1. Serikali iliasaidiana na Mahakama
itaanzisha mahakama kuu za wilayani Temeke, Ilala na Kinondoni. Wilaya hizo
tatu zitakua kama Mikoa Kimahakama.
2. Kesi kusikilizwa na kuendeshwa kwa njia ya
Mtandao”Tele justice”. Utaratibu huu haumlazimu mshitakiwa au mdaawa wa kesi
kufika Mahakamani. Kesi ya Prof.Mahalu ilitumia utaratibu huu.
3. Serikali ilisaidiana na Mahakama itaajiri
Majaji na Mahakimu wa muda” Temporally Judicial Officers”. Kwa kipindi cha
miezi 12 ili kupunguza mrundikana mkubwa wa kesi uliopo hivi sasa.
4. Serikali huenda ikaanzisha Mahakama kuu ya
Jinai, itakayokua na mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai pekee kama ilivyo hivi
sasa kwenye kesi ya kikatiba na kazi.hii itaondoa utaratibu wa hivi sasa wa
baadhi ya kesi za jinai kusikilizwa kwenye vikao maalum vya kimahakama katika
kesi za jinai(Criminal Court sessions).
5. Serikali inakusudia kuandaa na kuleta
muswada mpya wa sheria ya uhuru wa Habari utakaokua na viwango vya Kimataifa.
6. Serikali imeanzisha kupitia kwa Ofisi ya
Mwanasheria mkuu wa serikali kupita magerezani,kuangalia na kuwaondolea wafungwa
walio na kesi zisizo na kichwa wala miguu. Baadhi wa wafungwa wameshanufaika na
utaratibu huu.
7. Mahakama ya Kadhi huenda ikapatikana kwani
Serikali bado inamalizia majadiliano na wadau wa Mahakama hiyo. Mahakama hiyo
iwapo itaanzishwa iakua na mamalaka ya kusikiliza kesi za mirathi, ndoa na
talaka.
8. Mchakato wa Kupata Katiba mpya huenda
ukazaa matunda wakati wa sherehe ya miaka 50 ya Muungano kati ya Tanganyika na
Zanzibar hapo tarehe 26.04.2014.
No comments:
Post a Comment