Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kutoa ufafanuzi juu ya mafao ya
kujitoa. Ufanunuzi huu unakwenda
sambamba na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya
habari na kuleta mkanganyiko miongoni mwa Wanachama na Wadau wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii.
Kufuatia
hali hiyo Mamlaka inatoa ufafanuzi ufuatao:
Marekebisho kuhusu
kusitisha fao la kujitoa
yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya Hifadhi ya Jamii ambayo
ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha
kumudu hali ya maisha uzeeni.
Ni kweli kuwa Sheria za Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho. Mchakato
wa marekebisho hayo ulihusisha wadau kwa kuzingatia utatu yaani wawakilishi
kutoka vyama vya wafanyakazi, Chama cha
waajiri pamoja na Serikali.
Kwa kutambua tofauti ya ajira, tofauti ya mazingira ya
kazi, tofauti ya sababu za ukomo wa
ajira, na umuhimu wa Mwanachama
kunufaika na michango yake wakati angali katika ajira, Mamlaka inaendelea na mchakato wa
kuandaa miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama. Miongozo na kanuni hizo zitajadiliwa na wadau
wakiwemo wafanyakazi, waajiri na
Serikali kabla ya kuanza kutumika.
Kufuatia kuanza kutumika kwa
Sheria hiyo maombi mapya ya kujitoa
yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili
kuiwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii kutoa elimu kwa wadau.
Tangazo hili halitowahusu
wanachama waliojitoa kabla ya tarehe
20/07/2012.
Mamlaka inakanusha vikali
kwamba sitisho la fao la kujitoa si kwasababu za kiserikali au kwasababu mifuko
imefilisika. Tunapenda kuwahakikishia kwamba Mifuko yote ipo thabiti na michango yote ya wanachama ipo salama.
Hivyo, Mamlaka inawaomba
wanachama na wadau wote wa sekta ya
Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa lengo ya kulinda na kutetea maslahi ya
mwanachama.
Imetolewa na kitengo cha
Mawasiliano na Uhamasishaji
SSRA-Makao Makuu
No comments:
Post a Comment