Powered By Blogger

Tuesday, May 24, 2011

Tundu Lissu na wenzake waswekwa Lupango.

                                                      Mh. Tundu Lissu

Mwanasheria na mwanaharakati maarufu Mh. Tundu lissu(Mb) na watu wengine 7, jana walifikiswa katika mahakama ya wilaya ya Tarime baada ya kukamwata katika hospitali iliyohifadhi miili ya marehemu hao. Mheshimiwa huyo na wenzake walisomewa mashtaka yanayowakabili na kurudishwa  lupango baada ya utaratibu wao wa dhamana kutokukamilika. Wengine waliofikiswa mbele ya Mahakama hiyo ni Mwanasheria wa LEAT ndugu Nyambea Stanslaus, Mwita mwikwabe ambae alikua mgombea wa Chadema katika jimbo hilo la Tarime. Majina ya watuhumiwa wengine hayakuweza kupatikana mara moja.

Mh. Lissu na wenzake walipelekwa  lupango baada ya kukamatwa na polisi Wakiwa katika Hospitali iliyahifadhi mwili wa marehemu hao na walikuwa wakifuatilia maiti za watu waliouawa katika vurugu mgodini ili leo (juzi) ziende kuzikwa. Kamanda wa Polisi wa Wilaya hio hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia sakata hilo.

No comments: