Powered By Blogger

Monday, May 30, 2011

Mama akamatwa na polisi kwa kuuza bikira ya Mwanae: Tsh 15 Millioni

Mama mmoja kwa jina la Felicia Rea Mclure miaka 32 anayetoka katika mji wa  Salt Lake nchini Marekani, amefunguliwa mashtaka kwa kosa la kutaka kuuza Bikira ya mwanae mwenye umri wa miaka 13 kwa Dola 10,000 za Marekanai sawa na zaidi ya Tsh million 15  za kitanzania.

Bikra ya binti huyo ilikua iuzwe kwa bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Don. Binti huyo aliieleza Mahakama kwamba awali alikubali kufanya ngono na Don kulingana na makubaliano yaliyofikiwa baina yake, Don na mama yake; lakini baadae aliamua kukataa.

Mwanamama Felicia Re McClaure

Mpango wa mama huyo ulitibuka baada ya rafiki wa kiume"boyfriend" kukuta mlolongo wa ujumbe wa simu za mkononi ikielezea namna ambavyo mama huyo alipanga kutekeleza udhalimu huo. Mama huyo alikiri kwamba aliwahi kumpeleka Binti yake kwa Don ili kumuonesha namna alivyoumbika.

Mama huyo vilevile anakabiliwa na kosa la kumpiga picha za utupu binti yake huyo na kwenda kuziuza kwa wanaume na hatimaye kujipatia fedha.Hakimu ya mahakama hiyo ya Wilaya amebainisha ya kwamba, uchunguzi bado unaendelea ili kumpata Don na wanaume wengine ambao waliwahi kuuziwa picha na mwanamama huyo.
Mahakama ya Wilaya ya Utah

Felicia ambaye amekiri kutenda makosa hayo , anakabiliwa na mashtaka mawili katika Mahakama ya Wilaya ya Utah, mosi ni kosa la unyanyasaji wa ngono na mengine mawili ya unyonyaji wa kingono kwa mtoto mdogo. Mama Huyo kwa sasa yuko rumande baada ya kukosa dhamana ya Dola 250,000 sawa na zaidi ya shilingi Millioni 380 za kitanzania. Iwapo mwanamama huyo atapatikana na hatia atahukumiwa kusota jela kwa miaka mingi.


No comments: