Papaa musoffe akiingia Mahakamani |
HATIMAYE
mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini
Marijani Abdubakari Msoffe maarufu kwa jina la “Papa Msofe chuma cha reli
akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kesi ya
mauji.
Wakili Mwandamizi wa
serikali Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome alidai kuwa
Msofe ambaye ni mkazi wa Mikocheni,anakabiliwa na kosa moja la mauji ambalo ni
kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Papaa akiingizwa kwenye rejesta |
Wakili Kweka alidai
kuwa Novemba 6 mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa Papa Msoffe anayetetewa na
wakili wa kujitegemea Majura Magafu alimuua Onesphory Kitoli na kwamba
upelelezi wa kesi ya hiyo bado haujakamilika.
Kwa upande wake
hakimu Mchome alisema kesi hiyo ambayo ipo mbele yake ni mauaji na mahakama
yake haina mamlaka ya kuisikiliza na kwamba mahakama yenye mamlaka ya
kusikiliza ni Mahakama Kuu hivyo akamtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote.
“Kwa sababu hiyo
naiarisha kesi hii hadi Agosti 23 mwaka huu, kesi hii itakuja kwaajili ya
kujatwa na kwa kuwa kesi hii haina dhamana naamuru mshitakiwa apelekwe
gerezani”alisema Hakimu Mchome.
Msofe ambaye
alifikishwa kwenye eneo la mahakama hii jana saa 3:30 asubuhi chini askari
kanzu watatu ambao mmoja alikuwa amebeba silaha na kisha kumuingiza kwenye selo
ya mahabusu hiyo kwaajili ya kumuifadhi hadi ilipofika saa tano saa asubuhi
mshitakiwa huyo aliingizwa kwenye chumba namba tisa cha mahakamani hapo na
kuanza kusomewa maelezo yake huku ndugu na jamaa zake walikuwa wamefika
mahakamani hapo kwaajili kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao.
Msofe ambaye jina
lake limekuwa likitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo zinazopigwa na Bendi za
Miziki ya Dansi nchini ikiwemo Bendi ya FM Academia na Acudo Impact aliletwa na
askari kanzu hao akitokea kwenye sero ya jeshi la polisi ambako kwa zaidi ya
wiki moja sasa alikuwa akiishi ndani sero hiyo ya polisi kwaajili mahojiano na
mshitakiwa huyo na hatimaye jana akafikishwa mahakamani hapo kwa kesi ya mauji.
Papaa akirudishwa Mahabusu |
Itakumbukwa hivi
karibuni mjane mmoja aishie Mbezi Beach alilalamika kupitia vyombo vya habari
kuwa Papa Msofe anataka kumdhuru nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe wake
kupitia vyombo vya habari, hali iliyosababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kuingilia kati sakata hilo na hatimaye mjane huyo akarudishiwa nyumba yake
aliyokuwa akidai Msofe anataka kumdhurumu.
No comments:
Post a Comment