Powered By Blogger

Sunday, July 8, 2012

JAJI MKUU AAPISHA MAWAKILI WAPYA


Mdau Fortuatus Mhalila baada ya kuwa wakili

JAJI Mkuu wa Tanzania Chande Othaman amewaapisha na kuwatunuku leseni za kufanya kazi mawakili wa kujitegemea 286 na kuwataka waende vijijini kuwasaidia Watanzania.Kuapishwa kwa mawakili hao wapya kunaongeza idadi ya mawakili kutoka elfu mbili mia tatu kumi na sita waliokuwepo na kufikia elfu mbili mia sita na mbili.
Jopo la Mawakili Wakiwa katika sherehe ya kuapishwa kwao

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuwatunikia mawakili hao Jaji Chande alisema ipo haja kwa mawakili hao kujikita kwenye maeneo ya pembezoni ambayo yana idadi kubwa ya watanzania wenye mahitaji mengi ya kisheria.

Mdau lilian Kowero akitabasamu baada ya kuapishwa kua wakili msomi

Aidha alitoa wito kwa waliojiandikisha kuwa mawakili lakini hawajasajiliwa wafike Baraza la Elimu ya Sheria liwasajili na hatimaye kuapishwa na kuwa mawakili kamili hali itakayosaidia kuongeza idadi ya mawakili nchini.


Nao baadhi ya mawakili walioapishwa Ijumaa hii walikiri kuwepo kwa changamoto ya upungufu huo wa mawakili kwenye maeneo ya vijijini na kubainisha kuwa ipo haja kujikita kwenye maeneo hayo.Kiapo hicho ni sehemu ya mpango mkakati wa kupunguza changamoto ya upungufu wa mawakili kutokana na kwamba idadi hiyo bado ni ndogo kulinganisha na mahitaji ya watanzania ambao ni zaidi ya milioni 41.

No comments: