Powered By Blogger

Monday, May 28, 2012

WENGI WAMLILIA WAKILI MAARUFU, BONIFACE STANSLAUS.


MKURUGENZI Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) 'Jembe' amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia kutokea kwa kifo hicho.  Marehemu Boniface ameacha pengo kubwa sana kwa wanaasheria hasa waliojikita katika kesi za jinai, kwa weredi wake mkubwa sana wa kudadavua, na kuendesha mashauri mbalimbali ya jinai. Yumkini, weredi wake huo ndio umepelekea mamia ya wanasheria na wadau mbalimbali kutoa maoni yao katika kurasa mbalimbali za kijamii” social networks” kuonesha maoni yao kama ifuatavyo:

MAONI YA WADAU:

Dr. Eliezer Feleshi , DPP alisema bado ofisi yake na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji huyo wa uendeshaji wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa. 


Moses Masinga, wakili msomi wa kujitegemea aliandika facebook , so sad tuliokuwa wote Law School nadhani mnamkumbuka jamaa alivyokuwa JEMBE! Aisee duniani tunapita tu. It is not easy kuamini lakini habari ni hivyo.
Kheri Mbiro, wakili msomi wa kujitegemea aliandika katika ukurasa wake wa facebook, RIP Boniface Stanslaus Makulilo,Sr. State Attorney..your passing away couldn't have been any earlier...quite a crippling blow to the Attorney General's Chambers...indeed many of us never ceased to pick a trick or two up your sleeves whenever you stood up in court...."An authority"..for many..its saddening but the Lord's wishes are unquestionable...we pray for your soul....amen.
Innocent Mhina mwanasheria na wakili wa bank ya posta aliandika;jamaa alikua exta ordinary attorney principles nyingi sana zimetoka kwenye cases alizo argue yeye na zingine kwa kuomba muongozo wa mahakama ususani kwenye ishu ya inquiry at subordinate crts at wht tme iwe conducted and how,.cheki kesi ya seleman abdalah v/s republic you will appreciate him and not only that alikua mwalimu mzuri sana
 
Jerry Muro ambae bwana Boniface aliwahi kuendesha kesi yake alisema, R.I.P boniface stanslaus,naibu mkurugenzi wa mashtaka alikuwa mwendesha mashtaka wa serikali kny kesi yangu,japo nilishinda kesi ila alitoa changamoto kny kesi yangu haswa.
WASIFU WAKE:

Boniface alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahaha ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.

Nyadhifa ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka 2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.Kati ya Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mwanza.Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri ilipofika Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma.


                                       KESI KUBWA ALIZOZIMAMIA;

Miongoni mwa kesi kubwa ambazo mwandishi wa habari hizi amekuwa akimshuhudia akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa nchini

  • sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka jana, iliwahukumu kwenda jela miaka mitano.
  • kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka jana.
  •  kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara Jayankumar Patel "Jeetu Patel' na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.
  • Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja. 

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Boniface mahali pema peponi.Amin.

No comments: