Picha ya Maktaba: Wafanyakazi wakiwa kazini |
Wafanyakazi
wa Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine(GGM) wamegoma kufanya kazi sababu kuu
ikiwa kupinga sheria ya mafao ya kujitoa
inayowanyiwa wafanyakazi fursa ya kuchukua malipo hayo wanapoacha kazi hadi
pale watakapofikisha umri wa kustaafu. Hali
hiyo ilimlazimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uzimamizi na udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA)Bwana Afrikanus Mushi kuzungumza na wafanyakazi hao kwa
takriban masaa matatu na kuwaomba warejee kazini, mpaka mamlaka hiyo itakapotoa
na kufanya upembuzi yakinifu baada ya mwezi mmoja.
Wafanyakazi kusubiri kama mzee huyu ili wapate mafao |
Kauli hii
ya Mkurugenzi Huyo wa inakuja baada ya Mamlaka hiyo kupitia katika kitengo
chake cha mawasiliano na uhamasishaji kutoa taarifa kwa umma kwamba “Kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria
hiyo maombi mapya ya kujitoa
yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili
kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii kutoa elimu kwa wadau”. Haileweki kama kikao hicho cha Mkurugenzi Mkuu
na Wafanyakazi wa GGM, kutabadilisha hali hiyo ndani ya kipindi kifupi cha
Mwezi mmoja.
Wakati huo
huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii(facebook, twitter na blogs mbalimbali)
wadau wa mitandao hiyo wametoa maoni yao kama ifuatavyo:
Stanslaus Nyambea aliandika: Sheria
Kandamizi ya Mafao ya kuacha kazi kabla ya kustaafu yapitishwa Tanzania.Sheria
ina mapungufu makubwa ya kisheria:
1. Ina viashiria vya kibaguzi vya waziwazi,
yaani mfuko wa hifadhi wa wabunge unasema wanapewa mafao soon after bunge
likifa. Kwanini na wao wasiwekewe limit ya miaka 55?-Ubaguzi huu!
Pili, inalazamisha na kuamua matumizi ya mtu
binafsi, eti mkopo wa nyumba kwa watu hawa utatolewe na mfuko, wakati hata
ukiisha miaka 1000, hutaweza kulipa. Mosi, Kijamii hii sheria ni ya kupuuzi
sana; mosi inashau sisi tulioko kwenye sekta binafsi ajira zetu ni za muda.wengi
tunajiandaa kwenda kusoma kutumia hizo hela za mafao.
Kisiasa, tunajua kuwa
serikali yetu ni mfilisi, haina fedha kwakuwa zinaibwa, hivyo njia pekee ni
kuiba fedha zetu za mifuko ya hifadhi kujenga barabara, majengo na kutimiza
ahadi za kipuuzi za rai.
Novatus Rukwago aliandika: “Hapa kuna maswali machache makubwa ya msingi
ya kujiuliza hat kama hatujaanza kutafuta tufanye nini. Hivi hii imepitishwa na
nani? 2. Kama ni wabunge tunaowaita wawakilishi wetu, wamefanya hivyo kwa
maslahi ya nani?. 3. Je Rais ameshaisain au la. Kama bado, je amesikia kilio
cha wnanchi wake? Na kama tayari je alijua alichosain?. Tukipata majibu sahihi
ndo tuulizane tufanye maamuzi kwaajili ya leo na kwaajili ya kesho. Mungu
atunusuru na msiba huu”
Mwingine alisema’ Hiyo Miongozo HATUITAKI.. Mtushirikishe
kwenye Miongozo wakati wa KUTUNGA sheria ambayo inatuhusu sisi wenyewe
wafanyakazi Hamkutushirikisha why NOW matake kutushirikisha kwenye MIONGOZO?
Non Sense kabisa, Hivi wewe mtu amefanya kazi miezi mitatu na kibarua kikaisha
na mtu alikuwa analipwa 120,000 Hiyo NSSF yake unajua ni how Much?mpka
aisubirie kwa mpk afike miaka 60 na ajira zenyewe hizi za kubangaiza ambazo
serikali inaangalia tu wanapewa wageni wazawa tunaachwa unategemea hizi siku
zote anaishi vipi? hiyo sheria nafikiri inaweza fanayakazi serikalini ambako
watu huwa hawafukuzwi kazi, Kazi inaisha siku anastaafu akiwa na hiyo miaka 60,
sisi wa sekta Binafsi Mnatuonea tu, Vimishara venyewe ndo hivyo vya tia maji
tia maji, leo hii nimeachishwa kazi nina Miaka 30 ndo ni wait tena 30 years
nipewe Hifadhi yangu KWELI? Are you Serious?Please msiwe kama watoto. Hata hii
Mamlaka kweli inawatu wenye HEKIMA na BUSARA kweli?Nahisi ni mradi tu wa Mtu,
Hiyo mifuko ya jamii yenyewe inapiga Deal kinoma na Hela zetu lakini hatupewi
Share kwenye hiyo Miradi wala Riba!Basi wangekuwa hata wanatudanganyishia
kutuwekea mdhamana kwenye Mabenki tuwe twapata Mikopo ya Kununua Nyumba za NHC
au hata Kupewa Mikopo, As I know kuwa Hii mifuko ya Jamii ina weka Hela zetu
kwenye Mabenki kwa FIX deposit accounts..Tunajua yote wanayofanya tuka kaa
Kimya NOW ndio mnataka hata hichi kidogo tusikipate,Please Kuweni Serious”.
No comments:
Post a Comment