Mh. Naibu waziri wa Katiba na Sheria Kulia akiteta jambo nje ya ukumbi wa Bunge( Picha ya Maktaba) |
Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria Bi. Angellah Kairuki, wakati alipokutana na Wanaharakati wa
Kisheria wa Asasi zisizo za Kiserikali ofisini kwake jijini Dar-Es-Salaam. Mhe.
Kairuki amesema kuwa mchakato huo utakapokamilika utawezesha Wasaidizi wa Sheria kutambuliwa na sheria
husika na hivyo kupanua wigo kwa wananchi wa mijini na vijijini kuwa na msaada
wa kisheria wanapopatwa na matatizo.“Natambua umuhimu wa uundwaji wa Sheria hii
ya Paralegals ndio maana tumeanza mchakato huu kwa kuufanyia marekebisho na
kueleza dhana nzima ya Palalegals,” Alisema.
Amewataka
Wanaharakati hao kuendelea kuwasisitiza Wasaidizi wa sheria kuhakikisha kuwa wanatoa Huduma zao kwa uwazi
zaidi ili wananchi waweze kufaidika hiyo.Amesema Serikali itahakikisha kuwa
inaweka mazingira bora yatakayowawezesha
Wasaidizi wa Sheria kufanya kazi zao vizuri lakini kwa kuzingatia
misingi ya Sheria na Haki za Binadamu.
Wanaharakati hao
wamesema kuwa mpaka sasa Wasaidizi wa Sheria (Paralegals) bado hawajatambulika
kisheria na kwamba sheria haitoi nafasi kwa Mawakili wa Serikali au wa
kujitegemea kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo na Mabaraza ya Kikata maeneo
ambayo ndiyo yenye matatizo makubwa ya kisheria kwa wananchi wa kawaida.
Akizungumza kwenye
mkutano huo Wakili wa Kujitegemea Bw. Alphonse Katemi amesema wananchi wengi
wanakosa haki kwa sababu mfumo wa kisheria hauruhusu kwa Mawakili kutoa huduma
za kisheria katika Mahakama za mwanzo na Mabaraza ya Kata. “Kwa hiyo ni suala
ambalo kwa kweli wananchi wengi wanakosa haki kwa sababu ni mfumo wa kisheria
mawakili kwenye mabaraza haya ya ardhi
hawaruhusiwi,” Alisema Katemi na kuongeza kuwa huko ndiko kwenye maeneo
ambayo yanawatesa sana na kuwaumiza wananchi wa nchi hii.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasadizi wa Sheria Bi. Flora Masoy amesema kuwa endapo
hao Wasaidizi wa Sheria watawezeshwa kutambulika ni wazi kuwa ata kazi zao
wanazozifanya nazo zitatambulika kisheria.Wamesema iwapo Wasaidizi hao
watatambulika kisheria itawasaidia kutoa huduma za kisheria hasa kwa wananchi
waliopo vijijini ambao ndio wengi wanaokabiliwa na uelewa mdogo wa haki zao.“Wananchi
wengi hasa wa maeneo ya vijijini wanashindwa kupata huduma za kisheria vizuri
kutokana na kutokuwepo na watoaji wa kutosha wa huduma za kisheria,” Alisema
mmoja wa Wanaharakati.
Naye Mkurugenzi wa
Huduma za Kisheria wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph Ndunguru, amesema
kuwa kwa kutambua umuhimu wa Paralegals Serikali imeandaa Waraka wa Baraza la
Mawaziri kwa ajili ya kutunga sheria ambayo lengo kuu kuwatambua Wanasheria
Wasaidizi. Amesema katika mchakato huo
wa kuandikwa kwa sheria hiyo Serikali itahakikisha kuwa inawashirikisha wadau
mbalimbali katika kupata mawazo mapya yatayowezesha wananchi kupata msaada wa
kisheria. Chanzo Michuzi blog.
No comments:
Post a Comment