Powered By Blogger

Monday, August 29, 2011

Jackson molestation evidence ruled irrelevant to Conrad Murray trial.

Dr. Conrad Murray
 
 Michael Jackson's sexual molestation trial is "no-go territory" for defense lawyers in the trial of Dr. Conrad Murray, a judge ruled Monday.Los Angeles County Superior Court Judge Michael Pastor, however, will allow testimony from two doctors about what the defense contends was Jackson's request for the surgical anesthetic propofol, a drug the coroner ruled played a major role in his death.

Defense lawyers appeared frustrated with the rejection of their witnesses, although they declined to speak to reporters about it as they left the downtown Los Angeles courthouse after Monday's hearing.Murray is charged with involuntary manslaughter in the June 25, 2009, death of Jackson, who would have turned 53 Monday.The defense wanted to have a Santa Barbara County, California, detective testify about drugs found at Jackson's Neverland estate during a search related to the sex charge.

"In particular, it is relevant to the defense that Michael Jackson possessed both propofol and Demerol in his residence as early as 2003," the defense said in a motion filed Monday.Los Angeles County Deputy District Attorney David Walgren argued testimony about drugs Jackson possessed in 2003 "has absolutely nothing to do with the standard of medical care" Murray gave Jackson the day he died on June 25, 2009.

Bringing up anything about the molestation trial, which ended with Jackson's acquittal, would be "character assassination on the victim," Walgren said.Defense lawyer Ed Chernoff, in a hearing Monday afternoon, assured the judge that he did not intend to question the detective about the sex charge, but only about drugs he found in his search.

Murray's defense lawyers want to argue that Jackson was addicted to the painkiller Demerol and was undergoing withdrawal from the drug when he died, Chernoff said. He said he expects the prosecution will say he "merely liked Demerol" and was not addicted.Jackson's "past drug addictions, use desires, possessions" is relevant, Chernoff said in court.Pastor ruled that the events were too far in the past for this trial and could mislead the jury."Anything having to do with the year 2003, any incident with Neverland, Santa Barbara, medical doctors, fundamentally is irrelevant," Pastor said. "It proves absolutely nothing with regard to the year 2009."

Pastor ruled that Beverly Hills dermatologist Dr. Arnold Klein could not be called to testify about giving Jackson Demerol shots. Testimony about Jackson's visits to Klein's office in the days before his death could lead the jury "down the path of prescribing to Dr. Klein some sort of criminal culpability in the death of Mr. Jackson."However, Klein's medical records can be used in the trial, he ruled.Two of Klein's office employees also cannot be called as witnesses, he ruled.

Prosecutors in the trial of Murray, Jackson's last doctor, had asked the judge to exclude or limit the testimony of 26 witnesses Murray's lawyers said they might call.Pastor has indicated he would keep the trial limited to what happened the last several days of Jackson's life. His decisions on the prosecution's request to limit witnesses indicate how tightly the judge will limit the defense arguments.

Other witnesses the judge said the defense could not call include John Branca, the lawyer who became executor of Jackson's estate after his death. Nothing about Jackson's finances can be considered, he said.The Los Angeles coroner has ruled that Jackson's death was caused by an overdose of the surgical anesthetic propofol, combined with other drugs.

Prosecutors have accused Murray of having a role in the overdose. Jury selection is scheduled to begin on September 8, with opening statements expected to be heard on September 27. Lawyers estimate the trial will conclude in early November.

If convicted on the involuntary manslaughter charge, Murray could face up to four years in prison.Source CNN.

Friday, August 19, 2011

Wakili maarufu asomewa mashtaka kitandani, anyimwa dhamana, asota magereza.

HATIMAYE wakili maarufu nchini, Mediam Mwale, anayekabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwamo uhujumu uchumi na kupatikana na fedha haramu zaidi ya Sh18 bilioni, amekabidhiwa idara ya magereza baada ya kunyimwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Habari zilizopatikana kutoka polisi na magereza mkoani hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, zinadai mtuhumiwa huyo alipelekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, nje kidogo ya Manispaa juzi baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.Baada ya kukamilisha taratibu hizo, Mwale alichukuliwa na kupelekwa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha lililopo Kisongo hadi kesi yake itakapotajwa Agosti 31, mwaka huu.

Wakili Mwale alisomewa mashtaka 13 akiwa wodini Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua akiwa mikononi mwa polisi, baada ya mahakama kukataa kupokea hati ya awali mashtaka iliyokuwa na makosa kisheria.

Mwale anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena Agosti 31, mwaka huu kesi yake itakapotajwa, anadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali na kufanikiwa kujipatia kiasi hicho kikubwa cha fedha, kinyume cha sheria kati ya Januari mwaka jana hadi Julai mwaka huu.

Hati ya mashtaka inataja kosa la kwanza hadi la tatu kuwa, ni kughushi na kuorodhesha majina na kampuni sita zilizotumiwa na mshtakiwa kuhamishia fedha hizo kwa nyakati tofauti kuwa, ni Oliva Green, Nyamao Mbeche Hollo, Gregg Motachwa, Ogembo Meetchel, John H.Adam na Mosoto O. Hoye.
 
Mashtaka ya uhujumu uchumi yanadaiwa kutendeka kuanzia Februari 16, mwaka jana, Wakili Mwale anadaiwa kuhamisha Sh1.9 bilioni kati ya Kampuni ya Ogambo Chacha na Gregg Motachwa Mwita.

Shtaka la nne anadaiwa kuwa Machi 5, mwaka jana, alihamisha dola 200,000 za Marekani wakati shtaka la tano lililotendeka Machi 30, mwaka huohuo alihamisha dola 159,500, huku katika shtaka la sita anadaiwa kuhamisha dola 5,500 Septemba 27, mwaja jana.

Shtaka la saba anadaiwa kuwa, Novemba 2, mwaka jana alihamisha zaidi ya dola 1.2 milioni, kabla kufanya hivyo tena Desemba 21, mwaka huohuo alipohamisha dola 416,000 na kumalizia mwaka kwa kuhamisha dola 521,000 Desemba 24, 2010.

Januari 17, mwaka huu alihamisha dola 808,000 na Februari 9, alihamisha dola 527,000 kabla ya kukamilisha zoezi hilo Julai 13, mwaka huu kwa kuhamisha zaidi  Sh300 milioni.

Katika hatua nyingine, mahakama imeamuru polisi kurejesha mali za mshtakiwa ikiwamo gari la kifahari aina ya BMW na simu ya kiganjani baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Charles Magesa, anayesikiliza shauri hilo kukubaliana na ombi la Wakili wa utetezi, Loomu Ojare kuwa hazijaorodheshwa kwenye hati ya mashtaka.



Friday, August 12, 2011

BP YAFUNGIWA KWA MIEZI 3 NA EWURA; MKURUGENZI WAKE MAHAKAMANI.

Kituo kimejawapo cha BP kikiwa hakiuzi Mafuta
Mamlaka ya udhibiti ya huduma za maji na nishati nchini( EWURA), leo imeifugia kampuni ya mafuta ya BP kifungo cha miezi mitatu kutojuhusisha na shughuli za kuuza mafuta. Hatua hiyo imetokea baada ya Kampuni hilo ya mafuta ambayo serikali ina ubia wa takribani asilimia hamsini kukaidi amri ya serikali iliyoitaka kampuni hio kuuza mafuta kwa wananchi. Taarifa iliyotolewa na ndugu Haruna Masebu ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa EWURA, kwamba hatua hio imefikiwa baada ya kampuni hiyo kuvunja kifungu cha 24(1) cha Sheria ya Petroli ya Mwaka 2008. Ambacho kinazungumzia" prohibition against activities contrary to principles of fair Competition".

Aidha, taarifa hio imesema baada ya kutangazwa kwa bei mpya ya mafuta Agosti 3 mwaka huu, Kampuni mbalimbali kama Oilcom,Camel,Engen na BP waligoma kuuza mafuta kwa wananchi wakipinga punguzo hilo la bei. Licha ya kampuni hizo kuagizwa na EWURA, ni BP pekee iliyokaidi amri hio mpaka leo, kinyume na Sheria ya petroli. 

Mkurugenzi huyo amesema hatua zilizochukulia ni kufungia kampuni hio kwa muda wa miezi mitatu, adhabu hio itaambatana na Mkurugenzi Mtendaji( Managind Director) wa kampuni hilo kufunguliwa Mashtaka kwa mujibu wa sheria, kupitia kwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai. Hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na na kampuni hizo tatu zilizogoma kisha kusitisha mgomo huo kupewa onyo kali kutokurudia kosa hilo.

Hatua hii ya EWURA, Imekuja siku chache baada ya uhaba mkubwa wa mafuta kukumba sehemu mbalimbali nchini hali iliyopelekea malalamiko kutoka kwa taasisi mbalimbali pamoja na wanasiasa Serikali ilikua inalaumiwa juu ya ukimya wake katika kutatua suala hilo.

Mtaalamu wa VVU Uingereza; Jela kwa kumfanya Mtanzania Mtumwa.

Mahakama ya southwark, iliyomhukumu Baira.
Mtaalam VVU amefungwa jela kwa ajili ya kuweka mwanamke 21 mwenye umri wa miaka kama mtumwa. Mwanasayansi Balira Rebecca, 45, alikutwa na hatia katika mahakama ya Southwark taji, kusini London, kwa ajili ya kumweka Methodia Mathias katika utumwa. Yeye alihukumiwa kifungo cha miezi sita na amri ya kulipa Mathias £3000 sawa na zaidiu ya shillingi millioni 6 za Kitanzania kama fidia.

Mathias, 21, alidai Balira alimleta kutoka Tanzania alikokua akiishi, aliieleza Mahakama hio kwamba  awali yeye Mathias alikua anakaa na nu zake Balira wa Dar es Salaam na malipo kwa ajili ya maombi ya viza ya Uingereza yake, ambayo alikubaliwa, ndugu hao ndio waliratibu usafiri wake wa ndege kwenda Uingereza. Lakini alidai kuwa alikuwa anafanywa kama mtumwa katika gorofa hukoThamesmead, kusini-mashariki ya London baada ya kuja Uingereza.

Alisema kuwa kuna wakati fulani Balira alipandwa na hasira ya mara moja na  kuchukua mkasi na kukata bra yake hivyo kujeruhiwa pilikapilika hizo.Balira alijitetea kwamba aliivuta tu bra ya mtanzania huyi hivyo kutatua baada ya kugundua kulikua na upotevu wa fedha katika sefu  yake  septemba mwaka  jana.

Mahakama ilielezwa kwamba rafiki wa Mathias,Beatrice Kosgei, alitafuta msaada kutoka taasisi ya Kalayaan upendo, ambayo inawakilisha wafanyakazi wahamiaji wa ndani.

Kate Roberts, kutoka Kalayaan, alisema: "wao wanafurahia pale haki inapotendeka  katika kesi za wafanyakazi wa ndani ... vilevile kesi kama hizo ndio huonesha matukio ya unyanyasaji yanayowakabili wafanyakazi wa ndani"

Mwendesha mashtaka alisema Caroline Haughey Balira "alifanya matendo yalifikia utumwa usiostahimilika." Hata hivyo Balira alisafishwa na mashitaka ya biashara ya mtu ndani ya Uingereza kwa ajili ya kutumiwa kitumwa  na ya unyanyasaji wa kawaida
. Chanzo gazeti la Guardian la uingereza.

Wednesday, August 10, 2011

Jaji Mkuu awaapisha mawakili 288 Leo.


Mdau Alain Maduhu akiwa na wife Wake Mh.Janeth Pamoja na Mama Mkwe wake Jaji Mgaya. 


Baadhi ya Mawakili wakifuatilia sherehe yao ya kuapishwa

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh.Othman Chande leo amewatunuku vyeti vya uwakili jumla ya wanasheria 288 katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam. Idadi hiyo ya mawakili hata hivyo bado haikidhi haja, kwani bado kuna tatizo kubwa la mawakili hasa katika mikoa mbalimbali na maeneo tofauti tofauti ya wilayani.

Sunday, August 7, 2011

Ajinyonga kwa kuchoshwa na vipigo vya Mkewe.

MKAZI mmoja katika Mtaa wa NHC katika Mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti wilayani Mara, Samson Kitoshi (32) amejinyonga hadi kufariki dunia kwa kamba chumbani kwake kwa kile alichodai kuwa: “Amechoka kupigwa na mkewe kila wakati.”

Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu, linadaiwa kutokea jana saa tano asubuhi. Akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu (Jina tunalihifadhi) alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo, mama yao alimpa Sh 1,000 akanunue sukari na vitafunio, lakini asimpe baba yao chai... "Mama aliaga kuwa anakwenda Hospitali DDH kwa kuwa anaumwa. Baba akasema hatakunywa chai hiyo na kutuambia kuwa hatutamwona tena anatuaga na tusiingie ndani."

Marehemu baada ya kuingia chumbani kwake anadaiwa kuwa alifunga kamba juu ya dari na kujining'iniza hadi alipokata roho.Mtoto huyo wa darasa la tatu ambaye ana umri wa miaka 10 alisema hawakuweza kuingia ndani kama walivyoambiwa na baba yao, lakini baadaye aliamua  kumwamsha akidhani kuwa amelala ili anywe chai ndipo alipokuta amening'inia. Alipiga kelele kuomba msaada.

"Baba alikuwa amevua shati akawa amening'inia chini kuna meza nikaweka stuli ili nifungue kamba sikuweza nikapiga yowe majirani wakafika wakasema ameshakufa," alisema.

Kuhusu migogoro ya ndani, mtoto huyo alisema kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara hasa ukisababishwa na mama yao ambaye anauza pombe ya kienyeji ya wanzuki anaporudi akiwa amelewa kwani humfanyia vurugu baba yao.

"Hivi karibuni baba alifikia hatua ya kumtaka mama aondoke amechoka na mateso anayomfanyia, lakini mama alikataa kuwa hawezi kutoka na kudai yeye ndiye atakayetoka," alisema.Ndugu wa Kitoshi ambaye anaishi katika Kijiji cha Morotonga alisema kuwa marehemu aliyekuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka alikuwa akilalamika kupigwa na mkewe mara kwa mara.

"Huyu ni ndugu yangu hata leo amefika kwangu na akanikosa na kurudi nadhani alitaka kuniambia kitu. Baada ya muda nikapigiwa simu kuwa amekufa kwa kujinyonga, amechoshwa na kupigwa," alisema.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti, Paulo Mng'ong'o alijaribu kumtafuta mwanamke huyo kwa simu lakini mara baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni OCD, mama huyo alikata simu.

Baada ya muda mama huyo alifika nyumbani na kumkuta mume wake akining'inia kwenye kamba. Huko alipokewa kwa maneno makali kutoka kwa wanawake wenzake waliokuwa na hasira baadhi wakisema: “Ulitaka afe ujitawale sasa amekufa tanua... unadanganya ulikuwa hospitali mbona umelewa..."

Maneno hayo makali yalimwingia mwanamke huyo kwani alikaa chini kisha akalala chali na kupoteza fahamu. Hakuweza kunyanyuka hadi alipopakiwa kwenye gari la polisi pamoja na mwili wa mumewe na kupelekwa hospitali.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Mng'ong'o alisema polisi inalifanyia uchunguzi na kwamba itatoa taarifa kwa umma. Alisema wangefanya mahojiano na mke huyo wa marehemu baada ya kuzinduka kujua chanzo cha kifo hicho.Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC, Elias Nyamraba alisema kuwa wanasubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya hatua nyingine ikiwemo ya mipango ya mazishi akisema Kitoshi ni mzaliwa wa Kijiji cha Issenye.

Wakili maarufu nchini akamatwa; akutwa na milioni 20 za matumizi"madogo madogo".

WAKILI maarufu jijini Arusha, anadaiwa kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye akiba yake binafsi, zinazodaiwa kuingia kwa njia isiyo halali.Wakili huyo aliyejijengea umaarufu nchini kutokana na uendeshaji kesi zake, anadaiwa kukamatwa Agosti 2, mwaka huu wakati akiendesha gari lake la kifahari aina ya Escalade, Polisi wa Kimataifa Interpol walishikilia kabla ya kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi.

Taarifa zilipatikana zinadai ya kuwa, kushikiliwa kwa wakili huyo kunafuatia polisi nchini kufuatilia nyendo zake kwa kipindi kirefu kuhusiana na shughuli zake, huku wakihofia kiasi kikubwa cha fedha kilichokutwa kwenye akaunti yake binafsi kwenye benki moja nchini.Pia, taarifa hizo zinadai wakili huyo alikamatwa majira ya usiku na kwamba, kabla ya Interpol kumfikisha Kituo Kikuu cha Polisi walifanya upekuzi kwenye nyumba yake iliyopo mkoani Arusha.

Vyanzo vya habari vinadai kuwa, baada ya polisi hao kufanya upekuzi wa kina sehemu hizo mbili walimfikisha Kituo Kikuu cha Polisi ili kuruhusu hatua nyingine kufuata.Taarifa zinadai kuwa, wakati anakamatwa ndani ya gari alikutwa na zaidi ya Sh20 milioni na kwamba, baada ya kumhoji juu ya kiasi hicho cha fedha, inadaiwa aliwajibu hizo zilikuwa kwa ajili ya matumizi yake madogo.

“Walimkamata akiwa anaendesha gari lake hapa mjini, lakini ndani ya gari walikuta Sh20 milioni, walipomuuliza aliwajibu kuwa hizo ni kwa ajili ya matumizi yake madogo madogo,” kilisema chanzo cha habari. Inadaiwa chanzo cha polisi kufuatilia nyendo zake, inatokana na akiba ya wakili huyo kukutwa na kiasi cha zaidi ya Sh30 bilioni zinazodaiwa kuingizwa njia zisizo halali.

Pia, inadaiwa polisi walikuwa na mashaka na gari analotumia kuingizwa nchini kinyemela.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, hakukiri wala kukataa zaidi ya alisema suala hilo liko ngazi za juu, hawezi kuzungumzia.

“Kwa kweli hilo suala liko juu ya ngazi yangu, siwezi kulizungumzia chochote kwa sasa hadi nipate idhini kutoka kwa wakubwa wangu,” alisema Andengenye.

Andengenye alisema anasubiri taarifa kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam na akipata kibali atalitolea ufafanuzi.Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tawi la Arusha, Duncan Ooola, alikiri kukamatwa kwa wakili huyo na kwamba, walipofuatilia waliambiwa anachunguzwa na polisi.

“Ni kweli wamemkamata (jina tunalo) Jumanne, lakini sijui saa ngapi, tulikwenda polisi kujua chanzo walitwambia anachunguzwa, hiyo ndiyo taarifa ninayoweza kukupa,” alisema Ooola.Chanzo gazeti la mwananchi.

Thursday, August 4, 2011

Tendwa ampinga Werema

Mwanasheria Mkuu wa Serikali

VYAMA vya siasa nchini vitaendelea kufanya maandamano ya amani pale inapobidi kwa kuwa hatua hiyo inaruhusiwa kisheria na ni haki ya msingi ya kila mtu na chama chake katika kujitafutia haki. Aidha, imeelezwa kuwa mpango wa kutunga sheria itakayodhibiti maandamano ya vyama vya siasa nchini unaodaiwa kutajwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) , Jaji Frederick Werema, ni kutaka kuvinyima vyama haki za msingi za kikatiba.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Msajili wa Vyama, John Tendwa, alipozungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi katika jimbo la Igunga na marejesho ya fomu za gharama za uchaguzi mkuu uliopita. “Labda kama AG hakueleweka au alitafsiriwa vibaya, sidhani kama anaweza akasema ataleta muswada wa sheria ya kudhibiti vyama vya siasa kufanya maandamano nchini, kwa kuwa hiyo ni haki ya kikatiba na yeye ni mwanasheria anayeifahamu Katiba, sijui, sikumsikia ninyi ndio mnanieleza katika swali lenu hapa.

“Lakini kama hivyo ndivyo, basi itabidi abadilishe sheria nyingi sana, kwa sababu zipo kihalali na kwa malengo ya kujenga, endapo maandamano yanakuwa na nia nyingine hapo inawezekana kukawa na kasoro, lakini kuyadhibiti bila sababu kwa kuwa ni ya vyama vya siasa sidhani kama itakuwa sawa, ngoja tuone. Itakapotokea ndipo hapo tutajua,” Msajili alisema.

Akichangia hivi karibuni hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyotolewa bungeni na Shamsi Vuai Nahodha Werema alisema suala la maandamano ni haki ya kikatiba, lakini pia moja ya masharti ya chama cha siasa kinapoandikishwa, ni kuhakikisha hakitumii njia ya mapambano katika kufikia malengo.

Alisema ingawa maandamano yanaruhusiwa, lakini wakati mwingine yanatumika vibaya na kutolea mfano wa mbunge kuzungumzia kuandamana kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam na kwamba zipo baadhi ya nchi maandamano ingawa yanaruhusiwa, lakini yana utaratibu ili kutohusisha watu ambao wako kazini.

Alisema kutokana na hali hiyo, kuna haja ya kufanya marekebisho ya suala la maandamano ili yasifanyike sehemu za kazi na kuvuruga taratibu za wengine. Akizungumzia vyama vya siasa vilivyofanya marejesho ya gharama za uchaguzi, Tendwa alisema ni 12 huku NCCR-Mageuzi na UDP vikiwa vimeomba nyongeza ya wiki mbili kufanya hivyo.

“Wasipotekeleza hawa sheria itachukua mkondo wake kwa kuwafikisha mahakamani na kuwatoza faini ya Sh milioni tatu huku tukiwazuia kushiriki uchaguzi unaokuja”.

Wakati huo huo, Baraza la Vyama vya Siasa Nchini litakaa mwezi ujao kujadili namna ya kurejesha heshima na imani ya wananchi kwa vyama vyenye wabunge bungeni iliyopotea, baada ya wawakilishi hao kushindwa kutii kanuni na maadili ya uwakilishi wao ndani ya chombo hicho hasa katika Bunge la Bajeti linaloendelea sasa.

Akijibu maswali ya wanahabari kuhusu tabia mbaya za baadhi ya wabunge za kutotii kanuni za Bunge wawapo vikaoni na kutoleana maneno yasiyo na mantiki bila kutii Kiti cha Spika Tendwa alisema yeye kama Msajili wa Vyama hapaswi kuwazungumzia watu hao wanapokuwa bungeni kwa kuwa wana kiongozi wao.

“Sheria inanikataza kuwazungumzia, kuwaonya na kuwanyooshea kidole kwa jambo lolote wanapokuwa ndani ya Bunge kwa sababu wana Spika na Kamati ya Maadili vyenye jukumu la kuwaonya au kuwaondoa pindi wanapoonekana kushindikana kitabia. “Hivyo wananchi wasinitupie lawama bure kwa kuwa ni wangu wanapokuwa nje ya jengo lile la Bunge tena kupitia kwa vyama vyao. Sana sana tulichopanga kufanya ili kunusuru heshima ya Bunge na vyama vya siasa wanavyoviwakilisha ni kukutana na Baraza la Vyama vyote vya Siasa nchini na kujiwekea msimamo wa namna ya kurekebisha tabia hizo,” Msajili wa Vyama alisema.

Aliwahakikishia wananchi kuwa Bunge la Oktoba litakuwa na tofauti kubwa, kwa kuwa wao wapo kushirikiana na Spika Anne Makinda na Kamati ya Maadili ya Bunge kuhakikisha wabunge hawawi na uwakilishi usiohitajika.

“Mimi ni mlezi wa vyama ambavyo wabunge wametoka, hivyo ni lazima tunapoona kuwa tuliyowafundisha watoto wetu hawayafuati, tuangalie namna ya kuwafanya wayatii ili aibu ya malezi yasiyo bora isitupate.

“Lakini kama wataendelea kuwa na tabia hizo hizo za kuwawakilisha wananchi kwa staili ya mizozo, kukashifiana, kutishiana, kutoleana hasira na lugha chafu na tabia nyingine mbaya, viongozi wanaowajibika nao moja kwa moja watapaswa kuwachukulia hatua kwa sababu muda wa kujifunza kanuni na nidhamu umekwisha” Tendwa alisema akiwa mwanadamu wa kawaida anaumizwa na uwakilishi huo wa sasa wenye asilimia 70 ya vijana waliotazamiwa kuleta mageuzi bora.

“Sasa unafika wakati hata mtoto mdogo anayesikia mambo ya wabunge wetu anawabeza, heshima hakuna na linakuwa Bunge lenye bora wabunge na si wabunge bora. Umuhimu wa vijana wengi bungeni unapoteza maana, kwa kuwa la zamani lenye wazee wengi ndilo lilikuwa na busara kuliko hili lenye mabadiliko haya,” alisema.Chanzo gazeti la habari leo.