Siku chache zilizopita Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliteua Baraza lake
la mawaziri.Baraza hilo limekuja baadbaadhi ya mawaziri,
kushutumiwa kwa utendaji mbovu wa shughuli zao na kila siku na kutumia mamlaka
yao aidha kujinufaisha au kufisadi mali ya Umma. Kimsingi,lengo langu si
kudadisi kwa kina sababu zilizopelekea Mh.Rais kufanya mabadiliko hayo.
Nimehamasika kuandika suala hili baada ya vyombo mbalimbali vya habari,
wanazuoni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kua namaoni tofauti, wengine
wakienda mbali sana na kusema Rais amevunja kaika kwa kuwachagua baadhi ya
Mawaziri kushika wadhifa huo wakati wao si wabunge. Niseme kwamba katika maoni yangu hayo nitarejerea Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(1977), kama "Katiba".
Kimsingi,
nikiwa Mwanasheria nimeona si vibaya nikitoa mawazo yangu katika mkanganyiko
huu ambapo jamii isiyo na uelewa wa kisheria” layman”, huweza kukumbwa na
mkanganyiko usiostahili katika jambo hili. Mfano katika gazeti la mtanzania la
leo Jumapili, lilimnukuu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(
CHADEMA) likiwa na kichwa cha habari” MBOWE AMSHUKIA JK, ADAI AMEVUNJA KATIBA
UTEUZI WA MAWAZIRI”. Katika gazeti hilo lenye namba. ISSN 0856-5678 Toleo Na.
6049, gazeti hilo lilimnukuu Mh.Mbowe akisema mafuatayo,” inasikitisha Kuona Rais
anaendesha nchi kihuni na kuvunja kwa makusudi Katiba,wakati akifahamu kuwa
hawezi kumpa mtu uwaziri bila kuapishwa ubunge na kwamba kwa hatua hiyo Rais
Kikwete ameridharau bunge.
Niaze
kueleza kwamba Ibara ya 66(1) e kinatoa Mamlaka ya Kikatiba kwa Rais kuteua
wabunge wasiozidi 10 wenye sifa atakazoona inafaa kuitumikia nafasi hiyo,
sanjali na mamlaka hayo aliyopewa Rais aina nyingine ya mtu kuwa Mbunge pia
zinaainishwa katika Ibara hiyo hiyo; na kwamba mtu anaweza kua mbunge kwa
kuchaguliwa na wananchi au vilevile kupitia kwa viti maalum, ay nafasi aliyonayo
kama ya Mwanzaasheria Mkuu wa Serikali.
Hivyo basi Uteuzi wa Rais kwa Prof. Sospether Muhongo na Bi.Jane kuwa
wabunge na hatimaye uwaziri ni uteuzi wa kikatiba.
Watu
wanaosema Raisi amevunja katiba, wanamaoni ya kwamba wabunge walioteuliwa na
Rais kuwa mawaziri hawajaapa kuwa wabunge
kabla ya kushika na Kuteuliwa na Raisi kuwa Mawaziri. Nina wiwa kusema ya
Kwamba huu ni upotoshwaji mkubwa na pengine
uelewa mdogo wa Katiba pamoja na Sheria za nchi yetu.
Kimsingi
Swali la kutuongoza ni kwamba, ni wakati
gani mtu anakua Mbunge? Je ni pale mtu anapotangazwa na Tume kuwa Mbunge ?AU Je ni
Pale ambapo mtu anapoteuliwa na mtu mwenye mamlaka kuwa Mbunge? Au Je ni pale
mtu anapokua kiapo cha Ubunge? Ni rai yangu kwamba Sura ya 343 iliyofanywa
marekebisho mwaka 2002 na 2010 ,kifungu cha 98 kinasema mtu anakua mbunge pale
baada ya kutangazwa na Tume ya uchaguzi kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuwa mbunge
kupitia Jimbo husika, au pale mtu anapoteuliwa kwa mujibu wa Katiba kushika
wadhifa huo(Kama ambavyo Rais amefanya katika Ibara ya 66(1)e). Suala la kwamba
mtu huyo amekula kiapo cha kutumikia wadhifa huo wa ubunge au la! Hilo ni suala
jingine. Na kuapa au kutokuapa kwa mtu huyo hakumuondolei ubunge wake( does
neither disqualify him or her from holding that post nor invalidate the same).
Ninachomaanisha ni kwamba Mtu anapotangazwa au kuteuliwa kuwa mbunge, mtu huyo
atahesabika kuwa mbunge pale tu atakapotangazwa au kuteuliwa kushika wadhifa
huo. Kwa Mfano. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni Mbunge Kikatiba kwa nafasi
aliyonayo yeye kama Mwanasheria Mkuu katika Ibara ya 66(1)d na 55(5). Kama Rais
akiingia Madarakani na Kumteua Mwanasheria Mkuu wa serikali, Mwanasheria huyo
baada ya kuapa Kwa Rais anaanza majukumu yake kama Mwanasheria Mkuu, lakini
hataanza majukumu yake kama mbunge mpaka pale atakapoanza kushiriki katika
shughuli za Kibunge. Hii haina tofauti na uteuzi wa Mawaziri.
Pamoja
na hayo ibara ya 68 ya Katiba inaeleza wazi kwamba, na nanukuu Kila
Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza
kushiriki katika shughuli za Bunge. Kwa mantiki ya Ibara hii ni
kwamba Mawaziri hao walioteuliwa na Rais ni wabunge isipokua hawawezi kushiriki
katika shughuli za ubunge bila kula kiapo au pasipo kuapishwa na Bunge.
Swali la kujiuliza ni shughuli gani za bunge zinazozungumziwa na Ibara
hii ya 68. Shughuli za bunge kama inavyoelezewa ni kutunga sheria pamoja na majukumu
mingine ya waliyopewa Kikatiba.
Kwa
upande wa Pili, Rais amepewa mamalaka ya Kikatiba katika Ibara ya 55 (1),(2),(3)
kuteua Mawaziri na manaibu wao, hata hivyo mawaziri hao hawaruhusiwi kutekeleza
majukumu yao ya kiuwaziri pasipo kutii masharti ya Ibara ya 56 ya Katiba ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inayowataka Mawaziri hao kula kiapo kwa raisi
kabla ya kuanza majukumu yao. Ningekua na maoni tofauti kama, Mawaziri hao wangeanza kufanya shughuli zao za kiutendaji kama Mawaziri kabla ya kuapishwa na Rais..hapo ndipo tungesema wamekosa uhalali wa kiutendaji kama Mawaziri.
Kwa
mantiki hii basi ya tafrisi ya Kikatiba ni Kwamba Mh. Rais hajafanya kosa
lolote la kuwateua wabunge hao kua Mawaziri kabla ya kuapishwa na Bunge.
Ni
rai yangu kwamba, Wanasiasa waache maneno ya uchochezi kupotasha raia
ilikuepuka migogoro isiyokua na tija katika Taifa. Iwapo wadau wanaona ya
kwamba kuna ulazima wa Mawaziri kuapishwa na Bunge kabla ya kuanza majukumu yao
ya uwaziri, basi wapeleke maoni na mapendekezo yao kwenye Tume ya Mabadiliko ya
Sheria kutoa maoni yao, pale Tume inapoanza kupokea maoni hayo.
No comments:
Post a Comment