![]() |
Christopher Tisley |
Jamaa hapo pichani ameshitakiwa kwa jaribio la wizi kwa kutumiwa silaha, Baada ya kumtishia bastola karani wa duka moja huko Marekani, ili ampe senti 99 za dola ya kimarekani alizokua nazo sawa na shilingi 1500 za kitanzania.
Kulingana na taarifa iliyotolewa Mahakama hapo, Christopher Tisley, 34, alitembelea maeneo ya Magharibi mwa Lawrence Avenue huko Marekani na kumdai karani huyo fedha, karani huyo alipokataa mtuhumiwa huyo alitoa bunduki na kuanza kumtisha nayo.
Tisley,ambae ni mkazi wa Morgan Street, aliamuatoka nje ya duka hilo baada ya mteja kuingia katika duka hilo, hivyo kumpa mwanya karani huyo kufunga mlango kwa ndani. Japo mlango ulifungwa jamaa huyo aliendelea kugonga malango na madirisha akilazimisha apatiwe pesa.
Polisi walipofahamishwa walikuja na kukamata Tisley, japo silaha kwa wakati huo hakua na silaha inayodaiwa alitumia kutishia. Waendesha mashitaka wanasema jamaa huyo alipatikana na gramu 3 ya methamphetamine(unga wenye kemikali) katika milki yake.
Jaji wa mahakama anayostakiwa jamaa huyo alisema dhamana ya njemba huyo ni Dola 50,0000 sawa na zaidi ya shillingi Millioni 65,000,000/= za kitanzania. Tishley anashitakiwa kwa jaribio la kujipatia mali kwa nguvu na milki ya mali isiyoruhusiwa.
No comments:
Post a Comment