![]() |
Jaji Mkuu Mteule wa kenya |
Jaji Mkuu mteule wa kenya Dk. Willy Mutunga mwenye umri wa miaka 65, anakabiliwa na tuhuma mbalimbali moja ikiwapo ya kuvaa hereni katika mojawapo la sikio lake. Dk Mutumga alizidi kubainisha ya kwamba ni kama akiambiwa kuivua hereni yake hiyo ili awe Jaji mkuu, ni bora akaendelea na kuivaa hereni na kungatuka kwenye kiti hicho.
“I wear my ear ring not because of my sexuality but spirituality. There is no way I can remove this ear ring even if I become the Chief Justice. If am told I must remove it to get the job of Chief Justice I will say keep your job,” Dr Mutunga said.
Dk Mutunga amewahi kuwa mhadhili katika shule ya sheria kenya(law school), mwenyekiti wa zamani wa Jamii ya Sheria wa Kenya (kenya law society) na mtu mashuhuri katika mapambano ya kisiasa ya nchi ya kenya ambapo kwaka 1982 alipata mateso ya kunyimwa dhamana na mahakama kufuatia kukamatwa yake juu ya milki ya nyaraka mbalimbali za uchochezi Julai 10, 1982, wakati yeye alikuwa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Msomi huyo aliyepata shahada yake ya uzamili katika chuo kikuu cha Dar es salaam pia Jaji mkuu mteule nchini Kenya Dk Willy Mutuga amekanusha kama anashiriki mapenzi ya jinsia moja.Mutunga aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na kamati maalum ya bunge.Kamati hiyo ya bunge ilifanya vikao vyake vya siku mbili kusikia shutuma zilizotolewa dhidi ya walioteuliwa kuchukua nyadhifa za jaji mkuu,naibu jaji mkuu na mwendesha mashtaka mkuu
Anashiriki
Hatua hii ilichukuliwa baada ya baadhi ya watu na hasa makanisa yakidai walioteuliwa si watu wanaozingatia maadili ya kifamilia kukiwemo na shutuma kuvaa hereni kwenye sikio la kushoto kwa Dk Mutunga ni ishara kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja."Sishiriki mapenzi na wanaume,ila siwezi kuwabagua wanaume au wanawake wanaoshiriki mapenzi hayo,mimi mwenyewe mpwa wangu ni wa jamii hio",alisema Dk Mutunga.
Mchakato
Naibu jaji mkuu mteule Nancy Baraza pia alikuwa na muda wake wa kujitetea,alipoulizwa kwa nini alikita utafiti wake wa shahada ya uzamifu katika suala la haki za wapenzi wa jinsia moja. Baraza alisema anafanya hivyo kwa kuwa alitaka kuwa mbunifu na kufanya utafiti wa kipekee ambao haujawahi kufanywa nchini Kenya.
Baada ya vikao hivyo kwa umma ambavyo vimetumika kuwatathmini tena wateule,majina hayo yatawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura,ikiwa wataidhinishwa basi watachukuwa nyadhifa na iwapo watakataliwa bai mchakato wa usaili utaanza upya
No comments:
Post a Comment