Powered By Blogger

Saturday, May 14, 2011

Wanafunzi Sekondari ya wasichana wamuua Mlinzi wa shule.

Hivi Majuzi Wanafunzi wa shule ya sekondari Tabora( ya wasichana) wamemuua Mlinzi wa shule yao jina halikuweza kufahamika mara moja, kwa tuhuma za wizi wa mali zao.Mlinzi huyo aliuawa alipokutwa akiiba mali za wanafunzi hao. Wanafunzi hao wameeleza ya kwamba kwa muda mrefu sasa kumekuwapo na wizi shuleni kwao, na walikua na imani kwamba wezi wa mali zao hutoka maeneo ya jirani kwakua shule yao haikua na uzio.

Baadhi ya  wa wanafunzi hao, Consolata Kikoti na Flora Mtaondwa waliweka bayana kua wanafunzi wengi walichoshwa na upotevu wa vitu vyao, ndomaana waliamua kujichukulia sheria mkononi(mob justice)

Mkurugenzi wa kampuni ya Rukwa Security Co. Ltd yenye dhamana ya kulinda shule hio na Kamanda wa Polisi wa Mkoa afande Liberatus Barlow walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kimsingi kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mara kwa mara, binadamu wote ni sawa na hakuna binadamu aliye juu ya sheria. Kila binadamu anayo haki ya kuishi. Ni makosa kisheria kujichukulia sheria mkononi; kwani kuna vyombo vilivyokasimishwa mamlaka ya kisheria ya kuwatia hatiani watuhumiwa pale inapothibitika bila shaka yeyote wamefanya kosa lolote la jinai. frankiestong@gmail.com





No comments: