Waziri wa MaMambo ya Ndani wa Malawi; Nd.Uladi Musa |
MALAWI
imesema imeondoa ndege zake zilizokuwa zikifanya utafiti wa mafuta katika Ziwa
Nyasa kwa kuwa haitaki kuingia vitani, badala yake imeamua kupeleka mgogoro huo
Mahakama ya Kimataifa,
Mgogoro
baina ya Malawei na Tanzania hivi karibuni uliingia katika hatua nyingine,
baada ya Serikali ya Tanzania kuiagiza Malawi kuondosha ndege zilizokua
zinafanya utafiti wa mafuta katika eneo lake. Waziri wa Tanzania wa Mambo ya
Nje Bernard Membe aliliambia Bunge huko Dodoma
kwamba lazima Malawi iache mipango yake ya kuchunguza mafuta katika ziwa
nyasa na kukiita hicho ni kitendo cha
uchokozi.
Malawi
iliingia mkataba na Kampuni ya Uingereza Surestream mwaka jana kufanya utafiti
katika maeneo ya ziwa nyasa ambapo
inaaminika kuwa na mafuta na gesi kwa wingi.Hoja ya Tanzania katika
mgogoro huu ni kwamba katika sheria za kimataifa ni kwamba iwapo nchi mbili zinatengwa maji, mpaka ni katikati ya maji hayo na kwamba, Tanzania inapinga
umiliki wa Malawi kwa asilimia mia katika ziwa nyasa.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Malawi Uladi Mussa anasemaje?
Waziri
wa Malawi ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Ndani, Uladi Mussa, akizungumza na
Zodiak Broadcasting Station (ZBS) siku ya Jumanne aliimiza watu katika wilaya
mbili za Karonga na Chitipa zinazopakana na Tanzania kubakia shwari kwakua hakuna kitu ambacho kingetokea.
"Mimi
lazima kuwahakikishia watu wote katika nchi hii kubakia shwari. Sisi tuzungumza
na serikali ya Tanzania na mambo yote tatakua
mazuri. Ikishindikana sisi tutalipeleka suala hilo Mahakama ya
Kimataifa ya Haki, " alisema Waziri huyo.Waziri huyo alisisitizakwamba
ziwa yote ni ya Malawi na kuongeza kwamba serikali ina ushahidi wa kuthibitisha
hatua yake.
"Hakuna
suala hapa. Sisi wote tunajua ziwa ni letu. Kwa kweli kama madai kama hayo
yangekuja kutoka Msumbiji angalau
ingekuwa inaleta maana kwa kiasi fulani lakini si Tanzania. Tuna ushahidi wa
mikataba kuonesha kwamba Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi, "alisema Waziri wa
Mambo ya Ndani.
Hoja ya Malawi.
Serikali ya Malawi inasema kwamba hoja ya kwa Tanzania-kwamba ziwa litakua la pamoja
itatumika pale tu ambapo hakuna mkataba lakini katika hali hii mpaka ilikuwa
wazi na hasa ilivyoainishwa katika Mkataba wa 1890 Heligoland.
Aidha, alisema kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika
1963 Wakuu wa Nchi wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) alifanya azimio kwamba
nchi wanachama wanapaswa kutambua na kukubali mipaka waliokuwa rithi wakati wa
uhuru.
No comments:
Post a Comment