Powered By Blogger

Monday, May 9, 2011

Talaka ndani ya Sheria ya ndoa!



TALAKA si neno geni na jipya katika jamii zetu zinazotuzungua maana ni kati ya maneno yaliyozoeleka midomoni au masikioni mwa watu wengi katika ulimwengu wa sasa.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, talaka ni kitendo cha wanandoa kuachana na mahusiano ya kindoa yaliyokuwa baina yao.
Kwa mujibu wa ya sheria ya ndoa ya Tanzania, sura ya 29 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002, talaka ni kitendo cha mahakama yenye mamlaka katika shauri linalohusika, kutoa tamko la kuivunja ndoa iliyokuwapo,kwa sababu mbalimbali.

Kiistoria, sheria ya kiingereza(Common law) , ilikua haitambua uwepo wa talaka au sababu yeyote ile ya kuivunja ndoa kwa msingi wa talaka.” Hii ilitokana na dhana ya kwamba alichokiumba Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha”.Lakini baada ya miaka mingi kupita, sheria ya talaka ilianza kutumika nchini Uingereza baada ya sababu kadhaa za kisheria za kuvunja ndoa kwa talaka kuanzishwa.

Sheria ya Talaka (The Divorce Act) ya mwaka 1969 ilianzishwa nchini Uingereza kufuatia ripoti ya askofu Kent wa nchini humo. Baadaye serikali ya Tanzania kupitia tamko la serikali (Government Notice) namba 1 ya mwaka huo, iliyojulikana kama White Paper ilichukua msimamo na mtazamo huu wa sheria ya Kiingereza juu ya talaka.

Mnamo mwaka 1971, Sheria ya ndoa ilitungwa. Sheria hii ilileta mabadiliko makubwa ya kimsingi ya sheria juu ya talaka. Sheria  hii ilitambua umuhimu wa taraka hivyo  kukubali sababu moja tu inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na mahakama kwa tamko la talaka. Sababu hii moja ni kwamba wadaawa wanatakiwa kuithibithishia mahakama kwamba ndoa yao imevunjika kabisa na haiwezi kurekebishika kutokana na kasoro zisizo weza kurekebishika. Kiingereza tunasema” marriage has broken up irreparably au marriage has broken up beyond repair”. Ndoa iliyovunjika beyond repair ni sawa na garri lililoharibika haliwezi kutengenezeka tena ”light off” Hivyo, sheria ya Tanzania(bara) katika hili nayo ikachukua sababu moja inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na talaka.

Swali la kujiuliza hapa ni JE MAHAKAMA ITATHIBITISHAJE KUA NDOA IMEVUNJIKA KABISA NA HAIWEZI KUREKEBISHIKA?
Kuna sababu kadha wa kadha, zinazoweza kutumiwa na mahakama kuthibithisha ya kwamba ndoa imevunjika asilani na katu haiwezi kurekebishika.Sababu hizo ni pamoja na:-
a.     uzinifu nje ya ndoa [adultery]
b.    ukatili pamoja na     [cruelty]
c.      kumkimbia/kumtelekeza mwanandoa mwezako [desertion]

Uzinifu;- ni mojawapo ya vielelezo zinazoipa mahakama mamlaka kisheria kuivunja ndoa yoyote. Hata hivyo, unatakiwa kujua uzinifu una maana nyingi kutegemea na eneo husika.

Kimsingi uzinifu ni kitendo cha mwanandoa mmoja kufanya ngono nje ya mahusiano yake ya ndoa iliyo halalishwa.
Hapa katika kuondokana na wasiawasi wa kuweza kushindwa kuthibitisha uzinifu, sheria imetoa dhana kwamba pale tu itakapokutwa mume na mke wamelala pamoja na wako watupu, basi dhana hapa ni kwamba wametoka au wanataka kufanya ngono.

Dhana hii kama ilivyoanzishwa na mahakama katika shauri la Denise dhidi ya Denise, Jaji Single anasisitiza kwamba dhana hii ni ngumu kuipinga isipokuwa kama itathibitika kwamba mwanaume aliyekutwa ni hanithi au mwanamke huyo ni bikira.

Na uthibitisho wa uzinifu nje ya ndoa ni kama uthibitisho wa katika kesi ya jinai ambapo anayelalamika anatakiwa kuithibitishia mahakama pasi na shaka kwamba uzinifu umetokea.

Kwa upande wa Uingereza, kama itathibitika kwamba kulikuwa na uzinifu na kwamba mtoto alizaliwa nje ya ndoa, pia atahesabika ni mtoto haramu na hivyo kukosa haki zake zote kwa mzazi wake wa pili.
Hata hivyo, mara nyingi uzinifu unaweza kuthibitishwa na ushahidi wa mazingira kama vile mmoja wa wanandoa kuwa na ugonjwa wa zinaa na kadhalika.

Kifungu cha 170(2) cha sheria ya ndoa ya Tanzania, kinatoa maelekezo juu ya ushahidi wa aina hii.Hata hivyo, uzinifu si lazima uwe sababu ya mahakama kutoa talaka. Mahakama kwa kuzingatia mazingira ya kesi husika inaweza kuamuru mtu aliyefanya uzinifu na mmoja wa wanandoa kumlipa fidia muathirika wa uzinifu huo.


Ukatili pia ni kielelezo mojawapo ya vielelezo zinazoweza kuithibitishia mahakama kwamba ndoa hii ina kasoro zisizoweza kurekebishika. Kwenye shauri la Gollins v. Gollins, mahakama ilibainisha kwamba, hakuna maana ya moja kwa moja ya ukatili, lakini ni matendo yasiyothilimika na kuvumilika ndani ya ndoa. Maana hii haitofautianai sana na ile iliyotolewa katika shauri la  Said Mohamed v. Zena Ally,  ambapo ukatili hujumisha matendo au mienendo ya kuhatarisha, afya, maisha na utu wa mwanandoa. Ieleweka kwamba  sababu hii ya ukatili itatofautiana kutokana na mazingira na mazringira  hata utamaduni wa wanandoa wenyewe.kumtelekeza mwanandoa mwezako; kifungu 107(2) (e) cha sheria ya ndoa ya mwaka, 1971. Iwapo mwanandoa kambia au kamtelekeza  mwenzaka kwa kipindi kisichopungua miaka 3. 

Hii kithibithisho tosha kwamba ndoa imevunjika na haiwezi kurekebishika. Kumtelekeza mwanandoa huweza kutokea  katika nyanja mbili(2) tofauti. Mosi, pale mwanandoa anapoamua kuhama ndani ya nyumba ya ndoa na kuhamia sehemu nyingine bila kumjali mwenzake(simple desertion),hii ilisemwa katika shauri la Mummery v. Mummery. Ikumbukwe ya kwamba kumtelekeza mwanandoa si lazima kuhama nyumba pekee; vilevile huambatana na mwanandoa kutotoa matunzo mbalimbali ya kimsingi ndani ya ndoa.

Pili,kuna (constructive desertion), hii tutokea pale ambapo mwanandoa mmoja kumfanyie mwenzake matendo yanayomfanya mwenzake kuamua kuikimbia nyumba ya ndoa. Aina hii ilitokea kwenye kesi ya Mariam Tumbo v. Harold Tumbo.

Ikumbukwe ya kwamba; Makamana ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kisheria ya kuvunja ndoa baina ya wanandoa; Mahakama imepewa mamlaka hayo pale ambapo itathibitika ndoa imevunjika na haiwezi kurekebishika tena. Mahamaka itathibitisha hayo kwa vielelezo tajwa hapo juu.
frankiestong@gmail.com

1 comment:

Anonymous said...

ts nice and appreciated