Powered By Blogger

Friday, August 12, 2011

BP YAFUNGIWA KWA MIEZI 3 NA EWURA; MKURUGENZI WAKE MAHAKAMANI.

Kituo kimejawapo cha BP kikiwa hakiuzi Mafuta
Mamlaka ya udhibiti ya huduma za maji na nishati nchini( EWURA), leo imeifugia kampuni ya mafuta ya BP kifungo cha miezi mitatu kutojuhusisha na shughuli za kuuza mafuta. Hatua hiyo imetokea baada ya Kampuni hilo ya mafuta ambayo serikali ina ubia wa takribani asilimia hamsini kukaidi amri ya serikali iliyoitaka kampuni hio kuuza mafuta kwa wananchi. Taarifa iliyotolewa na ndugu Haruna Masebu ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa EWURA, kwamba hatua hio imefikiwa baada ya kampuni hiyo kuvunja kifungu cha 24(1) cha Sheria ya Petroli ya Mwaka 2008. Ambacho kinazungumzia" prohibition against activities contrary to principles of fair Competition".

Aidha, taarifa hio imesema baada ya kutangazwa kwa bei mpya ya mafuta Agosti 3 mwaka huu, Kampuni mbalimbali kama Oilcom,Camel,Engen na BP waligoma kuuza mafuta kwa wananchi wakipinga punguzo hilo la bei. Licha ya kampuni hizo kuagizwa na EWURA, ni BP pekee iliyokaidi amri hio mpaka leo, kinyume na Sheria ya petroli. 

Mkurugenzi huyo amesema hatua zilizochukulia ni kufungia kampuni hio kwa muda wa miezi mitatu, adhabu hio itaambatana na Mkurugenzi Mtendaji( Managind Director) wa kampuni hilo kufunguliwa Mashtaka kwa mujibu wa sheria, kupitia kwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai. Hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na na kampuni hizo tatu zilizogoma kisha kusitisha mgomo huo kupewa onyo kali kutokurudia kosa hilo.

Hatua hii ya EWURA, Imekuja siku chache baada ya uhaba mkubwa wa mafuta kukumba sehemu mbalimbali nchini hali iliyopelekea malalamiko kutoka kwa taasisi mbalimbali pamoja na wanasiasa Serikali ilikua inalaumiwa juu ya ukimya wake katika kutatua suala hilo.

No comments: