Umati nyumbani kwa babu
Baada ya kuona maelfu ya watanzania wanakwenda kwa wingi katika kijiji cha Samunge mjini loliondo kwa lengo la kupata kikombe cha dawa kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Sonjo Mtaa wa Samunge, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilituma watafiti wake mjini Loliondo kuangalia hali ya haki za binadamu katika eneo hilo.
Lengo la ufuatiliaji huu ni kubaini ukiukwaji wa haki za binadamu unaotokea katika kijiji hicho kutokana na maelefu ya watanzania na raia wa kigeni kumiminika kwa wingi katika kijiji cha Samunge.Ufuatiliaji huu ulilenga kuangalia jinsi serikali ilivyo lishughulikia suala hili la huduma ya tiba mbadala maarufu kama kikombe cha Babu wa Loliondo.Pia ufuatiliaji huu ulilenga kuangalia ubora hasa usalama wa dawa yenyewe, madhara ya msongamano wa watu na magari, huduma za jamii na matukio mengine ya kibinadamu. Habari hii chanzo chake ni kituo cha haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment