Powered By Blogger

Saturday, July 14, 2012

TUNDU LISSU AWADHIHAKI MAJAJI




MH. RAIS KIKWETE NA JAJI MKUU

Mh. Tundu Lissu ambae pia ni waziri kivuli wa sheria na Katiba, huenda akaburuzwa kwenyekwenye Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kwa kutoa maneno yenye mlengo wa dhihaka kwa  Waheshimiwa Majaji wanaoteuliwa  na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akichangia hatuba hio kama Msemaji wa kambi ya upinzani kwenye masuala ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Tundu Lissu alitamka maneno yenye mlengo wa dhihaka wa waheshimiwa hao wa Mahakama, ya kwamba baadhi yao hawana uwezo na pia kumkosoa Raisi kwa uteuzi wake huo wa watu wasio na uwezo.  

ALICHOKISEMA MWANASHERIA MKUU JUU YA KAULI ZA LISSU.


MWANASHERIA MKUU JAJI WEREMA

Mh. Werema alisema, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ana wajibu kuwaelekeza wanasheria hasa waliopo bungeni, kufuata misingi ya taaluma bila kuathiri haki yao wakiwa wabunge.“Nimefedheheka sana na mambo mawili yaliyotokea bungeni,” alianza kusema kwa sauti iliyosikika kuwa yenye huzuni, na kusema (mambo hayo) yamo kwenye hotuba ya Lissu.

Werema alisema baada ya Lissu kukosoa uteuzi wa majaji huku akisema wengine hawana uwezo, alizungumza naye ili kumuomba ayaondoe kwenye hotuba yake, lakini hakusema kama (Lissu) alikubali ama kukataa.Alisema maneno hayo ambayo yapo ukurasa wa tisa ibara ya pili ya hotuba hiyo, anaomba Lissu ayaondoe kabla ya kupitishwa bajeti ya wizara hiyo, vinginevyo kiti cha Spika kimuamuru (Lissu) aambatanishe vielelezo vinavyothibitisha maelezo yake.

Werema alisema Lissu ni mtaalamu wa sheria asiyetakiwa kufedhehesha mahakama na majaji, lakini pia alikiuka kanuni za Bunge kwa kuwataja watu wasiokuwa bungeni.Alitaja maeneo mengine yaliyomo kwenye hotuba ya Lissu na ambayo yanastahili kuondolewa ni yaliyohusu kushamiri kwa vitendo vya utekaji, utesaji na kudhuru watu, akitoa mfano wa Mbunge Kiwia, Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea, Waziri wa Uchukuzi na Dk Harrison Mwakyembe.

Werema alisema vitendo hivyo na vile vya umbakizaji kesi kwa raia wasiokuwa na hatia vilivyomo kwenye hotuba ya Lissu, havina ukweli bali vinapotosha.Wakati akimalizia kutoa hoja yake, Werema alisema Lissu anapaswa kutambua kwamba kuna Kamati ya Maadili ya Bunge na kwamba kuna uwezekano `akaburuzwa’ huko kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Wakati Werema akizungumza, Lissu alisimama kuomba mwongozo wa Spika, lakini Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, alimtaka akae ili Mwanasheria Mkuu amalize kuwasilisha hoja.Lakini Mwanasheria Mkuu alipomaliza kuzungumza, Mbunge Said Mkumba, alisimama kutumia ibara ya 68(7) ya kanuni za Bunge na kutaka muongozo wa Spika kwa kile alichosema, Lissu amevunja sehemu ya kiti anachokikalia bungeni.Baada ya Mkumba kuzungumza, Mhagama alimuita Lissu ambaye alisimama na kusema mwenye mamlaka ya kumjibu Mkumba ni kiti cha Spika, lakini Mhagama ‘alimgeuzia kibao’ na kumwambia amepoteza nafasi ya kutaka muongozo.

WAZIRI CHIKAWE ANENA
Waziri Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alielezea kusikitishwa na kauli ya Lissu, akisema amesikitishwa na jinsi lilivyosemwa hata kama palikuwa na hoja ya msingi.Alisema ibara ya 112 ya Katiba inaunda Tume ya Mahakama ambayo inamshauri Rais wakati wote na kwamba hakuna ukiukwaji wowote uliofanyika katika uteuzi wa majaji.

Friday, July 13, 2012

MAHAKAMA YAMSAFISHA JOHN TERRY.

John Terry
Terry(31)
 
Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Uingereza Terry(31) , aliyekuwa anakabiliwa na mshataka ya kutoa lugha ya kinaguzi kwa mchezaji mwenzake wa timu ya Taifa ya uingereza hivi punde amesafishwa na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Westiminster, Mh. Howard Riddle kwa kutokupatikana na hatia ya kutoa maneno hayo.

Mwendesha mashtaka katika kesi hiyo alisema kwamba mnamo tarehe 23 Octoba mwaka jana wakati wa mechi ya ligi kuu baina ya CHELSEA  na QPR, Terry alitoa maneno ya kibaguzi kwa mchezaji mwenye asili ya kiafrika Anton Ferdinand.Kesi hii ndio ilipelekea Mcheza soka huyo, Terry kunyanganywa majukumu yake ya unaodha wa timu ya taifa ya uingereza, vilevile ilipelekea kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Capello. 

Mwendesha Mashitaka katika kesi hiyo bwana Duncan Penny alisema ya kwamba Terry alitoa maneno yafuatayo kabla ya kufungwa mdomo na mchezaji mwenzake wa timu ya chelsea, Obi Mikel; "Fuck off, fuck off", "yeah, yeah", "and", and then "you fucking black cunt, fucking knobhea. 

kesi hii haikua ya kawaida  kwa waendesha mashtaka kwa kua si Anton Ferdinand aliyepeleka malalamiko Mahakamani. polisi walianzisha upelelezi  kama matokeo ya malalamiko yaliyotolewa na afisa moja wa polisi  aliyekua anaagalia mchezo kwenye televisheni. Afisa huyo alisema kwamba Terry alitoa lugha ya kibaguzi kwa mchezaji mwenzake.

Iwapo angepatikana na hatia, Terry angekabiliwa na faini ya Paundi  £ 2,500, takriban shillingi Millioni Tano za Kitanzania.

Wednesday, July 11, 2012

Ndoa ya Dr. Slaa, Josephine Yapingwa Kortini



Dr. Slaa na Mh. Rose Kamili Enzi zao


ROSE Kamili anayedai kuwa ni mke wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amefungua kesi Mahakama Kuu akiiomba isimamishe ndoa ya kiongozi huyo na mke mwingine inayotarajiwa kufungwa Julai 21, mwaka huu wilayani Karatu Mkoa wa Manyara.Dk Slaa anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Josephine Mushumbusi. Kamili ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), pia anaiomba Mahakama iamuru Dk Slaa amlipe Sh50 milioni za fidia aliyotumia kujihudumia pasipo matunzo ya mumewe huyo.
 
Dr. Slaa na Bi Josephine Mshumbuzi

Mbunge huyo kupitia kwa Wakili wake, Joseph Thadayo, aniomba pia Mahakama iamuru Mushumbusi amlipe kiasi cha Sh500 milioni za fidia ya maumivu aliyoyapata kutokana na kitendo chake cha kuingilia ndoa yao.

Kesi hiyo namba nne ya mwaka 2012 iliyopangwa kusikilizwa na Jaji Lawrance Kaduli, inatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza leo.

Katika hati hiyo ya madai, mbunge huyo anadai kuwa ndoa inayotarajiwa kufungwa kati ya Dk Slaa na Mushumbusi ni batili kwa sababu kuna ndoa nyingine halali na inayoendelea kuishi kati ya Slaa na Kamili iliyofungwa mwaka 1985.

Alidai baada ya kufugwa kwa ndoa hiyo, Juni 18, 1987 walifanikiwa kupata mtoto wa kike anayeitwa Emiliana Muchu na baadaye Septemba 23, 1988 walipata mtoto mwingine wa kiume, Linus Amsi.

Katika uhusiano wao, Dk Slaa akiwa ni Padri wa Kanisa Katoliki, alifanya taratibu zilizomwondosha katika nafasi hiyo na kuanza maisha ya familia.

Baada ya taratibu hizo, jamii ya Watanzania iliwatambua kama mume na mke na hata kumbukumbu za hati za kimataifa kama za kusafiria ziliwatambua kuwa wanandoa.

Kamili aliendelea kudai katika maelezo hayo kuwa yeye na Slaa waliishi maisha ya ndoa yenye amani yaliyowawezesha kupata mali kadhaa walizomiliki kwa pamoja ikiwemo nyumba iliyopo kwenye Kiwanja namba 609 Kitalu E iliyopo Sinza, Dar es Salaam, nyumba ya makazi iliyopo Kijiji cha Gongali huko Karatu na vifaa mbalimbali vya nyumbani.

Hati ya mashtaka imeendelea kudai kuwa uhusiano kati ya Slaa na Kamili, ulianza kuharibika mwaka 2009, baada ya mume huyo kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine kinyume cha sheria… “Tangu mwaka huo 2009, Slaa akaitelekeza familia yake kwa kutoipatia huduma,” imeeleza hati hiyo.Kamili anaiomba Mahakama iamuru kuwa yeye na Dk Slaa bado ni mke na mume na kwamba Mushumbusi aliingilia ndoa yao hivyo izuie ndoa inayotajiwa kufungwa Julai 21, mwaka huu huko Karatu, Manyara.

Kamili pia amewasilisha hati hiyo ya mashtaka kwa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akimweleza Askofu Mkuu huyo wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam kuwa moja ya Parokia za Dar es Salaam zina taarifa ya ndoa hiyo.
Nakala ya madai hayo pia imewasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Msajili wa Ndoa na kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbulu.

Dk Slaa: Nimeyazoea
Alipotakiwa kuzungumzia kesi hiyo nje ya Mahakama, Dk Slaa alisema: “Hayo mambo nimeyazoea na kimsingi hayanipi shida yoyote.”Alipoulizwa endapo anajipanga vipi kulipa fidia hiyo alijibu: “Kesi ni kesi hivyo siyo kila kinachoombwa kwenye kesi lazima kilipwe.”

Hata hivyo, Dk Slaa alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa kuwa liko kwa mawakili wake lakini akasema amebaini kuwa hizo ni hila na michezo michafu ya kisiasa.“Kwanza siyo pingamizi moja tu, kuna pingamizi mbili mahakamani lakini kwa ufupi ifahamike kuwa hizo ni hila.” Chanzo gazeti la Mwananchi.

Sunday, July 8, 2012

MAWAKILI NA WAZEE WA BARAZA KATIKA MAHAKAMA ZA MWANZO.



 1.0 UTANGULIZI


Kwa miongo mingi sana, Mashauri mbalimbali katika Mahakama za Mwanzo yamekua yanaongozwa na Mahakimu wasio wanasheria pamoja na wazee wa Baraza. Mawakili kama maofisa wa Mahakama hawakupewa na nafasi kuwawakilisha wadaawa mbalimbali katika Mahakama hizo za Mwanzo.  Kimsingi Waraka wa maendeleo ya UTUMISHI WA Umma Namba 1 wa mwaka 2010, umeondoa au kufuta nafasi za Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na kuwaweka Mahakimu wakazi wa Mahakama za Mwanzo.

Mabadiliko haya kwa namna moja au nyingine yatapelekea kuwepo mabadiliko ya sheria , na pengine kuakisi nafasi na umuhimu wa Mawakili na Wazee wa Baraza katika Mahakama za Mwanzo nchini.

1.0   NAFASI NA UMUHIMU WA MAWAKILI KATIKA MAHAKAMA ZA MWANZO
Baadhi ya Mawakili wapya walioapishwa Juzi


Ibara ya 13(6)a ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inaeleza ya Kwamba kila mtu ana haki ya kusikilizwa, Haki ya kusikiliza kwa namna moja au nyingine huusisha haki ya kuwakilishwa na Mawakili katika Mahakama za Mwanzo. Kimsingi wananchi wengi wamekua wakiikosa haki hii muhimu, iliyowekwa kikatiba pia kutolewa Maamuzi mbalimbali kama mojawapo ya msingi wa “principles of natural justice”.  Wananchi wamekua wakiikosa haki hii kutokana na mfumo na muundo wa Sheria zilizopo zinazowanyima Mawakili nafasi za kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama hizo za Mwanzo kama ilivyobainishwa katika  Sheria ya Mahakama Sura ya 11, Rejeo la Mwaka 2002.

Kuna na umuhimu mkubwa iwapo mawakili watapewa nafasi kisheria kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama za Mwanzo kama ifuatavyo;

a. Kupunguza mrundikano wa kesi Mahakamani, mawakili Kama maofisa wana majukumu ya kisheria kuisaidia Mahakama kutoa Maamuzi ya Haki. Iwapo pande za wadaawa zitawakilisha na Mawakili Mahakamani, yumkini mashauri mengi yatamalizika mapema, hivyo kuondoa Mrundikano wa kesi usio na tija Mahakamani.

b. Kumalizika Kwa Mashauri kwa Wakati, iwapo Mawakili watapata fursaya kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama za Mwanzo. Watawaongoza wadaawa au wateja wao kutatua migogoro yao kwa kutumia njia mbadala za kutatua migogoro hiyo yaani” Alternative Dispute Resolution”.

c. Wadaawa kupata haki yao ya kuwakilishwa, kama ilivyobainishwa hapo awali sio kila mtu ana uwezo wa kusimama mbele ya Mahakama ya kujitetea. Iwapo Mawakili watapata fursa ya  kuwawalisha wateja wao hii itatoa fursa kwa wadaawa wao kupata  ya kuwakilishwa ipasavyo katika mashauri yanawayowakabili.

d. Ajira, Kuanzishwa kwa Shule ya Sheria Nchini” Law School of Tanzania”, kwa namna ya pekee kumepelekea ongezeko kubwa la Mawakili nchini, wengi wa mawakili hao ni Vijana wasio na fursa ya kuajiliwa Serikalini, au Taasisi mbalimbali kutokana na ufinyu wa ajira Nchini. Hivyo basi nafasi hii itatua fursa ya ajira kwa Mawakili wengi kuwawakilisha wateja wao hasa kwa wananchi wengi walio vijijini ambapo kuna Mahakama Nyingi za Mwanzo.

2.0   NAFASI NA UMUHIMU WA WAZEE WA BARAZA KATIKA MAHAKAMA ZA MWANZO.

wazee wa Baraza wamekua Wakitumika si katika Mahakama za Mwanzo pekee Vilevile Katika  Mahakama Kuu, Wazee hawa wamekua na Mchango mkubwa sana katika kuisadia Mahakama Kutoa maamuzi ya haki.  Kifungu Cha 7(1) Cha  Sheria ya Mahakama, Sura ya 11 ya Mwaka rejeo la Mwaka 2002, Kinatoa akidi ya Mahakama katika mwenendo wa Mashauri katika Mahakama za Mwanzo ya Kwamba panatakiwa katika kila shauri pawepo na wazee wa baraza wasiopungua wawili.
Na kwamba, maoni ya wazee wa katika Mahakama za Mwanzo ni ya Muhimu na lazima yazingatiwe katika utaoaji wa maamuzi ya haki.  Na kwamba Mahakimu ni lazima wazingatie maoni ya Wazee hao wa baraza.
Swali la kujiuliza ni kama iwapo Mawakili wataruhusiwa kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama za Mwanzo Je kuna ulazima wa wazee wa Baraza kuendelea kuwepo?

Ni rai yangu kwamba wazee wa Baraza Bado wanaumuhimu Mkubwa sana kuendelea kuwepo( kama nitakavyoelezea hapo baadae wapepo katika misingi gani). Kwa uchache umuhimu wa Wazee wa Baraza ni kama Ufuatao;

a. Kwa kua Mahakama nyingi za Mwanzo zipo vijijini, ambapo kuna kesi nyingi sana za zinazohusisha mambo ya Kimila. Wazee wa Baraza ni muhimu hasa katika kuisadia Mahakama Kupata tafsiri mbalimbali za Kimila hasa katika masuala ya Mirathi, Ndoa  na…Kwa Mfano katika jamii ya kisukuma kuna faini ya “ Misango na Ngweke” (hii ni faini ambayo anapewa kijana kwa ajili ya utorosha binti). Uwepo wa wazee hawa kutasaidia sana Mahakimu wa Mwanzo Wakazi katika masuala ya kimila ya Ndoa, Mirathi na madai.
3.0   MUUNDO WA MAHAKAMA
Kwakua Mahakama za wilaya na Hakimu Mkazi zina nguvu sawa katika usikilizaji wa Mashauri ya mbalimbali hususan ya madai. Ni rai yangu kwamba hakuna haja ya kuendelea kua na Mahakama 2 tofauti. Mahakama hizi zingeunganishwa na kupatikana na Moja. Kwani kwa kawaida Rufani za , Mahakama hizi huenda Mahakama Kuu. Kwa mantiki hii basi Muundo huu wa Mahakama shurti ubadilishwe.

4.0   MAPENDEKEZO (NINI KIFANYIKE)
Ni ukweli usiopingika Kwamba Mawakili na uwepo wa Wazee wa Baraza katika Mahakama za Mwanzo nchini una maana kubwa katika kuziboresha Mahakama zetu, ili kutoa maamuzi ya haki na kwa wakati. Ili kufanukisha yote haya yafuatayo yanapaswa kuzingatia na kufanyika;
a.  Madadiliko ya Sheria, Vifungu mbalimbali vya kisheria ni lazimavibadilike katika mantiki ya kuwawezesha Mawakili kuhudhuria Mashauri ya Mahakama za Mwanzo kama ifuatavyo;
          i.     Kifungu cha 33(1) kinachowazuia Mawakili kutowawakilisha wateja wao katika Mahakama za Mwanzo kirekebishwe kutoa Mwanya kwa Mawakili hao kua na fursa hiyo.
        ii.     Kifungu cha 7(1) Cha Sheria Ya Mahakama, Sura ya 11,Rjeo la Mwaka 2002 kinachosema; in every proceeding in Primary Court, including a finding, the Court shall not sit with not less than two assessors.

Ni rai yangu kwamba kwa majukumu ya wazee wa baraza yawe kwenye kesi za madai pekee wa wasipewe nafasi katika kesi ya Jinai kama ambayo Kifungi tajwa hapo juu kinavyobainisha” in ever proceeding” mabadiliko yafanyike ili kuwe na ukomo kwenye mashauri ya jinai yaani” in Civil proceedings in Primary…..” Hii ni kwakua wazee hawa hawana weredi wa makosa mbalimbali ya kisheria.
b. Maoni ya wazee wa Baraza, kwa hali ilivyo hivi sasa maamuzi ya Mahakama ya Mwanzo yanategemea maoni ya Wazee Wa Baraza. Sheria ibadilishwe ili maoni haya ya wazee wa Baraza yewe” not binding” ili kulinda na kuakisi dhana nzima ya uhuru wa Mahakama” Independence of Judiciary”.
c. Miundombinu ya Mahakama za Mwanzo; Mahakama nyingi za Mwanzo zipo vijijini vikiwa na Miundo mbinu mibovu sana, majengo yaliyochakaa hivyo haitokua busara kwa Mahakimu Wakazi tarajiwa wa Mahakama hizo kufanya kazi katika Mazingira haya. Ni rai yangu kwamba za juhudi za hali na mali zifanyike kuboresha mazingira haya ya Mahakama hizi.
d. Lugha ya Mahakama; Kwa hali ilivyo hivi sasa Mashauri ya Mahakama ya Mwanzo yanaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili. Iwapo Mawakili wataruhusiwa kuingia katika Mahakama hizi basi Lugha ya kiingereza itumike kama Mbadala wa Lugha ya Kiswahili. Hivyo basi kifungu cha 13(1) Cha Sheria ya Mahakama, Sura ya 11 rejeo la mwaka 2002 kinachosemeka “the language of primary Court shall be in Kiswahili”.
5.0   HITIMISHO
Ni Rai yangu kwamba nafasi ya Mawakili katika utoaji wa maamuzi ni mkubwa sana, Sheria Zetu zibadilishwe ili kuakisi hali halisi ya mabadiliko haya.

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA YATOA UFAFANUZI KUHUSU UKOMO WA WANANCHI KUTOA MAONI MIKUTANONI.




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqw5BCClIgaOLXWTLBFkP2DxMzCoZ_OAoiPunI_eyWUNckGvbueKfmf963NYhR0zowS_NDfXLGLpn1GRcnfhntCmMdDyMjoM3nQQE23XJhqGFt3w4o-DXbS6tACd8czMAxVUSVw8sQ4_U/s1600/Bw.+Assaa+Rashid+-+Katibu+wa+Tume+.jpg
BWANA ASSAA RASHID

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi kuwa Tume hiyo imeweka ukomo wa idadi ya wananchi wanaotoa maoni katika mikutano yake inayoendelea katika mikoa minane na kuwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika mikutano inayoitishwa na Tume na kutoa maoni yao kwa uhuru na uwazi.

Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid amesema leo (Jumapili, Julai 8, 2012) kuwa Tume ingependa kupata maoni ya kila mwananchi na hivyo haiwezi kuweka ukomo kwa wananchi kutoa maoni katika mikutano inayoiitisha.

Ufafanuzi wa Tume hiyo unafuatia taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari zikinukuu baadhi ya wananchi wakilalamika kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeweka kikomo cha idadi ya maswali na watu wanaotakiwa kutoa maoni yao katika mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi.

Taarifa hizo ziliongeza kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekuwa ikitoa nafasi kumi tu kwa wananchi wanaopaswa kuuliza maswali yasiyozidi kumi katika mkutano mmoja na kwamba, katika baadhi ya Wilaya, ikiwemo Biharamulo yenye Kata 15, ni Kata sita tu ndizo zilizofikiwa na Tume.

“Katika baadhi ya Wilaya, kama Kusini Unguja na Bahi mkoni Dodoma, Tume imelazimika kuongeza muda wa kupokea maoni ya wananchi na wakati mwingine kuongeza idadi ya mikutano hadi kufikia mitatu badala ya miwili kwa siku. Hatua hizi zinalenga kutoa fursa zaidi kwa wananchi kutoa maoni yao,” amesema Bw. Assaa katika taarifa yake kwa vyombo habari.

Kuhusu mikutano iliyofanyika wilayani Biharamulo, Bw. Assaa amesema Tume ilipanga na imefanya mikutano sita kuanzia terehe 2 hadi 4 Julai, 2012 na jumla ya wananchi 267 walitoa maoni yao kwa mdomo na wananchi wengine 265 walitoa maoni yao kwa maandishi.Kwa mujibu wa katibu huyo, vituo ambavyo mikutano hiyo ilifanyika ni Kelenge, Movata, Nyamigogo, Runazi, Nyakanazi na Biharamulo Mjini.

“Katika mikutano hiyo na mikutano mingine yote Tume haikuweka na haitaweka ukomo wa idadi ya wananchi wanaopaswa kutoa maoni,” amefafanua Bw. Assaa na kuongeza kuwa Tume inatambua kuwa wananchi wana shauku kubwa ya kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya.

Hata hivyo, Katibu huyo alisema kuwa ingawa Tume ingependa kumfikia kila mmoja mahali alipo, jiografia ya nchi na muda ambao Tume imepewa, jambo hilo halitawezekana na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo Tume itafanya mikutano kama ratiba iliyotolewa inavyoelekeza.

Akifafanua kuhusu malalamiko kuwa baadhi ya Kata hazitafikiwa na Tume, Bw. Assaa amesema Tume haikupanga ratiba ya mikutano ya kukusanya maoni haikupangwa kwa kuzingatia Kata, bali imepangwa kwa kuzingatia eneo ambalo linaweza kujumuisha wananchi kutoka zaidi ya Kata moja.

Pamoja na kutoa maoni yao kupitia mikutano, Tume pia imewaomba wananchi kuendelea kutumia fursa nyingine kuwasilisha maoniyao kama tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz), barua pepe (maoni@katiba.go.tz) au kwa njia ya posta kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681, Dar es Salaam na S.L.P. 2775,Zanzibar. Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilianza kufanya awamu ya kwanza ya mikutano ya kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa minane tarehe 2 Julai mwaka huu na inatarajiwa kumalizika tarehe 30 mwezi huu. Mikoa hiyo ni Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga. Chanzo Michuzi Blog.

JAJI MKUU AAPISHA MAWAKILI WAPYA


Mdau Fortuatus Mhalila baada ya kuwa wakili

JAJI Mkuu wa Tanzania Chande Othaman amewaapisha na kuwatunuku leseni za kufanya kazi mawakili wa kujitegemea 286 na kuwataka waende vijijini kuwasaidia Watanzania.Kuapishwa kwa mawakili hao wapya kunaongeza idadi ya mawakili kutoka elfu mbili mia tatu kumi na sita waliokuwepo na kufikia elfu mbili mia sita na mbili.
Jopo la Mawakili Wakiwa katika sherehe ya kuapishwa kwao

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuwatunikia mawakili hao Jaji Chande alisema ipo haja kwa mawakili hao kujikita kwenye maeneo ya pembezoni ambayo yana idadi kubwa ya watanzania wenye mahitaji mengi ya kisheria.

Mdau lilian Kowero akitabasamu baada ya kuapishwa kua wakili msomi

Aidha alitoa wito kwa waliojiandikisha kuwa mawakili lakini hawajasajiliwa wafike Baraza la Elimu ya Sheria liwasajili na hatimaye kuapishwa na kuwa mawakili kamili hali itakayosaidia kuongeza idadi ya mawakili nchini.


Nao baadhi ya mawakili walioapishwa Ijumaa hii walikiri kuwepo kwa changamoto ya upungufu huo wa mawakili kwenye maeneo ya vijijini na kubainisha kuwa ipo haja kujikita kwenye maeneo hayo.Kiapo hicho ni sehemu ya mpango mkakati wa kupunguza changamoto ya upungufu wa mawakili kutokana na kwamba idadi hiyo bado ni ndogo kulinganisha na mahitaji ya watanzania ambao ni zaidi ya milioni 41.

Monday, May 28, 2012

WENGI WAMLILIA WAKILI MAARUFU, BONIFACE STANSLAUS.


MKURUGENZI Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) 'Jembe' amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia kutokea kwa kifo hicho.  Marehemu Boniface ameacha pengo kubwa sana kwa wanaasheria hasa waliojikita katika kesi za jinai, kwa weredi wake mkubwa sana wa kudadavua, na kuendesha mashauri mbalimbali ya jinai. Yumkini, weredi wake huo ndio umepelekea mamia ya wanasheria na wadau mbalimbali kutoa maoni yao katika kurasa mbalimbali za kijamii” social networks” kuonesha maoni yao kama ifuatavyo:

MAONI YA WADAU:

Dr. Eliezer Feleshi , DPP alisema bado ofisi yake na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji huyo wa uendeshaji wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa. 


Moses Masinga, wakili msomi wa kujitegemea aliandika facebook , so sad tuliokuwa wote Law School nadhani mnamkumbuka jamaa alivyokuwa JEMBE! Aisee duniani tunapita tu. It is not easy kuamini lakini habari ni hivyo.
Kheri Mbiro, wakili msomi wa kujitegemea aliandika katika ukurasa wake wa facebook, RIP Boniface Stanslaus Makulilo,Sr. State Attorney..your passing away couldn't have been any earlier...quite a crippling blow to the Attorney General's Chambers...indeed many of us never ceased to pick a trick or two up your sleeves whenever you stood up in court...."An authority"..for many..its saddening but the Lord's wishes are unquestionable...we pray for your soul....amen.
Innocent Mhina mwanasheria na wakili wa bank ya posta aliandika;jamaa alikua exta ordinary attorney principles nyingi sana zimetoka kwenye cases alizo argue yeye na zingine kwa kuomba muongozo wa mahakama ususani kwenye ishu ya inquiry at subordinate crts at wht tme iwe conducted and how,.cheki kesi ya seleman abdalah v/s republic you will appreciate him and not only that alikua mwalimu mzuri sana. 
 
Jerry Muro ambae bwana Boniface aliwahi kuendesha kesi yake alisema, R.I.P boniface stanslaus,naibu mkurugenzi wa mashtaka alikuwa mwendesha mashtaka wa serikali kny kesi yangu,japo nilishinda kesi ila alitoa changamoto kny kesi yangu haswa.
WASIFU WAKE:

Boniface alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahaha ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka 2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.

Nyadhifa ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka 2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.Kati ya Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mwanza.Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri ilipofika Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma.


                                       KESI KUBWA ALIZOZIMAMIA;

Miongoni mwa kesi kubwa ambazo mwandishi wa habari hizi amekuwa akimshuhudia akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa nchini

  • sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka jana, iliwahukumu kwenda jela miaka mitano.
  • kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka jana.
  •  kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara Jayankumar Patel "Jeetu Patel' na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.
  • Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja. 

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Boniface mahali pema peponi.Amin.

MAAMUZI YA KESI YA LULU KUSIKILIZWA JUNI 16.


Lulu akiwa Mahakamani
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba Lulu akiwa mahakamani hapo.Lulu akiwasili Mahakamani hapo.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.

Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.

Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.

Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.

Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.Baada ya kusikiliza mabishano hayo
ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.

 
kwani Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 Pamoja na Sheria ya watoto ya mwaka 2009,  suala la umri lina mantiki kubwa sana ya kisheria, kwani mfumo wa kusikilizwa kwa kesi za watoto wenye makosa mbalimbali ya jinai” Children in conflicting with the Laws” pamoja na adhabu zao ni tofauti na ule wa kesi za watu wazima. Chanzo Michuzi Blog.

Wednesday, May 23, 2012

Daktari aliyefanikisha kuuawa kwa Osama, ahukumiwa miaka 33 kwa Uhaini.


Dr. Afridi Shakeel
 
Daktari wa Pakistani ambae aliisaidia Marekani kubaini uwepo wa   Osama bin Laden nchini Pakistani amehukumiwa kifungo cha miaka 33 jela      kwa   kosa la       uhaini.

Dokta Afridi Shakeel alishitakiwa kwa kufanya kampeni bandia ya chanjo ya kusaidia CIA kupata sampuli ya DNA ya kiongozi wa al-Qaida na watu wa familia yake ili kuthibitisha uwepo wake katika katika mji huo wa Abbottabad, Pakistan.



Vikosi vya maalum vya Marekani vilimuua bin Laden wakati wa uvamizi uliyofanyika mwaka mwezi wa mei.

Maafisa wa serikali walisema kuwa mahakama ya kikabila iliyopo  kaskazini magharibi ya Pakistan Khyber ilimtia hatia Afridi kwa kosa la  uhaini. Mbali na kutumikia kifungo hicho cha  jela, daktari huyo pia atalazimika kulifaini ya $3,500.Maafisa wanasema kuwa chini ya mfumo wa kikabila, Afridi hakupewa haki ya kujitetea, au kupata mwanasheria.

Mapema mwaka huu, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta alisema Afridi alitoa msaada mkubwa sana katika kufuatilia uwepo wa bin Laden  nchini Pakistani hivyo kutoa wito kwa mamlaka ya Pakistan ya kumwachilia. Alisema Afridi angeweza kutoroka Pakistan kabla ya kukamatwa, lakini alichagua kukaa kwa sababu alikuwa na uzalendo.

Alipoulizwa kuhusu hukumu ya  Afridi wa, Msemaji wa Pentagon  George Little aliwaambia waandishi wa habari: " mtu yeyote ambaye amesaidia au kutiamkono Marekani katika kumtafuta Osama bin Laden hastaili kua na kosa kwa kua haikuwa kazi dhidi ya Pakistan bali Walikuwa wakifanya kazi dhidi ya al-Qaida.

Kifo cha Osama bin laden kwa namna moja au nyingine kimefifisha mahusiano ya kidemokrasia kati ya Marekani na Pakistani.

Tuesday, May 22, 2012

RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI WA RUFANI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama yaRufani.

Walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012.

Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000.

Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004