Powered By Blogger

Monday, May 28, 2012

MAAMUZI YA KESI YA LULU KUSIKILIZWA JUNI 16.


Lulu akiwa Mahakamani
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba Lulu akiwa mahakamani hapo.Lulu akiwasili Mahakamani hapo.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.

Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.

Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.

Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.

Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.Baada ya kusikiliza mabishano hayo
ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.

 
kwani Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 Pamoja na Sheria ya watoto ya mwaka 2009,  suala la umri lina mantiki kubwa sana ya kisheria, kwani mfumo wa kusikilizwa kwa kesi za watoto wenye makosa mbalimbali ya jinai” Children in conflicting with the Laws” pamoja na adhabu zao ni tofauti na ule wa kesi za watu wazima. Chanzo Michuzi Blog.

No comments: