Saturday, July 14, 2012

TUNDU LISSU AWADHIHAKI MAJAJI
MH. RAIS KIKWETE NA JAJI MKUU

Mh. Tundu Lissu ambae pia ni waziri kivuli wa sheria na Katiba, huenda akaburuzwa kwenyekwenye Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kwa kutoa maneno yenye mlengo wa dhihaka kwa  Waheshimiwa Majaji wanaoteuliwa  na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akichangia hatuba hio kama Msemaji wa kambi ya upinzani kwenye masuala ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Tundu Lissu alitamka maneno yenye mlengo wa dhihaka wa waheshimiwa hao wa Mahakama, ya kwamba baadhi yao hawana uwezo na pia kumkosoa Raisi kwa uteuzi wake huo wa watu wasio na uwezo.  

ALICHOKISEMA MWANASHERIA MKUU JUU YA KAULI ZA LISSU.


MWANASHERIA MKUU JAJI WEREMA

Mh. Werema alisema, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ana wajibu kuwaelekeza wanasheria hasa waliopo bungeni, kufuata misingi ya taaluma bila kuathiri haki yao wakiwa wabunge.“Nimefedheheka sana na mambo mawili yaliyotokea bungeni,” alianza kusema kwa sauti iliyosikika kuwa yenye huzuni, na kusema (mambo hayo) yamo kwenye hotuba ya Lissu.

Werema alisema baada ya Lissu kukosoa uteuzi wa majaji huku akisema wengine hawana uwezo, alizungumza naye ili kumuomba ayaondoe kwenye hotuba yake, lakini hakusema kama (Lissu) alikubali ama kukataa.Alisema maneno hayo ambayo yapo ukurasa wa tisa ibara ya pili ya hotuba hiyo, anaomba Lissu ayaondoe kabla ya kupitishwa bajeti ya wizara hiyo, vinginevyo kiti cha Spika kimuamuru (Lissu) aambatanishe vielelezo vinavyothibitisha maelezo yake.

Werema alisema Lissu ni mtaalamu wa sheria asiyetakiwa kufedhehesha mahakama na majaji, lakini pia alikiuka kanuni za Bunge kwa kuwataja watu wasiokuwa bungeni.Alitaja maeneo mengine yaliyomo kwenye hotuba ya Lissu na ambayo yanastahili kuondolewa ni yaliyohusu kushamiri kwa vitendo vya utekaji, utesaji na kudhuru watu, akitoa mfano wa Mbunge Kiwia, Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea, Waziri wa Uchukuzi na Dk Harrison Mwakyembe.

Werema alisema vitendo hivyo na vile vya umbakizaji kesi kwa raia wasiokuwa na hatia vilivyomo kwenye hotuba ya Lissu, havina ukweli bali vinapotosha.Wakati akimalizia kutoa hoja yake, Werema alisema Lissu anapaswa kutambua kwamba kuna Kamati ya Maadili ya Bunge na kwamba kuna uwezekano `akaburuzwa’ huko kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Wakati Werema akizungumza, Lissu alisimama kuomba mwongozo wa Spika, lakini Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, alimtaka akae ili Mwanasheria Mkuu amalize kuwasilisha hoja.Lakini Mwanasheria Mkuu alipomaliza kuzungumza, Mbunge Said Mkumba, alisimama kutumia ibara ya 68(7) ya kanuni za Bunge na kutaka muongozo wa Spika kwa kile alichosema, Lissu amevunja sehemu ya kiti anachokikalia bungeni.Baada ya Mkumba kuzungumza, Mhagama alimuita Lissu ambaye alisimama na kusema mwenye mamlaka ya kumjibu Mkumba ni kiti cha Spika, lakini Mhagama ‘alimgeuzia kibao’ na kumwambia amepoteza nafasi ya kutaka muongozo.

WAZIRI CHIKAWE ANENA
Waziri Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alielezea kusikitishwa na kauli ya Lissu, akisema amesikitishwa na jinsi lilivyosemwa hata kama palikuwa na hoja ya msingi.Alisema ibara ya 112 ya Katiba inaunda Tume ya Mahakama ambayo inamshauri Rais wakati wote na kwamba hakuna ukiukwaji wowote uliofanyika katika uteuzi wa majaji.

No comments: