Powered By Blogger

Sunday, May 22, 2011

Msaada Kizimbani!


 Mwanasheria, mimi ni kijana mwenye msakani yangu katika jiji moja maarufu kwa kua na mawe mengi. Kiufupi najishughulisha na deal za hapa mjini. Katika pilika pilika zangu za kufanya shughuli zangu za kila siku, nilikutana na mzee mmoja ambae anauza Plot yake kubwa kwa shillingi Millioni Mia Moja, Hivyo mimi na jamaa wenzangu tukapewa kazi ya kutafuta mteja wa hilo Eneo. Kwa bahati nzuri tulipata mtanzania mmoja mwenye asili ya kiasia na katika kubagain bei akasema atatoa 150/= M kwa hilo eneo. Sasa sijui cha kufanya maana hio nyongeza ya millioni 50 tumeizidisha sisi, pasipo kukubaliana na mwenye eneo. Hofu yetu ni kwamba Mhindi anataka kuonana na mwenye eneo ili kulipa hio 150 M. Tuna hofu mwenye eneo anaweza kutuzunguka akachukua pesa yote au akatupa kiduchu.Je tufanya nini ili sheria itulinde? Nipostie wadau wanishauri. Mdau Dennis.

2 comments:

Lukiko said...

Kuna visa vingi vya namna hii vinatokea kila siku katika jamii zetu, mlichofanya nyie ni "udalali" ambao kwa bahati mbaya sheria haiwalindi, cha muhimu ni kuongea vizuri na muuzaji na kukubaliana ya kwamba nyie mtatafuta mteja wa bei anayotaka na ikitokea mmepata mteja atakayetoa zaidi ya hiyo bei basi "cha juu" ni mali yenu, ni vizuri kama makubaliano hayo mkiyafanya kwa njia ya maandishi ili walau muwe na ushahidi wa hoja zenu ikitokea anataka kuwageuka.

Anonymous said...

Swala la Pesa ni kiasi kilichowekwa hadhalani ni kikubwa.Unapozungumzia umepata mjeta M150 wakati muuzaji alisema M100. Mtu yoyote yule lazima abadilike tu. Tofauti hiyo ni kubwa Kaka. Inshu kama hizo lazima wewe dadali umtoe ( Umalizane kabisa)na muuzaji ili wewe uje ukutane na mteja, wewe ukiwa muuzaji si kama dalali.Hapa ni Capital ndio inayo takiwa.