MKURUGENZI
Msaidizi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface
Makulilo (44) 'Jembe' amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali
ya Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini(DPP),
Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia kutokea kwa kifo hicho. Marehemu Boniface ameacha pengo kubwa sana kwa wanaasheria hasa waliojikita katika kesi za
jinai, kwa weredi wake mkubwa sana
wa kudadavua, na kuendesha mashauri mbalimbali ya jinai. Yumkini, weredi wake
huo ndio umepelekea mamia ya wanasheria na wadau mbalimbali kutoa maoni yao katika kurasa mbalimbali za kijamii” social networks”
kuonesha maoni yao kama
ifuatavyo:
MAONI YA WADAU:
Dr. Eliezer Feleshi , DPP
alisema bado ofisi yake na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji huyo
wa uendeshaji wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake
mzuri katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na
utaenziwa.
Moses Masinga, wakili msomi wa kujitegemea
aliandika facebook , so sad tuliokuwa wote Law School
nadhani mnamkumbuka jamaa alivyokuwa JEMBE! Aisee duniani tunapita tu. It is
not easy kuamini lakini habari ni hivyo.
Kheri Mbiro, wakili msomi wa kujitegemea aliandika katika ukurasa wake wa facebook,
Innocent Mhina mwanasheria na wakili wa bank ya posta aliandika;jamaa alikua exta ordinary attorney principles nyingi sana zimetoka kwenye cases alizo argue yeye na zingine kwa kuomba muongozo wa mahakama ususani kwenye ishu ya inquiry at subordinate crts at wht tme iwe conducted and how,.cheki kesi ya seleman abdalah v/s republic you will appreciate him and not only that alikua mwalimu mzuri sana.
Jerry Muro
WASIFU WAKE:
Boniface
alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahaha
ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka
2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa
rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama
Wakili wa Serikali, ilipofika Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa
Wakili wa Serikali Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na
kuwa Wakili Kiongozi wa Serikali.
Nyadhifa
ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai wake ni kati ya mwaka 2003-2007
alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Mbeya.Kati ya Mei 2007 na Oktoba
2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda ya Mwanza.Novemba 2009 hadi
Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake
mzuri ilipofika Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa
Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa
uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma.
KESI KUBWA ALIZOZIMAMIA;
Miongoni
mwa kesi kubwa ambazo mwandishi wa habari hizi amekuwa akimshuhudia
akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika mahakama mbalimbali hapa nchini
- sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8 katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka jana, iliwahukumu kwenda jela miaka mitano.
- kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka jana.
- kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara Jayankumar Patel "Jeetu Patel' na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.
- Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya mauji ya Ubungo Mataa ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7 inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Boniface mahali pema peponi.Amin.
No comments:
Post a Comment