MH. RAIS KIKWETE NA JAJI MKUU |
Mh. Tundu Lissu ambae pia ni waziri kivuli
wa sheria na Katiba, huenda akaburuzwa kwenyekwenye Kamati ya Maadili ya Bunge
kwa kwa kutoa maneno yenye mlengo wa dhihaka kwa Waheshimiwa Majaji wanaoteuliwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akichangia hatuba hio kama Msemaji wa kambi
ya upinzani kwenye masuala ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Tundu Lissu alitamka
maneno yenye mlengo wa dhihaka wa waheshimiwa hao wa Mahakama, ya kwamba baadhi
yao hawana uwezo na pia kumkosoa Raisi kwa uteuzi wake huo wa watu wasio na
uwezo.
ALICHOKISEMA
MWANASHERIA MKUU JUU YA KAULI ZA LISSU.
MWANASHERIA MKUU JAJI WEREMA |
Mh. Werema alisema, akiwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, ana wajibu kuwaelekeza wanasheria hasa waliopo bungeni, kufuata
misingi ya taaluma bila kuathiri haki yao wakiwa wabunge.“Nimefedheheka sana na
mambo mawili yaliyotokea bungeni,” alianza kusema kwa sauti iliyosikika kuwa
yenye huzuni, na kusema (mambo hayo) yamo kwenye hotuba ya Lissu.
Werema alisema baada ya Lissu kukosoa
uteuzi wa majaji huku akisema wengine hawana uwezo, alizungumza naye ili
kumuomba ayaondoe kwenye hotuba yake, lakini hakusema kama (Lissu) alikubali
ama kukataa.Alisema maneno hayo ambayo yapo ukurasa wa tisa ibara ya pili ya
hotuba hiyo, anaomba Lissu ayaondoe kabla ya kupitishwa bajeti ya wizara hiyo,
vinginevyo kiti cha Spika kimuamuru (Lissu) aambatanishe vielelezo vinavyothibitisha
maelezo yake.
Werema alisema Lissu ni mtaalamu wa sheria
asiyetakiwa kufedhehesha mahakama na majaji, lakini pia alikiuka kanuni za
Bunge kwa kuwataja watu wasiokuwa bungeni.Alitaja maeneo mengine yaliyomo
kwenye hotuba ya Lissu na ambayo yanastahili kuondolewa ni yaliyohusu kushamiri
kwa vitendo vya utekaji, utesaji na kudhuru watu, akitoa mfano wa Mbunge Kiwia,
Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea, Waziri wa Uchukuzi na Dk Harrison Mwakyembe.
Werema alisema vitendo hivyo na vile vya
umbakizaji kesi kwa raia wasiokuwa na hatia vilivyomo kwenye hotuba ya Lissu, havina
ukweli bali vinapotosha.Wakati akimalizia kutoa hoja yake, Werema alisema Lissu
anapaswa kutambua kwamba kuna Kamati ya Maadili ya Bunge na kwamba kuna
uwezekano `akaburuzwa’ huko kwa mujibu wa kanuni za Bunge.
Wakati Werema akizungumza, Lissu alisimama
kuomba mwongozo wa Spika, lakini Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, alimtaka
akae ili Mwanasheria Mkuu amalize kuwasilisha hoja.Lakini Mwanasheria Mkuu
alipomaliza kuzungumza, Mbunge Said Mkumba, alisimama kutumia ibara ya 68(7) ya
kanuni za Bunge na kutaka muongozo wa Spika kwa kile alichosema, Lissu amevunja
sehemu ya kiti anachokikalia bungeni.Baada ya Mkumba kuzungumza, Mhagama
alimuita Lissu ambaye alisimama na kusema mwenye mamlaka ya kumjibu Mkumba ni
kiti cha Spika, lakini Mhagama ‘alimgeuzia kibao’ na kumwambia amepoteza nafasi
ya kutaka muongozo.
WAZIRI
CHIKAWE ANENA
Waziri Katiba na Sheria, Mathias Chikawe,
alielezea kusikitishwa na kauli ya Lissu, akisema amesikitishwa na jinsi
lilivyosemwa hata kama palikuwa na hoja ya msingi.Alisema ibara ya 112 ya
Katiba inaunda Tume ya Mahakama ambayo inamshauri Rais wakati wote na kwamba
hakuna ukiukwaji wowote uliofanyika katika uteuzi wa majaji.
No comments:
Post a Comment