Powered By Blogger

Wednesday, May 25, 2011

Wastaafu Afrika ya Mashariki: Washindwa Kesi.





Baadhi ya wastaafu wa Afrika ya Mashariki
WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jana walizua tafrani katika viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania, kufuatia kitendo chao cha kufunga Barabara ya Kivukoni kwa zaidi ya saa nne.Tafrani hiyo ilisababisha kufungwa kwa lango kuu la kuingilia katika jengo la mahakama kuu, baada ya wastaafu hao kutaka kuingia ndani ya jengo hilo hukuwa wakiwa wamejawa na jazba.

 wastaafu hao walizua tafrani hio kutokana na kesi yao  ya madai ya Shilingi 2 Trilioni dhidi ya serikali kutupiliwa mbali na mahakama kuu.Hukumu iyo iliyosomwa kwa lugha ya kiingereza na kuchukua muda wa saa zima, ilitupilia mbali madai ya walalamikaji hao na kupelekea tafrani hio baada ya wafanyakazi kutokuridhika Chombo hicho cha kutoa haki.

Jitihada za Charles Semgalawe  wakili anayewatetea ndugu, jamaa na baadhi ya wasataafu wa jumuiya hio kuwaomba kuondoka katika maeneo ya mahakama ziligonga mwamba kwani  baada ya kuwaambia suala la kuondoka baadhi ya wastaafu walianza kufunga barabara ya kivukoni kwa kuweka mawe yaliyokua karibu na mahakama na wengine waliamua kulala barabarani. Hata hivyo Tafrani hio ilizimwa na polisi mnamo mida ya saa tisa alasiri baada ya kuondoa vizuizi vya mawe vilivyowekwa na awastaafu hao, na kutoa nafasi ya magari mengine kupita.

Kwa mujibu  wa Mwenendo wa sheria za madai, wastaafu hao bado wana nafasi ya kupinga hukumu hiyo katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania.






No comments: