JAJI
Mkuu wa Tanzania Chande Othaman amewaapisha na kuwatunuku leseni za kufanya
kazi mawakili wa kujitegemea 286 na kuwataka waende vijijini kuwasaidia
Watanzania.Kuapishwa
kwa mawakili hao wapya kunaongeza idadi ya mawakili kutoka elfu mbili mia tatu
kumi na sita waliokuwepo na kufikia elfu mbili mia sita na mbili.
Jopo la Mawakili Wakiwa katika sherehe ya kuapishwa kwao |
Akizungumza
na Waandishi wa habari baada ya kuwatunikia mawakili hao Jaji Chande alisema
ipo haja kwa mawakili hao kujikita kwenye maeneo ya pembezoni ambayo yana idadi
kubwa ya watanzania wenye mahitaji mengi ya kisheria.
Mdau lilian Kowero akitabasamu baada ya kuapishwa kua wakili msomi |
Aidha
alitoa wito kwa waliojiandikisha kuwa mawakili lakini hawajasajiliwa wafike
Baraza la Elimu ya Sheria liwasajili na hatimaye kuapishwa na kuwa mawakili
kamili hali itakayosaidia kuongeza idadi ya mawakili nchini.
Nao
baadhi ya mawakili walioapishwa Ijumaa hii walikiri kuwepo kwa changamoto
ya upungufu huo wa mawakili kwenye maeneo ya vijijini na kubainisha kuwa ipo
haja kujikita kwenye maeneo hayo.Kiapo
hicho ni sehemu ya mpango mkakati wa kupunguza changamoto ya upungufu wa
mawakili kutokana na kwamba idadi hiyo bado ni ndogo kulinganisha na mahitaji
ya watanzania ambao ni zaidi ya milioni 41.
No comments:
Post a Comment