![]() |
Baba Askofu Valentino Mokiwa |
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, chini ya Jaji Kakusulo Sambo imeamuru kukamatwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk. Valentino Mokiwana Stanley Hotay kwa kukiuka amri ya Mahakama na kumsimika Askofu, StanleyHotay. Amri hiyo imetolewa ikiwa ni siku mbili tangu kusimikwa kwa askofu huyo, ambapo Ijumaa iliyopita mahakama hiyo ilisitishwa kusimikwa kwa Askofu Hotay kutokanana kesi iliyofunguliwa dhidi yake na waumini wa kanisa hilo, ambapo Askofu Hotay aliingia katika mgogoro wa kikatiba kutokana na umri wake.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa sherehe za kumsimika askofu huyo zilifanyika Makao Makuu ya Dayosisi hiyo ya Mount Kilimanjaro na kuongozwa na Askofu Mokiwa, ambapo alieleza kuwa sherehe zilizofanyika ni za kumsimika Askofu wa Kanisa la Anglikana na si Askofu wa kanisa hilo Dayosisi hiyo, na kwamba kusimikwa rasmi kungelifanywa baada ya mashauri yaliyoko mahakamani kumalizika. Katika kesi hizo moja ya madai namba 18/2011 na Jinai namba 48/2011 zilifunguliwa dhidi ya Wadhamini wa Kanisa hilo na Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo, Hotay na Bw. Lothi Oilevo, Bw. Godfrey Mhone na Bw. Frank Jackob pamoja na mambo mengine waliiomba Mahakama kuzuia kusimikwa kwa askofu huyo kwa madai ya kuchakachua umri.
Akinukuuvifungu mbalimbali vya sheria, Jaji Sambo alisema Askofu Mokiwa na Hotay walichokifanya kwa yeyote ni ukiukaji wa amri ya mahakama “Nimeridhika kuwa amri halali ya mahakama imekiukwa na ieleweke bayaha kuwa nchi hii inatawaliwa na Utawala wa Sheria na hilo limekuwa likisisitizwa mara kwa mara na rais wetu Mh.Jakaya kikwetwe na Viongozi wengine wa Juu alisema Jaji huyo.
Aliieleza mahakama kuwa ma-askofu hao wamefanya kitendo muhimu kilichosababisha amri ya mahakama isiheshimiwe jambo ambalo ni hatari kwa utawala wa sheria; “kama anasema utanifanya na kuingilia hata kukiuka amri ya Mahakama Kuu sembuse, mahakama zingine za chini itakuweje!..hivyo mahakama ni wajibu wake kutumia vifungu kadha wa kadha kama kifungu cha 114 (i) C na K na (iii) pamoja na kifungu namba 124 vinavyoipa mahakama hii kuwaadhibu wale watakaokiuka amri ya mahakama…huwezi kuacha mahakama inachezewa na vifungu vyote hivyo vipo…sasa naamuru…ni amri ya dola kuwa Askofu Dk. Mokiwa na Hotaywakamatwe mara moja”.
Awali Jaji huyo alisema walalamikaji waliwasilisha mahsuri hayomahakamani kuomba itolewa amri ya kuzuia sherehe hizo kimya kimya lakini kwa busara na mahakama hiyo ikaamua kuuita upande mwingine ambao nao ulitoa pingamizi la awali lililotaka ombi hilo liondolewa na sherehe za kumsimika Askofu huyo zifanyike lakini baada ya mahakama kuona muda wa kutoa maamuzi ni mfupi iliamuru sherehe hizo kusimama hadi uamuzi wa mahakama utakapotolewa jana (Jumatatu).
Alidai kuwa pamoja na jitihada zote hizo za kutumia busara wao waliendelea na kumsimika mchungaji huyo kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, wakati mahakama iliona si busara kuendelea na zoezi hili wakati wapo watu wengine wakipiga kelele juu ya hilo, lakini kabla mahakama hiyo haijatoa maamuzi, wao wamemwapisha, na sasa ni kuwa mwenendo mzima wa shauri hilo hauna maana yoyote kwani ni kweli kabisa kuwa ni ngumu kumtoa Uaskofu maana yake ni kwamba mwenendo mzima wa mashauri hayo umevamiwa.
Jaji huyo alisema wadai katika madai yao walieleza kuwa Katiba ya Kanisa hilo inaelekeza kuwa mgombea kiti hicho anayeweza kukalia kiti hicho lazima awe na miaka kati ya 40 na 60 ndipo anapoweza kukabidhiwa dhamana ya kuwa kiongozi wa ngazi hiyo, ambapo Askofu huyo alidaiwa kuwa mwaka jana alikuwa anayo miaka 38 tu. Awali, wakili wa Upande wa Madai Meinrad D’souza aliileza mahakama hiyo kuwa amri iliotolewa na Mahakamam hiyo haikutekelezwa hivyo sherehe za kumsimika Uaskofu Hotay zilishafanyika Jumapili iliyopita jambo ambalo ni kukiuka amri halali ya mahakama, hivyo kwa ukiukaji huo aliiomba mahakama hiyo kwa vya sheria vilivyopo kuwakamata wahusika wakuu wa tukio hilo ambao ni Askofu Mokiwa na Hatay.
“Mheshimiwa Jaji kabla ya kuendelea na lolote kuna jambo muhimu limetokea kutokana na amri ya mahakama yako iliyotolewa Ijumaa iliyopita, amri hiyo imekiukwa na sherehe za kumsimika Askofu Stanley Hotay zimefanyika Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro, upo ushahidi wa kutosha juu ya hilo na kwamba kwa mujibu wa katiba ya Kanisa Askofu kupatikana kwa kuchaguliwa kutoka katika Dayosisi husika, labda hiyo ni utaratibu mpya wa kuwapata maaskofu”aliongeza D’souza. Akijibu hoja hizo, Wakili Tadayo alisema kilichofanyika ni kumsimika Uaskofu wa Kanisa hilo Tanzania na si Askofu wa Dayosisi hiyo na kwamba kitendo cha kumsimika uaskofu hakina maana kuwa ndiyo Askofu wa Dayosisi hiyo, kitendo hicho na cha awali na iwapo shauri litaisha mahakamani atasimikwa rasmi kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, hivyo aliomba Mahakama hiyo kuendelea kusoma maamuzi wa mahakama juu ya maombi ya walalamikaji.
No comments:
Post a Comment