Kaka habari, Mimi ni kijana(Jina kapuni), mkazi wa Dar es salaam. Wiki iliyopita nilipigiwa simu na rafiki yangu akiniomba akaunti namba yangu ya benki, kwamba anataka hela yake itumwe kwenye hio akaunti.Mie bila hiyana nikamkubalia maana ni mtu tulie naye karibu. Sasa after few days akaniomba nikaangalie kama io hela imeingia, nikaenda atm kucheck kama hio hela imekua deposited. Cha ajabu nikakuta mamilioni ya shillingi nikajalibu kukomand kiasi kidogo cha fedha na zikatoka.
Baada ya hapo nikawasiliana na huyo rafiki yangu kumwambia pesa yake imeingia but nikamuuliza mbona nipesa nyingi sana. Akanitoa wasiwasi kwamba hela hizo hazina tatizo lolote. A day thereafter nikapigiwa simu na polisi wakitaka next week nifike kutoa maelezo maana hio ilikua pesa ya wizi . Kimsingi hio hela haikuchukuliwa. Lakini niko njia panda maana nahofu kuingizwa kwenye jambo nisilokua nahusika. Nahitaji ushauri wa kisheria juu ya hili. Asante.
No comments:
Post a Comment