Mchungaji
wa kanisa la Evangelical Assemblies of God nchini EAGT Daniel Mwasumbi
amefikishwa katika mahakama ya mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kumbaka na kumpa
mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari jijini Mbeya.
Mbele
ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Mheshimiwa Gilbert Ndeuluwo, mchungaji
Mwasumbi mwenye umri wa miaka 57 alisomewa mashitaka na kukana kutenda makosa
hayo.
Akisoma
maelezo Mwanasheria wa serikali Achilaus Mulisa alisema kati ya mwaka 2008 hadi
2011 mshitakiwa huyo alimbaka mwanafunzi Neema Benson mwenye umri wa miaka 17
kinyume cha sheria za kanuni ya adhabu 130 kifungu kidogo cha kwanza na
cha pili E pamoja na kanuni ya adhabu ya 131 iliyorekebishwa mwaka 2002.
Katika
shitaka la pili mshitakiwa huyo anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi huyo katika
kipindi hicho kinyume cha sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978.Hata
hivyo mshitakiwa alikana makosa yote yanayomkabili.Na
kwa mujibu wa mwanasheria wa serikali upelelezi juu ya kesi hiyo umekamilika kwa
ajili ya kuwaleta mbele ya mahakama mashahidi watatu.
Mshitakiwa
aliachiwa huru kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na mtu mmoja kwa thamani ya
fedha taslimu shilingi milioni 2 na kesi hiyo imeahirishwa hadi jumatano ijayo
Januari 30 mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa. Chanzo Sahara Media.