![]() |
Mh.Mille Othiambo |
Mbunge pichani hapo juu, jana jioni katika kikao cha kupitisha majina ya wateuliwa wa nafasi za juu za Mahakama nchini kenya aliibua mtafaruku mzito baada ya kudai asilimia 15% ya wahesimiwa wabunge wa Jumba hilo ni Mashoga. Madai hayo yalichafua hali ya hewa la Bunge hilo, na yalipingwa kupingwa vikali kutoka kwa wabunge wenzake. Hali hiyo ilimlazimu Naibu Spika wa bunge hilo Farah Maalim kumuomba Bi Odhiambo kuondoa au kufuta matamshi yake pamoja na kuomba msamaha.
Bi. Othiambo alitamka maneno hayo wakati wa majadiliano bungeni humo, kuhusiana na kupitishwa au kutokupitishwa kwa majina matatu yaliyopendekezwa kwa ajili, ya Jaji Mkuu wa kenya, Naibu wake pamoja na Mkurugenzi wa makosa ya jinai.
Bi Odhiambo alikataa kuomba radhi wala kufuta usemi wake kwani alisema madai anayoyasema yametokana na utafiti uliandikwa katika ripoti ya mwanaharakati Betty Murungi wakati mwanaharakati huyo alipohojiwa mbele ya Kamati ya Utekelezaji na Usimamizi wa katika,wakati wa zoezila uteuzi wa wagombea mbalimbali wa nafasi hizo za juu katika Mahakama. Mbunge huyo alinukuliwa akisema: "I am merely reporting what was said to us before the committee. Mr Speaker if you want to get me out because of that I am happy; I will leave,".
Kutokana na Mbunge huyo kukataa kukanusha usemi wake, Naibu spika akisoma Kanuni na 197 na 198 ya Bunge hilo, alimsimamisha Bi.Othiambo asihudhulie vikao viwili vya Bunge."Kwa mujibu wa masharti katika Kanuni ambazo nimezitaja ninamsimamisha Mheshimiwa Millie Odhiambo asihudhulie Bunge kwa siku mbili," alisema.Cha kustaajabisha kabla naibu spika, hajamaliza kutoa hukumu yake Mbunge huyo aliamua kutoka nje ya kikao vya Bunge.
Hata hivyo wabunge walionekana kutokuridhika na hawakua na furaha na adhabu hiyo didhi ya Bi Odhiambo Ndipo Mh.Mbunge Bifwoli Wakoli kusema ahabu hio ni ndogo, ingefaa Mh.Othiambo asimamishwe kwa muda wa mwaka mmoja kutoingia Bungeni.
Naibu Spika vilevile alikubaliana na Mbunge Mwingine,Asman Kamama aliyeomba hotuba ya Bi Odhiambo ni kuondolewa kutoka Hansard ambapo taarifa zote rasmi hurekodiwa.
Kikao hicho cha kupitisha majina ya wagombea, kilimamlizika mida ya usiku kwa wabunge kupitisha majina ya walioteuliwa kuwa Jaji Mkuu,Makamu wake na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai wa Kenya.
Kikao hicho cha kupitisha majina ya wagombea, kilimamlizika mida ya usiku kwa wabunge kupitisha majina ya walioteuliwa kuwa Jaji Mkuu,Makamu wake na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai wa Kenya.
No comments:
Post a Comment