Hivi punde, Mahakama Kuu kanda ya Tabora imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na aliyekua mgombea wa uchaguzi, kupitia tiketi ya CCM, bwana Jamal Tamimu kupinga matokeo ya Uchaguzi yaliyompa ushindi Mbunge Kijana wa NCCR MAGEUZI ndugu Felix Mkosamali.
Akitoa hukumu hiyo, iliyodumu kwa zaidi ya masaa matatu Mheshimiwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mwanza aliyekua anasikiliza kesi hiyo, Aishieli Sumari akisema ya kwamba Mlalamikaji alishindwa kutibitisha kesi yake kwa kiwango kinachotakiwa kisheria pasipo kuacha shaka yeyote.
Awali, katika hati yake ya madai Bwana Jamal(CCM) alilalamika ya kwamba katika Uchaguzi huo wa Jimbo la Muhambwe Mh. Mkosamali alimtolea maneno ya kashfa bwana Jamal ya kwamba ni Jambazi, si raia wa Tanzania, Muuaji na mchuuzi wa Viungo Vya Albino. Upande wa malalmikaji uliwakilishwa na wakili Msomi bwana Obuya katika shauri hilo.
Pamoja na hayo mlalamikaji katika shauri hilo hakutokea Mahakamani hapo hukumu ilipokua inasomwa.
Hukumu hio, iliyohudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji wa kibondo, mawakili wasomi wa Serikali, Bwana Prosper Mwangamila, na Renatus Mkude kwa upande walalamikiwa wa kwanza(Mwanasheria Mkuu wa Serikali) Pamoja na Dr. Murungu na Bwana Kabuguzi( Mawakili mlalamikiwa wa kwanza bwana Mkosamali).
Hukumu hii inafanya kesi zilizo baki za matokeo ya uchaguzi kuwa saba, Ikiwemo ile ya UKonga, Meatu, kasulu nk.
Hukumu hii inafanya kesi zilizo baki za matokeo ya uchaguzi kuwa saba, Ikiwemo ile ya UKonga, Meatu, kasulu nk.
No comments:
Post a Comment