Powered By Blogger

Tuesday, May 3, 2011

Uharibifu wa matembele wamfikisha pabaya

MKAZI wa Tabata Msimbazi Christina Peter (35), amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni kwa madai ya kuharibu matembele ya jirani yake.Kesi hiyo imesomwa na Karani Hyasinta Mambo mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Adelf Sachore.

Imedaiwa kuwa Aprili 2, mwaka huu, saa 2 asubuhi, Tabata Msimbazi,mshitakiwa alikwenda kwenye bustani ya mbogamboga ya mlalamikaji Edson Peter na kuharibu mboga zote zilizokuwemo. Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi itatajwa tena Aprili 25, mwaka huu.

Wakati huo huo mshitakiwa mwingine, Mohamedi Rashid (32), mkazi wa Vingunguti Machinjioni amefikishwa katika Mahakama hiyo kwa tuhuma za wizi.Kesi hiyo imesomwa na Karani Hyasinta Mambo mbele ya Hakimu Adelf Sachore. Chanzo gazeti la Darleo.

No comments: