Bi. Nancy Baraza |
Jopo maalum la majaji
lililoteuliwa na rais Mwai Kibaki kuchunguza tuhuma zilizokuwa zinamkabili
Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza kumdhalilisha mlinzi mmoja katika duka
moja kubwa mjini Nairobi, imependekeza, jaji huyo kuondolewa madarakani.
Akisoma hukumu hiyo mjini Nairobi
leo, mwenyekiti wa jopo hilo, Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Augustino
Ramadhan, amesema Nancy Baraza akiwa mtumishi wa chombo cha kusimamia sheria na
haki hakutakiwa kwa namna yoyote kutenda kosa hilo dhidi ya mlalamikaji Bi Rebecca
Kerubo.
Amesema kitendo alichofanya Nancy
Baraza na ni cha utomvu mkubwa wa nidhamu na hivyo kupendekeza kwa Rais Mwai
Kibaki kumwondoa katika wadhifa wake wa naibu jaji mkuu.
Nancy Baraza alituhumiwa
kumnyanyasa na kumpiga Bi Kerubo tarehe 31 Desemba 2011, baada ya kutakiwa
kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuingia katika duka hilo, utaratibu ambao umekuwa
ukitekelezwa kwa wateja wote.
No comments:
Post a Comment