Powered By Blogger

Friday, May 6, 2011

Tendo hili la Maofisa wa TRA lina uhalali kisheria?


Kaka asante kwa kuanzisha blog hii, mimi ni  mfanyakazi wa benki moja, huko Geita. Wiki chache zilizopita road licence ya gari yangu iliisha. Nikaenda kukata  nyingine kwenye ofisi za mamlaka ya mapato. wakanipa stakabadhi inayoonesha kuwa nimelipa lakini nembo:”stika” ya road licence niliambiwa nisubiri maana zinakua processed kwenye ofisi kuu ya Mamlaka ya Mapato Mwanza.

Hivi majuzi, nilikuja kikazi Mwanza mjini na nikiwa katika pilika pilika zangu nilipaki gari sehemu moja ya maarufu kwa jina la pizzeria. Niliporudi nikashangaa kutokukuta plate namba za gari yangu nilichanganyikiwa sikujua la kufanya. Nilipouliza wadau nikaambiwa zimechulukiwa na maofisa wa  Mamlaka ya mapato. Sasa kwakua mida ilikua imeenda niliamua kuliendesha gari hivyohivyo mpaka  nyumbani.

Jana tarehe 05/5/2011 nilimtuma ndugu yangu afuatilie plate namba za hio kwenye ofisi za TRA. Alipofika akaambiwa gari langu lilikua halina road licence ndio maana walichukua plate namba. Lakini walipooneshwa ile stakabadhi  bado nikalipishwa faini ya  shilingi 25,000/= kama gharama zao za usumbufu.

Je kaka, hivi ni haki mimi kunyanyasika kiasi hiki? Kama ushuru nilipa tena mapema na wao wakaniambia nisubirie hio stika then waotoa plate namba za gari na kunipiga faini isiyokua na msingi wowote. tena wa Au ndivyo sheria zinavyosema. Please nipostie kwa wadau wanishauri nifanye  maana nahisi kuonewa.

Mimi Mdau wa blog.

4 comments:

Anonymous said...

Mkuu,

Hongera kwa kuanzisha blog ya Sheria, maana ni sekta muhimu ambayo hata hivyo uelewa wetu bado uko chini.

Sasa mbona hujibu maswali wanayouliza wadau? Naamini nitakuwa naongea kwa niaba ya wasomaji wote nikisema kuwa tunakuja hapa tukitegemea kupata ushauri wa kisheria.

Ukiendelea kutojibu maswali basi hii blog itakufa mkuu.

rugy said...

ndugu pole sana.

Najua kuwa si halali kwa mtu kufanya hivyo ilhali wakijua kuwa kosa ni la kwao kutokukupa road licence, hasa katika situation kama hizo ambazo huwa unasafiri kwenda umbali mrefu.

Ila kitu kimoja mabacho ungekifanya kabla ya kuhama mji ni ungerudi pale TRA-Geita na ukawauliza kama zipo, na kama wangesema hakuna, then ungewambia situation uliyonayo na wakakupa suggestion ya nini cha kufanya ili usije ukakwazika katika mji mwingine.

Ila all in all, hii inaonyesha jinsi vitengo vya serikali visivyokuwa na uhakika katika ufanishi kazi wake

Anonymous said...

pole sana, kwa matatizo yaliyokupata. kwa mtazamo wa kawaida na haraka haraka sidhani kama ilikua sahihi kwa maofisa hao wa TRA, kufanya kitendo walichokifanya. Kama kweli ulilipa na kupewa stakabadhi kwanini wakuathibu kwa uzembe wao wa kutokukupa stika kwa muda muafaka? Ninachokushauli mimi nenda kwa uongozi upeleke malalamiko yao husika, pengine waweza kusaidiwa

FRANK.T.MUNAKU said...

Mdau, Pole sana na tatizo linalokukabili. kwa kuangalia maelezo la tukio hili nashangaa ni kwa nini Maofisa hao wa TRA..kuamua kufanya hivyo. Kimsingi kama ulishalipa inatia shaka kwanini huadhibiwe kwa kosa ambalo hujalifanya.Nakushauli upeleke malalamiko yako kitengo cha malalamiko(TRA)kama kipo, au kwa Uongozi wa mamlaka hiyo hapo mwanza. Iwapo uongozi utakataa kutatua tatizo lako basi kuna taratibu za kisheria kupeleka dai lako Mahakamani. Tafuta mawakili wakupe mwongozo zaidi.