hili halitowahusu wanachama waliojitoa kabla ya  tarehe 20/07/2012.
Mamlaka inakanusha vikali kwamba  sitisho la fao la kujitoa si  kwasababu za kiserikali au kwasababu mifuko imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na  michango yote ya wanachama ipo salama.

Hivyo, Mamlaka inawaomba wanachama na wadau wote wa  sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea  kwa lengo ya kulinda na kutetea maslahi ya mwanachama.

Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji

SSRA-Makao Makuu

Tuesday, July 17, 2012

JAJI KIONGOZI AKANUSHA MADAI YA TUNDU LISSU.


MH.JUNDU WA KWANZA MBELE


JAJI  Kiongozi Fakhii Jundu amekanusha madai yaliyotolewa na Mnadhimu wa Upinzani Tundu Lisu kuwa majaji wengi wanaoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete huteuliwa bila ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Akizungumza na  mahakimu na wafanyakazi wa Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kinondoni, Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na  Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni, alisema majaji wote wanaoteuliwa na Rais Kikwete wanateuliwa baada ya kufuata taratibu zote ikiwamo na ile ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

“Kumekuwapo na malalamiko kuwa kuna majaji wanateuliwa na Rais bila ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama,  malalamiko hayo si ya kweli hakuna jaji aliyewahi kuteuliwa bila ya kuwapo kwa  ushauri  wa Tume ya Mahakama,”alisema Jaji Kiongozi.Pia  alisema  kumekuwepo na malalamiko  mengi yanayoelekezwa  katika idara za mahakama ikiwamo ucheleweshwaji wa utoaji wa haki, mrundikano wa mashauri mahakamani na kutolewa kwa hukumu zenye utata.

Jaji Jundu alisema  jamii na wadau mbalimbali  wamekuwa wakipeleka malalamiko kwao ya  kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama  Kuu  kuhusu ucheleweshwaji wa utoaji haki katika mashauri yanayowakabili kwa wakati.

Hivyo aliwaagiza mahakimu  kuwahimiza mawakili wa serikali katika kila shauri  kukamilisha upelelezi  haraka iwezekanavyo  na dhamana zitolewe bila ya kuwapo kwa masharti magumu ili kupunguza mrundikano wa mahabusu gerezani.

“Mahakimu wengi wamekuwa wakipenda kutoa adhabu za vifungo kitu ambacho kinasababisha mrundikano wa mahabusu gerezani, angalieni  uwezekano wa  kutumia adhabu mbadala kwa sababu sheria inaruhusu ili kupunguza mrundikano huo wa mahabusu katika magereza, huko hali siyo nzuri,”.Alisema mashauri yanayo suasua wayapunguze mahakamani kwa kuzingatia kanuni ya siku 60 na aliwaonya  kwamba wasiitumie kanuni hiyo vibaya.

Kwa upande wa mashauri yaliyokaa muda mrefu, Jaji Jundu alisema  ‘kama shauri limekaa  muda mrefu, washtakiwa wakiachiliwa huru  kuwakamata ni mchezo unaoiabisha mahakama’.

Jaji huyo  pia aliwataka mahakimu nchini kujipanga, kuwahi kazini na  kusikiliza mashauri kwa wakati na kutoa hukumu mapema  iwezekanavyo zikiwamo kesi za madai.

Aliwasisitiza mahakimu  kuacha  kutumia vifungu vya sheria vya kiufundi vinavyopokonya haki na kusababisha  mrundikano wa mahabusu magerezani.

“Kuna baadhi ya mahakimu katika mashauri ya mirathi  wanajifanya wao ndiyo wagawa mali au wananufaisha watu wengine wasiostahili  na familia husika; hakimu kazi yake ni kuteua msimamizi wa mirathi na si vinginevyo ,”alisisitiza kusema Jaji huyo Kiongozi.

Hivyo aliwataka mahakimu kuepuka rushwa, wamekuwa wakilalamikiwa kuwa wanaongoza kwa kupokea rushwa kitendo ambacho kinaifedhehesha idara hiyo ya mahakama na kuwaonya kuwa wanapopokea rushwa wasione kuwa hiyo ni siri  ikibainika hatua kali zitachukuliwa. Chanzo gazeti la Mwananchi.