1.0 UTANGULIZI
Kwa miongo
mingi sana,
Mashauri mbalimbali katika Mahakama za Mwanzo yamekua yanaongozwa na Mahakimu
wasio wanasheria pamoja na wazee wa Baraza. Mawakili kama maofisa wa Mahakama
hawakupewa na nafasi kuwawakilisha wadaawa mbalimbali
katika Mahakama hizo za Mwanzo. Kimsingi
Waraka wa maendeleo ya UTUMISHI WA Umma Namba 1 wa mwaka 2010, umeondoa au
kufuta nafasi za Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na kuwaweka Mahakimu wakazi wa
Mahakama za Mwanzo.
Mabadiliko
haya kwa namna moja au nyingine yatapelekea kuwepo mabadiliko ya sheria , na
pengine kuakisi nafasi na umuhimu wa Mawakili na Wazee wa Baraza katika
Mahakama za Mwanzo nchini.
1.0
NAFASI NA
UMUHIMU WA MAWAKILI KATIKA MAHAKAMA ZA MWANZO
Baadhi ya Mawakili wapya walioapishwa Juzi |
Ibara ya 13(6)a ya Katiba ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, 1977 inaeleza ya Kwamba kila mtu ana haki ya
kusikilizwa, Haki ya kusikiliza kwa namna moja au nyingine huusisha haki ya
kuwakilishwa na Mawakili katika Mahakama za Mwanzo. Kimsingi wananchi wengi wamekua
wakiikosa haki hii muhimu, iliyowekwa kikatiba pia kutolewa Maamuzi mbalimbali kama mojawapo ya msingi wa “principles of natural
justice”. Wananchi wamekua wakiikosa
haki hii kutokana na mfumo na muundo wa Sheria zilizopo zinazowanyima Mawakili
nafasi za kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama hizo za Mwanzo kama
ilivyobainishwa katika Sheria ya
Mahakama Sura ya 11, Rejeo la Mwaka 2002.
Kuna na umuhimu mkubwa iwapo
mawakili watapewa nafasi kisheria kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama za
Mwanzo kama ifuatavyo;
a.
Kupunguza
mrundikano wa kesi Mahakamani, mawakili Kama
maofisa wana majukumu ya kisheria kuisaidia Mahakama kutoa Maamuzi ya Haki.
Iwapo pande za wadaawa zitawakilisha na Mawakili Mahakamani, yumkini mashauri
mengi yatamalizika mapema, hivyo kuondoa Mrundikano wa kesi usio na tija
Mahakamani.
b.
Kumalizika
Kwa Mashauri kwa Wakati, iwapo Mawakili watapata fursaya kuwawakilisha
wateja wao katika Mahakama za Mwanzo. Watawaongoza wadaawa au wateja wao kutatua
migogoro yao
kwa kutumia njia mbadala za kutatua migogoro hiyo yaani” Alternative Dispute
Resolution”.
c.
Wadaawa
kupata haki yao ya kuwakilishwa, kama
ilivyobainishwa hapo awali sio kila mtu ana uwezo wa kusimama mbele ya Mahakama
ya kujitetea. Iwapo Mawakili watapata fursa ya
kuwawalisha wateja wao hii itatoa fursa kwa wadaawa wao kupata ya kuwakilishwa ipasavyo katika mashauri
yanawayowakabili.
d.
Ajira, Kuanzishwa
kwa Shule ya Sheria Nchini” Law School of Tanzania”,
kwa namna ya pekee kumepelekea ongezeko kubwa la Mawakili nchini, wengi wa
mawakili hao ni Vijana wasio na fursa ya kuajiliwa Serikalini, au Taasisi
mbalimbali kutokana na ufinyu wa ajira Nchini. Hivyo basi nafasi hii itatua
fursa ya ajira kwa Mawakili wengi kuwawakilisha wateja wao hasa kwa wananchi
wengi walio vijijini ambapo kuna Mahakama Nyingi za Mwanzo.
2.0
NAFASI NA
UMUHIMU WA WAZEE WA BARAZA KATIKA MAHAKAMA ZA MWANZO.
wazee
wa Baraza wamekua Wakitumika si katika Mahakama za Mwanzo pekee Vilevile
Katika Mahakama Kuu, Wazee hawa wamekua
na Mchango mkubwa sana
katika kuisadia Mahakama Kutoa maamuzi ya haki.
Kifungu Cha 7(1) Cha Sheria ya Mahakama, Sura ya 11 ya Mwaka rejeo
la Mwaka 2002, Kinatoa akidi ya
Mahakama katika mwenendo wa Mashauri katika Mahakama za Mwanzo ya Kwamba
panatakiwa katika kila shauri pawepo na wazee wa baraza wasiopungua wawili.
Na
kwamba, maoni ya wazee wa katika Mahakama za Mwanzo ni ya Muhimu na lazima
yazingatiwe katika utaoaji wa maamuzi ya haki.
Na kwamba Mahakimu ni lazima wazingatie maoni ya Wazee hao wa baraza.
Swali
la kujiuliza ni kama iwapo Mawakili
wataruhusiwa kuwawakilisha wateja wao katika Mahakama za Mwanzo Je kuna ulazima
wa wazee wa Baraza kuendelea kuwepo?
Ni
rai yangu kwamba wazee wa Baraza Bado wanaumuhimu Mkubwa sana
kuendelea kuwepo( kama nitakavyoelezea hapo
baadae wapepo katika misingi gani). Kwa uchache umuhimu wa Wazee wa Baraza ni kama Ufuatao;
a.
Kwa kua Mahakama nyingi za Mwanzo zipo vijijini,
ambapo kuna kesi nyingi sana
za zinazohusisha mambo ya Kimila. Wazee wa Baraza ni muhimu hasa katika kuisadia
Mahakama Kupata tafsiri mbalimbali za Kimila hasa katika masuala ya Mirathi,
Ndoa na…Kwa Mfano katika jamii ya
kisukuma kuna faini ya “ Misango na
Ngweke” (hii ni faini ambayo anapewa kijana kwa ajili ya utorosha binti).
Uwepo wa wazee hawa kutasaidia sana
Mahakimu wa Mwanzo Wakazi katika masuala ya kimila ya Ndoa, Mirathi na madai.
3.0
MUUNDO WA
MAHAKAMA
Kwakua
Mahakama za wilaya na Hakimu Mkazi zina nguvu sawa katika usikilizaji wa
Mashauri ya mbalimbali hususan ya madai. Ni rai yangu kwamba hakuna haja ya
kuendelea kua na Mahakama 2 tofauti. Mahakama hizi zingeunganishwa na
kupatikana na Moja. Kwani kwa kawaida Rufani za , Mahakama hizi huenda Mahakama
Kuu. Kwa mantiki hii basi Muundo huu wa Mahakama shurti ubadilishwe.
4.0
MAPENDEKEZO
(NINI KIFANYIKE)
Ni
ukweli usiopingika Kwamba Mawakili na uwepo wa Wazee wa Baraza katika Mahakama
za Mwanzo nchini una maana kubwa katika kuziboresha Mahakama zetu, ili kutoa
maamuzi ya haki na kwa wakati. Ili kufanukisha
yote haya yafuatayo yanapaswa kuzingatia na kufanyika;
a.
Madadiliko ya Sheria, Vifungu
mbalimbali vya kisheria ni lazimavibadilike katika mantiki ya kuwawezesha
Mawakili kuhudhuria Mashauri ya Mahakama za Mwanzo kama
ifuatavyo;
i. Kifungu cha 33(1)
kinachowazuia Mawakili kutowawakilisha wateja wao katika Mahakama za Mwanzo
kirekebishwe kutoa Mwanya kwa Mawakili hao kua na fursa hiyo.
ii. Kifungu cha 7(1) Cha Sheria Ya Mahakama, Sura
ya 11,Rjeo la Mwaka 2002 kinachosema; in every proceeding in Primary Court,
including a finding, the Court shall not sit with not less than two assessors.
Ni
rai yangu kwamba kwa majukumu ya wazee wa baraza yawe kwenye kesi za madai
pekee wa wasipewe nafasi katika kesi ya Jinai kama
ambayo Kifungi tajwa hapo juu kinavyobainisha” in ever proceeding” mabadiliko yafanyike ili kuwe na ukomo kwenye
mashauri ya jinai yaani” in Civil
proceedings in Primary…..” Hii ni kwakua wazee hawa hawana weredi wa makosa
mbalimbali ya kisheria.
b.
Maoni ya
wazee wa Baraza, kwa hali ilivyo hivi sasa maamuzi ya Mahakama ya
Mwanzo yanategemea maoni ya Wazee Wa Baraza. Sheria ibadilishwe ili maoni haya
ya wazee wa Baraza yewe” not binding”
ili kulinda na kuakisi dhana nzima ya uhuru wa Mahakama” Independence of Judiciary”.
c.
Miundombinu
ya Mahakama za Mwanzo; Mahakama nyingi za Mwanzo zipo vijijini vikiwa
na Miundo mbinu mibovu sana,
majengo yaliyochakaa hivyo haitokua busara kwa Mahakimu Wakazi tarajiwa wa
Mahakama hizo kufanya kazi katika Mazingira haya. Ni rai yangu kwamba za juhudi
za hali na mali
zifanyike kuboresha mazingira haya ya Mahakama hizi.
d.
Lugha ya
Mahakama; Kwa hali ilivyo hivi sasa Mashauri ya Mahakama ya Mwanzo
yanaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili. Iwapo Mawakili wataruhusiwa kuingia katika
Mahakama hizi basi Lugha ya kiingereza itumike kama
Mbadala wa Lugha ya Kiswahili. Hivyo basi kifungu cha 13(1) Cha Sheria ya
Mahakama, Sura ya 11 rejeo la mwaka 2002 kinachosemeka “the language of primary Court shall be in Kiswahili”.
5.0
HITIMISHO
Ni
Rai yangu kwamba nafasi ya Mawakili katika utoaji wa maamuzi ni mkubwa sana, Sheria Zetu
zibadilishwe ili kuakisi hali halisi ya mabadiliko haya.
No comments:
Post a Comment