Mh. Mathias Chikawe |
Waziri wa sharia na Katiba, Mheshimiwa
Mathias Chikawe akiwasilisha bungeni mipango na makadirio na matumizi ya fedha
ya wizara yake kwa mwaka 2012-2013 amesema serikali kwa Kushirikiana na
muhimili wa Mahakama utaanzisha mpango utakaojulikana kama”Tele Justice”, au
utaratibu wa kusikutoa kiliza kesi na haki kwa njia ya Tehama ili kutoa haki hapa
nchini na kupunguza gharama kubwa zinazotokana na utaratibu wa sasa.
Mpango huu ambao umezoeleka kwenye nchi
zilizoendelea, utaunganishwa magerezani na mahakamani hivyo utawezesha
kesi kusilikizwa bila ya mtuhumiwa kutolewa gerezani na kupelekwa
Mahakamani.
Mh chikawe alisema ya kwamba” utaratibu huu
utamuwezesha Jaji au hakimu kusikiliza kesi bila mtuhumiwa kupelekwa Mahakamani,
Kwa sasa tunafanya uchambuzi tuanze gereza lipi na Mahakama zipi, ili
utekelezaji uanze rasmi kwa mwaka wa fedha 2012-2013”. Mheshimiwa huyo alisema
haoni kama itakua shida kwa Mahakama kufanikiwa katika mfumo huo kwani hata
Sekta ya mawasiliano hapo zamani ilikua duni sana mpaka kufikia matumizi ya
simu za viganjani zinazotumika hivi sasa.
Sanjali na hayo Mh.Chikawe alisema kwamba
Mwaka huu wa fedha Serikali inakusudia kuajili Majaji na Mahakimu wa Muda
watakaoshughulikia mrundikano wa kesi uliopo hivi sasa. Majaji hao na Mahakimu
wataajiriwa kwa Mkataba wa miezi 12 ili kupunguza mashauri takribani (199,741)
ambazo bado hazijamalizika.
No comments:
Post a Comment