Saif al- Islam |
Mtoto wa marehemu Ghadafi Saif al-Islam alisema iwapo kesi yake itaendeshwa Libya basi inakuwa
sawa na kuuawa, kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakama ya ICC(International Criminal Court).Kijana
huyo mwenye umri wa miaka 40 anashikiliwa na wapiganaji mjini Zintan. Amekuwa
akishikiliwa Libya tangu Novemba 2011Alishtakiwa na ICC kwa uhalifu dhidi ya
ubinadamu.
Serikali
ya mpito ya Libya mpaka sasa imekataa kumkabidhi Saif Uholanzi ambako mahakama
ya ICC iko ikisema kuwa hana budi kukabiliana na mashataka yake nchini Libya.Kanali
Gaddafi, ambaye utawala wake wa kidikteta ulidumu kwa miaka 42 aliuawa katika
mazingira ya kutatanisha baada ya kukamatwa na waasi mwezi Octoba, katika
kitendo ambacho kilishutumiwa vikali na makundi ya haki za binadamu.
'Ulinzi wa bandia'
"Siogopi
kufa lakini ikiwa itaendeshwa hapa hiyo muuite tu kuwa ni uuaji na
mmalizane," Saif al-Islam alinukuliwa na mawakili akisema.Mwezi Juni,
wafanyakazi waliotumwa na ICC walikamatwa baada ya kukutana na Saif al-Islam,
na kushikiliwa kwa zaidi ya wiki tatu.Nyaraka zilizowasilishwa mahakamani
zinasema wakati wa mkutano huo afisa aliyejifanya mlinzi alimzuia mwanasheria
wa ICC kuchukua kiapo kutoka kwa Saif al-Islam.
"Mlinzi
huyo ambaye kimsingi ni Bw Ahmed Amer – mwanasheria anayezungumza lugha kadhaa
alijumuishwa kwenye timu hiyo makusudi kuwalaghai " nyaraka ziliandika,
kwa mujibu wa Reuters."Alirejea chumbani na (mkalimani wa ICC akiwepo)
alianza kupiga kelele kuwa maelezo hayo yalikuwa hatari sana, yamekiuka usalama
wa Libya na kwa Ulinzi wasingeyarudisha"Mkutano ulistishwa baada ya dakika
45 na nyaraka zao kuharibiwa, wakili alisema. Baadaye walikamatwa.
Hatua
hiyo ilionekana kuwa "kimyume cha sharia, uhaini na ukiukwaji wa taratibu
za usalama wa Taifa kwa ama Bw Gaddafi au washauri wake na kuonyesha kuwa
Gaddafi hataki kesi yake iendeshwe na mahakama za Libya." Walisema
mawakili kwenye nyaraka.
Maafisa
wa Libya walimshutumu wakili Melinda Taylor, aliyekuwa akiongoza ujumbe wa ICC,
kwa kuwa na vifaa vya upelelezi vikiwa vimeshikizwa kwenye barua ya Saif
al-Islam wakati wa mkutano.
No comments:
Post a Comment