Powered By Blogger

Wednesday, May 11, 2011

Wakamatwa kwa mauaji ya vikongwe tisa.



  
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon. N. Sirro
 
 
Polisi jijini Mwanza, inawashikilia watu takribani 14 kwa tuhuma za mauaji ya vikongwe katika Wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza kwa imani za uchawi na ushirikina. Taarifa hii metolewa na Kamananda Mkuu wa Polisi wa jiji la Mwanza Simon sirro. 
 
kamanda huyo amebainisha ya kwamba msako wa polisi uliofanywa katika wilaya mbalimbalin za Geita, Misungwi ulipelekewa kukamatwa kwa watuhumiwa hao waliotumia mapanga na silaha nyingine za jadi kutelekeza uhalifu wao. Aidha aliwataja baadhi ya wahalifu walioshirikiana na waganga wa jadi katika kutelekeza ukatili huo.

Sirro amebainisha ya kwamba watuhumiwa hao waliokwisha kamatwa wamewataja baadhi ya watu waliowatuma kutekeleza ukatili huo, baadhi ya watu hao ni waganga wa tiba za jadi waliotoa mchango wa kuwapa watuhumiwa "dawa" kabla na baada ya kutekeleza uhalifu huo. Kamanda huyo alifafanua zaidi na kubainisha ya kwamba waalifu walipewa dau la shilingi 100,000 hadi 200,000/= ili kutekeleza uhalifu wao.
 
Kwa mujibu wa Kifungu cha 196 na 197 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16, iwapo watuhumiwa hao watakutwa na hatia watahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

frankiestong@gmail.com

No comments: