MHASIBU wa Kampuni ya Tasu, Machafu Chokoma (59) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili, likiwemo la kughushi sahihi na kujipatia Sh milioni 1.8 kwa njia ya udanganyifu. Chokoma alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita na kusomewa mashitaka na Hakimu Wilberforce Luhwago wa mahakama hiyo.
Wakili wa Serikali Sakina Sinda, alidai mshitakiwa alighushi saini ya Kaimu Mhasibu wa kampuni hiyo, George Kambute, kwenye hundi No.504642. Kwa mujibu wa madai hayo, hundi hiyo iliyoghushiwa ilionesha kuwa Kimbute amesaini ili atoe fedha hizo kutoka akaunti yenye namba 015007803600 jambo si la kweli.
Sinda aliendelea kudai kuwa, Oktoba 22 mwaka jana katika Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, Dar es Salaam, Chokoma alijipatia Sh milioni 1.8 kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti hiyo kwa kutumia hundi ya kughushi iliyoonesha imesainiwa siku hiyo hiyo. Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Luhwago aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 23 mwaka huu itakapotajwa tena. Hata hivyo Mshitakiwa aliiachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Habari hii chanzo chake ni Habari leo.

No comments:
Post a Comment