Powered By Blogger

Tuesday, July 17, 2012

MBUNGE"MTUHUMIWA WA RUSHWA" ASOMEWA MAELEZO YAKE.



Mh. Badwel akiwa akiwa na Maofisa wa Polisi


MBUNGE wa Bahi, mkoani Dodoma, Bw. Omary Badwel (CCM), anayekabiliwa na kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya sh. milioni moja, amedai Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Bi. Sipora Liana, ameshindwa kuonesha ushirikiano kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), kama wanavyofanya wenzie.


Mbele ya Hakimu Bw. Faisal Kahamba, wakili wa Serikali kutoka Taasisi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bi. Janeth Machullya, alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakati akimsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali.

Bi. Machullya alidai kuwa, mshtakiwa alitoa aneno hayo kwa Bi. Liana walipokutana katika Hotel ya Peacock, baada ya kumpigia simu kwa ahadi ya kumpa ujumbe muhimu.

Alidai Bw. Badwel alimwambia Bi. Liana kuwa, Wakurugenzi wenzake huwa wanatoa kiasi cha fedha kwa wajumbe wa kamati hiyo kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa mahesabu katika Wilaya zao kabla kamati haijaenda kufanya ukaguzi.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo anatakiwa kutoa sh. milioni nane kwa kamati hiyo ili kila mjumbe apate sh. milioni moja ambapo Bi. Liana alimjibu kuwa, wakati huo hakuwa na kiasi hicho ila anaweza kwenda ATM na kumpatia sh. milioni moja.

Baada ya kumueleza hayo, Bw. Badwel alichukuwa karamu, karatasi na kuandika namba yake ya akaunti katika Benki ya NMB ambayo ni 5051602671, kumpa Bi. Liana na kumueleza fedha ambazo zitakazobaki, aziingine katika akaunti hiyo kabla ya kikao cha kamati Juni 4 mwaka huu.

Walipomaliza mazungumzo hayo, mshtakiwa alimruhusu Bi. Liama akatowe hizo fedha na baada ya muda, alirudi nazo kwenye bahasha ambazo ni noti za sh. 10,000 na Bw. Badwel alizipokea na kuziweka pembeni mwa sahani yake ya chakula pamoja na simu.

Ilidaiwa kuwa, baada ya hapo Bi. Liana aliondoka ndipo mshtakiwa alikamatwa na Maofisa wa TAKUKURU, kwa kukutwa na rushwa ya sh. milioni moja na kuomba sh. milioni nane.

Baada ya maofisa wa taasisi hiyo kuzikagua fedha hizo, walikuta nyingine zikiwa zinafanana namba na zile wanazotumia wao kwa ajili ya mitego.

Katika maelezo hayo, ilidaiwa LAAC ilipangiwa kufanya ukaguzi wa hesabu katika Wilaya ya Bagamoyo na Mkuranga ambapo Bw. Badwel alimpigia simu Bi. Liana kwa mara ya kwanza Mei 30 mwaka huu, kupitia namba 0784858255 na kujitambulisha kwake.

Katika mawasiliano yao, Bw. Badwel alimwambia Bi. Liana kuwa ana ujumbe wake kutoka kamati ya LAAC, hivyo anataka wakutane haraka kabla ya Juni 4 mwaka huu ili ampatie ambapo mambo si shwari katika kamati hiyo.

Juni mosi mwaka huu, Bw. Badwel alipiga simu kwa mara nyingine bila kueleza ujumbe huo unahusu nini zaidi ya kusisitiza wakutane ndipo Juni Juni 2 mwaka huu, walipokutana katika hoteli hiyo,  upande wa Kasuku Bar.

Katika kesi hiyo, Bw.Badwel anadaiwa kuomba rushwa ya sh milioni nane, kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bi. Sipora Liana.

Ilidaiwa kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Mei 30 na Juni 2, 2012, katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa anadaiwa Juni 2, 2012 katika hoteli ya Peacock, Dar es Salaam, akipokea rushwa ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mshtakiwa ambaye ni mjumbe wa LAAC, aliomba kiasi hicho cha fedha ili kuwashawishi wajumbe wa kamati hiyo waweze kupitisha taarifa ya fedha ya mwaka 2011/2012.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi. Upande wa mashtaka umedai kuwa na na mashahidi 16 na vielelezo mbalimbali. Chanzo gazeti la Majira.

WAZIRI NA MWANASHERIA WATISHIWA KUUAWA.


Dr. Huvisa

SERIKALI imepata hasara ya sh. milioni 50 katika utekelezaji wa bomoa bomoa kwa wakazi waliojenga ndani ya hifadhi ya bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach na Kawe, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa, aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bomoa bomoa ambayo ilifanyika Julai 10 mwaka huu katika maeneo hayo na kusisitiza kuwa, Serikali itawadai wote waliobomolewa nyumba zao ili kurejesha gharama zilizotumika.


Alisema mbali ya kufanikisha bomoa bomoa hiyo, amepokea vitisho vya kuuwawa na watu wasiofahamika kupitia simu yake ya mkononi kama ataendelea na mpango huo.

Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi za Mazingira (NEMC), Bw. Heche Manchare, nae alikumbana na vitisho vya kuuawa ambapo taarifa hizo zimeripotiwa polisi.

“Sheria ya mazingira inatamka wazi kuwa, gharama zinazotokana na hatua mbalimbali za kuondoa tatizo la kimazingira, zitarejeshwa na watuhumiwa waliosababisha tatizo husika.


“Kimsingi mimi sitishiki na vitisho hivi, Serikali itaendelea  kusimamia sheria ya mazingira na haitamvumilia mtu, watu au kikundi kinachotishia watumishi wa Serikali ambao wanatekeleza kazi za usimamizi wa sheria za nchi.

“Endapo watagundulika, hatua kali dhidi yao zitachukuliwa, tukumbuke kuwa Serikali imeazimia kukabiliana na tatizo hili ambalo ni kubwa hasa wakati huu tunapokumbwa na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Dkt. Huvisa.

Aliongeza kuwa, gharama hizo ni kubwa lakini kama wananchi watafuata sheria zitaepukwa na uzingatiaji sheria na taratibu za nchi uwe wajibu wa kila mwananchi ili kuepuka hasara inayotokea Serikali inapoamua kutumia nguvu kutekeleza sheria.

Dkt. Huvisa alisema bomoa bomoa hiyo ilifanywa na ofisi yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Manispaa ya Kinondoni na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambapo polisi walihusika kuimarisha ulinzi katika utekelezaji.

Alisema ubomoaji huo ni utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ambapo nyumba 17 zilibomolewa yakiwemo majengo ambayo ujenzi wake ulikuwa ukiendelea katika mkondo wa mto.

“Lengo la kufanya hivi ni kuiepusha jamii na madhara yatokanayo na mafuriko ya mara kwa mara, fukwe, mito na vijito vinatakiwa kuwa wazi ili maji ya mvua yaweze kupita kwa wingi kama iliyonyesha Desemba 2011.

“Mvua hii ilisababisha vifo na uharibifu mali katika Bonde la Msimbazi, vitendo vya kuzuia mikondo ya maji, kuipindisha, kuichepusha au kuifinya upana wake kwa kujaza kifusi ni makosa chini ya Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004,” alisema.

Hata hivyo, Dkt. Huvisa aliwataka wote waliojenga au kuendelea na ujenzi katika maeneo yenye vyanzo vya maji, kando ya bahari, maziwa, mito, mabwawa na misitu inayolindwa kisheria kuondoka mara moja na wale ambao watakiuka agizo hilo, hatua za kisheria zitachukuliwa, kubomolewa nyumba, kuondolewa katika maeneo hayo na kulipia gharama zote za ubomoaji.

“Agizo hili pia linawahusu wakulima na wafugaji wanaofanya shughuli zao katika vyanzo vya maji,” alisema Dkt. Huvisa na kusisitiza kuwa, baada ya Bunge kazi hiyo itaendelea katika mikoa yote ya Tanzania ili kusimamia sheria husika.

Pia Dkt. Huvisa alitolea ufafanuzi wa nyumba iliyojengwa kwenye kiwanja namba 2019/2020 na kudai kuwa, Wizara yake imepokea zuio la Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na zuio la kuivunja.

“Hata hivyo, hakuna mamlaka yoyote ya Serikali iliyotoa kibali kwa ujenzi huo hivyo hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kesi kuamuliwa na imepangwa Septemba 20 mwaka huu,” alisema.Chanzo gazeti la Majira.

Saturday, July 14, 2012

MAMBO 8 MAZURI KWENYE BAJETI YA WIZARA SHERIA 2012/2013






1.     Serikali iliasaidiana na Mahakama itaanzisha mahakama kuu za wilayani Temeke, Ilala na Kinondoni. Wilaya hizo tatu zitakua kama Mikoa Kimahakama.
2.    Kesi kusikilizwa na kuendeshwa kwa njia ya Mtandao”Tele justice”. Utaratibu huu haumlazimu mshitakiwa au mdaawa wa kesi kufika Mahakamani. Kesi ya Prof.Mahalu ilitumia utaratibu huu.
3.    Serikali ilisaidiana na Mahakama itaajiri Majaji na Mahakimu wa muda” Temporally Judicial Officers”. Kwa kipindi cha miezi 12 ili kupunguza mrundikana mkubwa wa kesi uliopo hivi sasa.
4.    Serikali huenda ikaanzisha Mahakama kuu ya Jinai, itakayokua na mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai pekee kama ilivyo hivi sasa kwenye kesi ya kikatiba na kazi.hii itaondoa utaratibu wa hivi sasa wa baadhi ya kesi za jinai kusikilizwa kwenye vikao maalum vya kimahakama katika kesi za jinai(Criminal Court sessions).
5.    Serikali inakusudia kuandaa na kuleta muswada mpya wa sheria ya uhuru wa Habari utakaokua na viwango vya Kimataifa.
6.    Serikali imeanzisha kupitia kwa Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali kupita magerezani,kuangalia na kuwaondolea wafungwa walio na kesi zisizo na kichwa wala miguu. Baadhi wa wafungwa wameshanufaika na utaratibu huu.
7.    Mahakama ya Kadhi huenda ikapatikana kwani Serikali bado inamalizia majadiliano na wadau wa Mahakama hiyo. Mahakama hiyo iwapo itaanzishwa iakua na mamalaka ya kusikiliza kesi za mirathi, ndoa na talaka.
8.    Mchakato wa Kupata Katiba mpya huenda ukazaa matunda wakati wa sherehe ya miaka 50 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar hapo tarehe 26.04.2014.

KESI SASA KUENDESHWA KWA MTANDAO.

Mh. Mathias Chikawe
Waziri wa sharia na Katiba, Mheshimiwa Mathias Chikawe akiwasilisha bungeni mipango na makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2012-2013 amesema serikali kwa Kushirikiana na muhimili wa Mahakama utaanzisha mpango utakaojulikana kama”Tele Justice”, au utaratibu wa kusikutoa kiliza kesi na  haki kwa njia ya Tehama ili kutoa haki hapa nchini na kupunguza gharama kubwa zinazotokana na utaratibu wa sasa.
Mpango huu ambao umezoeleka kwenye nchi zilizoendelea, utaunganishwa magerezani na mahakamani hivyo  utawezesha  kesi kusilikizwa bila ya mtuhumiwa kutolewa gerezani na kupelekwa Mahakamani.

Mh chikawe alisema ya kwamba” utaratibu huu utamuwezesha Jaji au hakimu kusikiliza kesi bila mtuhumiwa kupelekwa Mahakamani, Kwa sasa tunafanya uchambuzi tuanze gereza lipi na Mahakama zipi, ili utekelezaji uanze rasmi kwa mwaka wa fedha 2012-2013”. Mheshimiwa huyo alisema haoni kama itakua shida kwa Mahakama kufanikiwa katika mfumo huo kwani hata Sekta ya mawasiliano hapo zamani ilikua duni sana mpaka kufikia matumizi ya simu za viganjani zinazotumika hivi sasa.

Sanjali na hayo Mh.Chikawe alisema kwamba Mwaka huu wa fedha Serikali inakusudia kuajili Majaji na Mahakimu wa Muda watakaoshughulikia mrundikano wa kesi uliopo hivi sasa. Majaji hao na Mahakimu wataajiriwa kwa Mkataba wa miezi 12 ili kupunguza mashauri takribani (199,741) ambazo bado hazijamalizika.