Ndugu Mwanasheria, naomba Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa makamu, ninayeishi nchini marekani, katika mji wa Newfoundland jimbo la Wayne. Sasa nimekua na matatizo fulani fulani na mke wangu ambaye anaishi Tanzania. Na nimeona njia muafaka ya mimi kuendelea na maisha yangu ni kuachana naye. Tatizo langu kubwa sijui ni taratibu gani za kufanya(legal procedures), ili niweze kudivorce na huyu mama? Tafadhali naomba Mnipe ushauri wa kisheria juu ya taratibu za kufuatwa ili niweze kutengana kisheria na mke wangu huyo wa ndoa. Ikizingatiwa kwamba mie naishi marekani nayeye anaishi Tanzania.Asante.
3 comments:
kama unasababu za msingi za kisheria ambazo, ni ukatili kwa upande wa mkeo kama anakufanyia, uzinzi au kukutenga na kukutenga huko kusiwe chini ya miaka mitatu lakini usichukulie kukaa kwenu mbali ni utengano hapana..muwe mmetengana kwa mgogoro na bila kukutana kimili kwa mda niliousema..hizo ni sababu za kisheria kuweza wewe kuiomba mahakama itoe talaka....lakini pia kwa taratibu za kisheria sijajua wewe una utaifa gani maana hujasema lakini mbali na hayo tunaangalia ni wapi ndoa yenu ilipofungiwa maana sheria ya ndoa ya Tanzania inazitambua ndoa zilizofungwa nje ya Tanzania lakini zikasajiliwa Tanzania na hata zile zilizofungwa kwenye balozi zote za Tanzania nje ya T anzania. lakini mbali na hapo mahakama haipokei mashauri yoyote ya ndoa bila kupitia balaza la usuluhishi aidha la kanisani au la kata kama ndoa yako ni ya kidini au ya kiserikali katika hayo mawili juu.....
Kabla ya kukushauri ni vyema tukajiridhisha kwamba ndoa ilifungwa wapi na tatizo lipo wapi? Ni vizui ukaja bongo kama ndoa ilifunwa huku (lex loci contractus) na ukaendelea na maisha. Kama mlifunga huko basi unaweza ukainitiate process huko na ukaja kukazia hukumu huku (lex domicile). Lakini kama ulioa huku njoo ukamilishe huku. Laiti mkeo angekuwepo huko basi ungepetition hukohuko majuu.
Wadau, kwa mujibu wa maelezo ya ziada aliyonipatia mtu huyu, yeye ni mtanzania na ndoa ilifungwa Tanzania(Lex Contractus); but mke wake anaishi Tz, Bwana huyo anaishi marekani. Asanteni tuendelee kumshauri.
Post a Comment