Koffi Olomide |
Mwanzamuziki gwiji wa miondoko ya rumba amefungwa kifungo cha miezi 3 na Mahakama moja ya mjini kinshasa baada ya kukutwa na hatia kwa kuvuruga usalama wa umma.
Mapema jana Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini
Kinshasa na kufikishwa mahakamani. Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinshasa ilifurika
kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin
akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi leo(Alhamisi)asubuhi wakati
atakaposhitakiwa rasmi.Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide
aliwakilishwa na mawakili 10 lakini idadi hio ya mawakili iliongezeka na kufikia 14 .Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake
Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.
Jopo la mawakili wanaomtetea mwanamuziki huyo, huenda ikakata rufaa baada ya kutoridhishwa na kifungo alichohukumiwa mteja wao.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya
"soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer",
lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile
wanatambulika kwa kunengua maungo
No comments:
Post a Comment