Powered By Blogger

Wednesday, January 30, 2013

MCHUNGAJI EAGT APANDISHWA KIZIMBANI



Mchungaji wa kanisa la Evangelical Assemblies of God nchini EAGT Daniel Mwasumbi amefikishwa katika mahakama ya mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari jijini Mbeya.

Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Mheshimiwa Gilbert Ndeuluwo, mchungaji Mwasumbi mwenye umri wa miaka 57 alisomewa mashitaka na kukana kutenda makosa hayo.

Akisoma maelezo Mwanasheria wa serikali Achilaus Mulisa alisema kati ya mwaka 2008 hadi 2011 mshitakiwa huyo alimbaka mwanafunzi Neema Benson mwenye umri wa miaka 17 kinyume  cha sheria za kanuni ya adhabu 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili E  pamoja na kanuni ya adhabu ya 131 iliyorekebishwa mwaka 2002.

Katika shitaka la pili mshitakiwa huyo anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi huyo katika kipindi hicho kinyume cha sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978.Hata hivyo mshitakiwa alikana makosa yote yanayomkabili.Na kwa mujibu wa mwanasheria wa serikali upelelezi juu ya kesi hiyo umekamilika kwa ajili ya kuwaleta mbele ya mahakama mashahidi watatu.

Mshitakiwa aliachiwa huru kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na mtu mmoja kwa thamani ya fedha taslimu shilingi milioni 2 na kesi hiyo imeahirishwa hadi jumatano ijayo Januari 30 mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa. Chanzo Sahara Media.

No comments: