Powered By Blogger

Wednesday, June 15, 2011

Mtoto atekwa shuleni na kuchinjwa

Katika habari iliyolipotiwa na gazeti la Habari leo, MWANAFUNZI Doris Lutego (12) wa Shule ya Msingi Livingstone, wilayani Njombe mkoani Njombe ameuawa kinyama baada ya kuchinjwa na watu wasiofahamika, akitenganishwa kichwa na kiwiliwili chake. Habari zilizolifikia gazeti hilo( juzi jioni )na kuthibitishwa jana na Polisi Mkoa wa Iringa, zinaeleza kwamba mwanafunzi huyo, alikutwa na mkasa huo wa kusikitisha usiku wa kuamkia juzi saa 10 alfajiri.

Taarifa kutoka shuleni hapo zinadai kwamba watu wasiofahamika walivamia shule hiyo na kumteka mwanafunzi huyo. Hata hivyo haikufahamika mara moja sababu za wavamizi hao kumteka na hatimaye kumchinja mwanafunzi huyo, mkazi wa mtaa wa shule ya Uhuru, mjini Makamambo wilayani humo.

Taarifa hiyo inaonesha kwamba baada ya mwanafunzi huyo kutekwa na taarifa kuzagaa shuleni na maeneo yanayozunguka shule hiyo, jitihada za kumtafuta zilizofanywa na wanafunzi kwa kushirikiana na wananchi na viongozi wa shule hiyo hazikuzaa matunda.

Chanzo cha  habari  cha gazeti hilo, kilieleza kuwa, sehemu za mwili wa mwanafunzi huyo zilikutwa katika maeneo tofauti ya Kitongoji cha Kambarage, wilayani humo.

“Mapema Jumatatu asubuhi, ulionekana mfuko wa Salfeti nyuma ya nyumba ya Balozi wa Kitongoji hicho, ukiwa na kiwiliwili cha mwanafunzi huyo, huku kichwa chake kikikutwa karibu na nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji hicho kikiwa kimehifadhiwa kwenye mfuko wa madaftari ya mwanafunzi huyo,” alisema mtoa habari wetu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarit Mangalla alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuongeza kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akisoma darasa la tano katika shule hiyo. Mangalla alisema kuwa taarifa zilizofika Polisi juzi zilikuwa ni za kutekwa kwa mtoto huyo, huku baadhi ya meno yake na damu vikikutwa katika kitanda chake.

Kwa mujibu wa  vifungu vya 196 na 197 vya Sheria Ya Makosa ya Jinai Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekemisho mwaka 2002, ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kuuwa, kusababisha mauti ya mtu mwingine. Iwapo wauaji hao watapatikana na hatia watahukumiwa kunnyongwa mpaka kufa.

Mhasibu kizimbani kwa kughushi sahihi

MHASIBU wa Kampuni ya Tasu, Machafu Chokoma (59) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili, likiwemo la kughushi sahihi na kujipatia Sh milioni 1.8 kwa njia ya udanganyifu. Chokoma alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita na kusomewa mashitaka na Hakimu Wilberforce Luhwago wa mahakama hiyo.

Wakili wa Serikali Sakina Sinda, alidai mshitakiwa alighushi saini ya Kaimu Mhasibu wa kampuni hiyo, George Kambute, kwenye hundi No.504642. Kwa mujibu wa madai hayo, hundi hiyo iliyoghushiwa ilionesha kuwa Kimbute amesaini ili atoe fedha hizo kutoka akaunti yenye namba 015007803600 jambo si la kweli.

Sinda aliendelea kudai kuwa, Oktoba 22 mwaka jana katika Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, Dar es Salaam, Chokoma alijipatia Sh milioni 1.8 kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti hiyo kwa kutumia hundi ya kughushi iliyoonesha imesainiwa siku hiyo hiyo. Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Luhwago aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 23 mwaka huu itakapotajwa tena. Hata hivyo Mshitakiwa aliiachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Habari hii chanzo chake ni Habari leo.

Monday, June 13, 2011

Majambazi yaua, yapora Mil.12 Muhimbili.

WATU wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, jana asubuhi walivamia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam,wakampiga risasi na kumuua mlinzi wa hospitali hiyo, Juma Nagungu, kisha kupora fedha kiasi cha zaidi ya Sh milioni 12. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi jirani na eneo la mapokezi na kusababisha hofu kwa watu mbalimbali wakiwemo wagonjwa, kufuatia risasi zilizofyatuliwa na majambazi hao.

Eligaesha alisema, awali Nagungu na wafanyakazi wawili wanawake wa Idara ya Fedha hospitalini hapo, walikuwa wakizihamisha fedha hizo ambazo ni makusanyo ya siku za mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa kutoka mapokezi kwenda idara ya uhasibu.

Amesema walipokaribia kufika huku wakiwa ndani ya gari aina ya Nissan lenye namba za usajili SU 36713, ghafla walishambuliwa kwa risasi ambayo mojawapo ilimpiga sehemu za mbavuni mlinzi na wao kuzipora fedha hizo zilizokuwa kwenye mkoba kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi waliokuwa wametoka kuzichukua kisha kutoweka nazo.

“Lengo ilikuwa wazikusanye fedha hizo na zingine zilizokuwamo ndani ya idara ya uhasibu ili wazipeleke benki kwa pamoja, lakini kwa bahati mbaya kabla hawajafika nazo tukio hilo likatokea,” amesema Eligaesha.

Kwa mujibu Eliegesha, mlinzi huyo alifariki dunia muda mfupi wakati wakimuwahisha kitengo cha dharura kwa ajili ya matibabu na kuongeza kuwa majambazi hao walikimbia kwa kutumia mlango wa kawaida wa kutokea magari. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Faustine Shilogile, alisema hakuna mtu anayeshikiliwa kufuatia tukio hilo huku upelelezi ukiendelea.

Alisema hadi Polisi wanafika katika eneo hilo majambazi hao walikuwa tayari wameshakimbia na bila kujua mahali walikoelekea.

Mahakama Kuu yaamuru Askofu Mokiwa na mwenzake wakamatwe.


Baba Askofu Valentino Mokiwa
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, chini ya Jaji Kakusulo Sambo imeamuru kukamatwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk. Valentino Mokiwana Stanley Hotay kwa kukiuka amri ya Mahakama na kumsimika Askofu, StanleyHotay. Amri hiyo imetolewa ikiwa ni siku mbili tangu kusimikwa kwa askofu huyo, ambapo  Ijumaa  iliyopita mahakama hiyo ilisitishwa kusimikwa kwa Askofu Hotay kutokanana    kesi iliyofunguliwa dhidi yake na waumini wa kanisa hilo, ambapo Askofu Hotay aliingia katika mgogoro wa kikatiba kutokana na umri wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa sherehe za kumsimika askofu huyo zilifanyika Makao Makuu ya Dayosisi hiyo ya Mount Kilimanjaro na kuongozwa na Askofu Mokiwa, ambapo alieleza kuwa sherehe zilizofanyika ni za kumsimika Askofu wa Kanisa la Anglikana na si Askofu wa kanisa hilo Dayosisi hiyo, na kwamba kusimikwa  rasmi kungelifanywa baada ya mashauri yaliyoko mahakamani kumalizika. Katika kesi hizo moja ya madai namba 18/2011 na Jinai namba 48/2011 zilifunguliwa dhidi ya Wadhamini wa Kanisa hilo na Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo, Hotay na Bw. Lothi Oilevo, Bw. Godfrey Mhone na Bw. Frank Jackob pamoja na mambo mengine waliiomba Mahakama kuzuia kusimikwa kwa askofu huyo kwa madai ya kuchakachua umri.

Akinukuuvifungu mbalimbali vya sheria, Jaji Sambo alisema Askofu Mokiwa na Hotay walichokifanya kwa yeyote ni ukiukaji wa amri ya mahakama “Nimeridhika kuwa amri halali ya mahakama imekiukwa na ieleweke bayaha kuwa nchi hii inatawaliwa na Utawala wa Sheria na hilo limekuwa likisisitizwa mara kwa mara na rais wetu Mh.Jakaya kikwetwe na Viongozi wengine wa Juu alisema Jaji huyo.

Aliieleza mahakama kuwa ma-askofu hao wamefanya kitendo muhimu kilichosababisha amri  ya mahakama isiheshimiwe jambo ambalo ni hatari kwa utawala wa sheria; “kama anasema utanifanya na kuingilia hata kukiuka amri ya Mahakama Kuu sembuse, mahakama zingine za chini itakuweje!..hivyo mahakama ni wajibu wake kutumia vifungu kadha wa kadha kama kifungu cha 114 (i) C na K na (iii) pamoja na kifungu namba 124 vinavyoipa mahakama hii kuwaadhibu wale watakaokiuka amri ya mahakama…huwezi kuacha mahakama inachezewa na vifungu vyote hivyo vipo…sasa naamuru…ni amri ya dola kuwa Askofu Dk. Mokiwa na Hotaywakamatwe mara moja”.

 Awali Jaji huyo alisema walalamikaji waliwasilisha mahsuri hayomahakamani kuomba itolewa amri ya kuzuia sherehe hizo kimya kimya lakini kwa busara na mahakama hiyo ikaamua kuuita upande mwingine ambao nao ulitoa pingamizi la awali lililotaka ombi hilo liondolewa na sherehe za kumsimika Askofu huyo zifanyike lakini baada ya mahakama kuona muda wa kutoa maamuzi ni mfupi iliamuru sherehe hizo kusimama hadi uamuzi wa mahakama utakapotolewa jana (Jumatatu).

Alidai kuwa pamoja na jitihada zote hizo za kutumia busara wao waliendelea na kumsimika mchungaji huyo kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, wakati mahakama iliona si busara kuendelea na zoezi hili wakati wapo watu wengine wakipiga kelele juu ya hilo, lakini kabla mahakama hiyo haijatoa maamuzi, wao wamemwapisha, na sasa ni kuwa mwenendo mzima wa shauri hilo hauna maana yoyote kwani ni kweli kabisa kuwa ni ngumu kumtoa Uaskofu maana yake ni kwamba mwenendo mzima wa mashauri hayo umevamiwa.

 Jaji huyo alisema wadai katika madai yao walieleza kuwa Katiba ya Kanisa hilo inaelekeza kuwa mgombea kiti hicho anayeweza kukalia  kiti hicho lazima awe na miaka kati ya 40 na 60 ndipo anapoweza kukabidhiwa dhamana ya kuwa kiongozi wa ngazi hiyo, ambapo Askofu huyo alidaiwa kuwa mwaka jana alikuwa anayo miaka 38 tu. Awali, wakili wa Upande wa Madai Meinrad D’souza aliileza mahakama hiyo kuwa amri iliotolewa na Mahakamam hiyo haikutekelezwa hivyo sherehe za kumsimika Uaskofu Hotay zilishafanyika Jumapili iliyopita jambo ambalo ni kukiuka amri halali ya mahakama, hivyo kwa ukiukaji huo aliiomba mahakama hiyo kwa vya sheria vilivyopo kuwakamata wahusika wakuu wa tukio hilo ambao ni Askofu Mokiwa na Hatay.

“Mheshimiwa Jaji kabla ya kuendelea na lolote kuna jambo muhimu limetokea kutokana na amri ya mahakama yako iliyotolewa Ijumaa iliyopita, amri hiyo imekiukwa na sherehe za kumsimika Askofu Stanley Hotay zimefanyika Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro, upo ushahidi wa kutosha juu ya hilo na kwamba kwa mujibu wa katiba ya Kanisa Askofu kupatikana kwa kuchaguliwa kutoka katika Dayosisi husika, labda hiyo ni utaratibu mpya wa kuwapata maaskofu”aliongeza D’souza. Akijibu hoja hizo, Wakili Tadayo alisema kilichofanyika ni kumsimika Uaskofu wa Kanisa hilo Tanzania na si Askofu wa Dayosisi hiyo na kwamba kitendo cha kumsimika uaskofu hakina maana kuwa ndiyo Askofu wa Dayosisi hiyo, kitendo hicho na cha awali na iwapo shauri litaisha mahakamani atasimikwa rasmi kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, hivyo aliomba Mahakama hiyo kuendelea kusoma maamuzi wa mahakama juu ya maombi ya walalamikaji.

Sunday, June 12, 2011

Jaji Mkuu Kenya: Avaa hereni,atuhumiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Jaji Mkuu Mteule wa kenya

Jaji Mkuu mteule wa kenya Dk. Willy Mutunga mwenye umri wa miaka 65, anakabiliwa na tuhuma mbalimbali moja ikiwapo ya kuvaa hereni katika mojawapo la sikio lake. Dk Mutumga alizidi kubainisha ya kwamba ni kama akiambiwa kuivua hereni yake hiyo ili awe Jaji mkuu, ni bora akaendelea na kuivaa hereni na kungatuka kwenye kiti hicho.

“I wear my ear ring not because of my sexuality but spirituality. There is no way I can remove this ear ring even if I become the Chief Justice. If am told I must remove it to get the job of Chief Justice I will say keep your job,” Dr Mutunga said.


Dk Mutunga amewahi kuwa mhadhili katika shule ya sheria kenya(law school), mwenyekiti wa zamani wa Jamii ya Sheria wa Kenya (kenya law society) na mtu mashuhuri katika mapambano ya kisiasa ya nchi ya kenya ambapo kwaka 1982 alipata  mateso ya kunyimwa dhamana na mahakama kufuatia kukamatwa yake juu ya milki ya nyaraka mbalimbali za uchochezi Julai 10, 1982, wakati yeye alikuwa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Msomi huyo aliyepata shahada yake ya uzamili katika chuo kikuu cha Dar es salaam pia Jaji mkuu mteule nchini Kenya Dk Willy Mutuga amekanusha kama anashiriki mapenzi ya jinsia moja.Mutunga aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na kamati maalum ya bunge.Kamati hiyo ya bunge ilifanya vikao vyake vya siku mbili kusikia shutuma zilizotolewa dhidi ya walioteuliwa kuchukua nyadhifa za jaji mkuu,naibu jaji mkuu na mwendesha mashtaka mkuu

Anashiriki

Hatua hii ilichukuliwa baada ya baadhi ya watu na hasa makanisa yakidai walioteuliwa si watu wanaozingatia maadili ya kifamilia kukiwemo na shutuma kuvaa hereni kwenye sikio la kushoto kwa Dk Mutunga ni ishara kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja."Sishiriki mapenzi na wanaume,ila siwezi kuwabagua wanaume au wanawake wanaoshiriki mapenzi hayo,mimi mwenyewe mpwa wangu ni wa jamii hio",alisema Dk Mutunga.

Mchakato

Naibu jaji mkuu mteule Nancy Baraza pia alikuwa na muda wake wa kujitetea,alipoulizwa kwa nini alikita utafiti wake wa shahada ya uzamifu katika suala la haki za wapenzi wa jinsia moja. Baraza alisema anafanya hivyo kwa kuwa alitaka kuwa mbunifu na kufanya utafiti wa kipekee ambao haujawahi kufanywa nchini Kenya.

Baada ya vikao hivyo kwa umma ambavyo vimetumika kuwatathmini tena wateule,majina hayo yatawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura,ikiwa wataidhinishwa basi watachukuwa nyadhifa na iwapo watakataliwa bai mchakato wa usaili utaanza upya

Legal Joke: Contribution to bury a lawyer

A lawyer, known more for his drinking at the bar than for his practice before it, died in poverty. The other attorneys from the city, feeling sorry for his family, started a fund to cover his funeral expenses. A local businessman was asked to make a contribution.” Will you please donate a dollar, so we can bury a lawyer?” Only a dollar to bury a lawyer?" asked the businessman, "Here's $100 -- go and bury 99 more of them."

In another indecent, a man went to his lawyer and told him, "My neighbour owes me $500 and he doesn't want to pay up. What should I do?" "Do you have any proof?", asked the lawyer. "Nope," replied the man. "Okay, then write him a letter asking him for the $1,000 he owes you," said the lawyer. "But its only $500!" replied the man. "Precisely, that's what he will reply and we will have the proof we need," said the lawyer.

Thursday, June 9, 2011

Waajiri wakaidi kupandishwa kizimbani

Mh.Gaudensia Kabaka
SERIKALI imewataka waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kushiriki katika mafunzo ya sheria za kazi yanayotolewa nchini kote kinyume na hivyo Idara ya Ukaguzi inaweza kuwafikisha  mahakamani. Mpango huo wa elimu unagusa wadau wote waliopo katika sekta binafsi na sekta ya umma.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alisema hayo juzi Dar es Salaam wakati akizungumzia elimu inayotolewa kwa wadau hao ili kuwaongezea uelewa juu ya sheria za kazi, haki na wajibu wao katika utekelezaji wake.

Sheria hizo ni za mwaka 2004 ambazo ni sheria namba sita ya ajira na mahusiano kazini na sheria namba saba ya taasisi za kazi.

Alisema, mpango huo umeanza kutekelezwa rasmi Machi mwaka huu kupitia ofisi zao nchini kote na kwamba hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 1,000 kutoka sehemu mbalimbali wameshiriki katika mafunzo hayo.

“Licha ya kwamba mpango huo unahusisha waajiri na wafanyakazi, lakini wapo waajiri wanaowakataza wafanyakazi wao kushiriki, jambo ambalo halileti tija katika utendaji kazi,” alisema Waziri Kabaka bila ya kuwataja waajiri wanaofanya hivyo.

Waziri Kabaka alisema, kwa waajiri wanaowakataza wafanyakazi wao kushiriki katika mafunzo hayo kanuni za sheria hizo zinaruhusu Idara yaUkaguzi kuwapeleka mahakamani waajiri ambao hawatotekeleza.

Alisema, hakuna mwitikio wa wafanyakazi kushiriki katika mafunzo hayo, huku waajiri wakidai kuwa kwa kufanya hivyo kunaweza kupunguza uzalishaji kwenye sehemu zao za kazi.

Alisema, upo umuhimu wa wafanyakazi kuhudhuria katika mpango huo na kuzifahamu sheria hizo za kazi ili ziwasaidie kuondoa manung’uniko na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika sehemu za kazi kutokana na kila upande kufahamu haki na wajibu unaowapasa.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwepo kwa amani na utulivu na mahusiano baina ya waajiri na wafanyakazi ambapo kwa kufanya hivyo kutaongeza uzalishaji na utoaji wa huduma sehemu za kazi na kuongeza pato lao na hivyo kukuza uchumi.

Msaada Kizimbani!



Kaka habari, Mimi ni kijana(Jina kapuni), mkazi wa Dar es salaam. Wiki iliyopita nilipigiwa simu na rafiki yangu akiniomba akaunti namba yangu ya benki, kwamba anataka  hela yake itumwe kwenye hio akaunti.Mie bila hiyana nikamkubalia maana ni mtu tulie naye karibu. Sasa after few days akaniomba nikaangalie kama io hela imeingia, nikaenda atm kucheck kama hio hela imekua deposited. Cha ajabu nikakuta mamilioni ya shillingi nikajalibu kukomand kiasi kidogo cha fedha na zikatoka.

Baada ya hapo nikawasiliana na huyo rafiki yangu kumwambia pesa yake imeingia but nikamuuliza  mbona nipesa nyingi sana. Akanitoa wasiwasi kwamba hela hizo hazina tatizo lolote. A day thereafter nikapigiwa simu na polisi wakitaka  next week nifike kutoa maelezo maana hio ilikua pesa ya wizi . Kimsingi hio hela haikuchukuliwa. Lakini niko njia panda maana nahofu kuingizwa kwenye jambo nisilokua nahusika. Nahitaji ushauri wa kisheria juu ya hili. Asante.

Wednesday, June 8, 2011

NAFASI ZA KAZI KWA WANASHERIA - TANESCO




  1. Principle Legal officer- Risk Management, Good Governance and Compliance (1 post): Based on Dar es Salaam.

Minimal Requirements:

a.       A good Bachelor of law Degree
b.      A recognized member of Tanganyika Law society
c.       At least 3 years of working experience in a recognized legal firm or institution
d.      Must be a Computer literate

  1. Zonal Legal Officers(4 posts)- Central,North-East,South-West Highlands& Lake
                                                         Zone officers.

Minimal Requirements:

      a. A good Bachelor of law Degree
b. A recognized member of Tanganyika Law society
                  c. At least 3 years of working experience in a recognized legal firm
                      or institution.
d.      Must be a Computer literate


HOW TO APPLY:

Applications should be sent to hrg.humanresources@tanesco.co.tz

Or, SENIOR MANAGER HUMAN RESOURCES,
TANESCO LTD UMEME PARK,
UBUNGOPO.BOX.9024
DAR ES SALAAM


DEADLINE: Application should reach the undersigned not later than 14 days after initial appearance of this advert.

BINTI WA MIAKA 18 RUMANDE KWA KUFANYA MAPENZI NA MTOTO WA MIAKA 2!!


Mtoto aliefanyiwa matendo machafu
 Wakazi wa maeneo ya kigogo majuzi walishuhudia jambo ambalo ni nadra kutokea mara kwa mara katika maisha yao ya kila siku. katika tukio hilo la kustaajabisha binti(jina halifahamiki) alikutwa kwenye gofu akimfanyia matendo ya kingono mtoto anaekisiwa kua na umri wa miaka 2 na nusu hivi. Mama wa  mototo huyo katika kumtafuta mwanae alimbamba dada huyo akiwa amevua nguo zote amemlaza mwanae chini amemkalia kwa juu huku akikata mauno kama yupo na mwanaume mkubwa na sauti za utamu juu.

Mama wa mtoto huyo alipokutana na hali hiyo  alipigwa na  butwaa ndipo  alipokimbilia kuita majirani ili waone jambo lile ndio kumfurumua msichana huyo na kumpeleka polisi.Mtoto alikutwa kalala kalegea hana nguvu ameloa nguo zake maskini. Binti huyo bado anasota rumande akisubili hatima ya Kesi yake. Ikumbukwe ya kwamba katika kifungu 15(3)  cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 16, mtoto chini wa umri wa miaka 12 anakisiwa kutokuwa na uwezo  wa kufanya mapenzi"he is not capable to have canal knowledge. Habari hii kwa hisani ya Dina marios blog.

Legal Joke: A lawyer named Strange died.

A Lawyer named Strange died, and his friend asked the tombstone maker to inscribe on his tombstone, "Here lies Strange, an honest man, and a lawyer." The inscriber insisted that such an inscription would be confusing, for passersby would tend to think that three men were buried under the stone. However he suggested an alternative: He would inscribe, "Here lies a man who was both honest and a lawyer. That way, whenever anyone walked by the tombstone and read it, they would be certain to remark: "That's Strange!"

Monday, June 6, 2011

Mchungaji KKKT jela kwa rushwa ya ngono


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, imemhukumu kifugo cha miaka mitano Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Michael Ngilangwa, baada ya kupatikana na hatia ya kuomba rushwa ya ngono kwa  mwanafunzi ili amsaidia masomo.

Mchungaji Ngilangwa alikuwa mwalimu wa sekondari ya Pomerini iliyopo wilaya ya Kilolo.Akitoa hukumu hiyo mjini hapa jana, Hakimu wa Mkazi wa Mahakama Iringa, Bi, Martha Mpaze, alisema mshitakiwa wakati wote wa  kesi hakuwa na shahidi, ambapo alijitetea mwenyewe.

Upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano. Alisema mshitakiwa katika utetezi wake, alisema kesi hiyo ni ya kubambikizwa kosa hilo kutokana na wivu uliokuwepo kati yake na baadhi ya walimu wa sekondari ya Pomerini kumfanyia.

Alidai walimu hao walifanyia fitina baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Mkuu wa Shule Pomerini, hatua iliyomwongezea maadui ambao walikuwawakimfanyia fitina na kuandaa mazingira ya mtego ili ili akamatwe na mwanafunzi.Alisema katika utetezi wake, Mchungaji Ngilangwa alidai baada ya kushika wadhifa huo  wazazi wengi walikuwa wakimpelekea matatizo ya watoto wao, akiwemo mzazi wa mwanafuzni aliyemshitaki kwa madai ya kumuomba  rushwa ya ngono.

Alisema siku ya tukio mshtakiwa aliyokamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) alipigiwa simu na mama wa mwanafunzi huyo kuwa wanatoka Dar es Salaam hivyo aliomba awatafutie vyumba katika nyumba za kulala wageni.

Katika utetezi wake alidai kwamba alikwenda nyumba ya  wageni na kuchukua vyumba viwili kimoja cha kulala watu wawili.Alidai kwa kuwa ulikuwa ni usiku, alichukua chumba namba 4 kwa ajili yake.

Bi. Mpaze alisema mshtakiwa anaonekana kuwa na makosa kwa kuwa katika kitabu cha wageni alijaza kuwa anatoka Njombe kwenda Iringa wakati siyo kweli.Alisema ukweli ni kuwa mshtakiwa alikuwa anatoka Pomerini kwenda Iringa mjini.

Alisema kuwa ushihidi mwingine ambao unamtia hatiani Mchungaji Ngilangwa ni ule wa TAKUKURU kumkuta na vidonge vya kuzuia mimba, ambavyo alimpatia mwanafunzi wake ameze kwa kuwa wangefanya ngono bila kutumia kondomu.

Hakimu huyo alisema ushahidi mwingine ni ule wa ujumbe ambao TAKUKURU ilinasa sauti walipokuwa wakiongea na mwanafunzi wake.Hakimu huyo alikuwa akimwambia mwanafunzi huyo aende chumba namba nne ndiko wangelala.

"Mshtakiwa anatiwa hatiani kwa ushahidi mwingine ambapo TAKUKURU ilimkuta akiwa na mwanafunzi wake huyo saa 5:00 usiku wakati sheria ya nyumba hiyo ya kulala wageni walipokutwa inakataza watu wasio wanandoa kulala chumba kimoja.

Hakimu huyo alisema kama TAKUKURU wasingewahi mwanafunzi huyo angebakwa na azma yake ya kuomba rushwa ya ngono ingetimia.

Mshtakiwa huyo alipotakiwa kujitetea aliomba mahakama imfikirie kwa kuwa ana watoto wanne wanaomtegemea, wawili wanasoma sekondari na wengine shule ya msingi.

Mchungaji Ngilangwa aliongeza kuwa mzazi wake ni mzee wa miaka 82, hivyo hana mtu wa kumtunza.

Akitoa hukumu Hakimu Bi. Mpaze, alisema mahakama imezingatia kuwa mkosaji wa mara ya kwanza lakini akahukumiwa adhabu wa miaka mitano jela.Katika kesi ya pili ya kuomba rushwa ya ngono mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya sh. 500,000 au endapo atashindwa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela. Chanzo gazeti la Majira.

Mh. Mbunge Asota Rumande wiki Mbili.


Mh. Magdalena Sakaya
MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya pamoja na wenzake 10, jana walirudishwa tena rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na mahakama.Masharti waliyopewa washtakiwa hao yaligawanyika katika sehemu mbili yakiwatofautisha wale wanaotoka ndani ya Wilaya ya Urambo pamoja na wale wanaotoka nje ya wilaya hiyo.

Kwa wale wanaotoka nje ya Wilaya ya Urambo akiwamo, Mbunge Magdalena Sakaya walipewa masharti ya kupata hati ya mali isiyohamishika pamoja na kusaini dhamana ya Sh 3milioni  huku wale wanaotoka ndani ya wilaya wakitakiwa kupeleka barua ya ofisa mtendaji wa kata.

Washtakiwa wote walishindwa kutimiza masharti na walirudishwa rumande ambapo Hakimu Mkazi, Oscar Bulugu aliahirisha kesi hadi Juni 20 mwezi huu shauri lao litakapotajwa tena.Kabla ya washtakiwa hao kupandishwa kizimbani kulikuwa na makundi ya watu ambao wengi wanadaiwa ni wafuasi wa  CUF waliokuwa wakifuatilia shauri hilo wakiwa na imani kuwa washtakiwa watapata dhamana.

Kufuatia makundi ya watu hata idadi ya polisi nayo ilikuwa kubwa kuimarisha  ulinzi wa kutosha kukabiliana na aina yoyote ya vurugu endapo ingetokea  mahakamani hapo.Pamoja na baadhi ya watu kuhangaika kuhakikisha washtakiwa hao wanapata dhamana, jitihada zao zilikwama huku wengine wakisikika wakidai kuwa endapo viongozi wa kitaifa wa chama hicho wangekuwepo huenda washtakiwa wangepata dhamana.

Washtakiwa wote 11 akiwamo Mbunge Sakaya, walifikishwa wiki iliyopita baada ya kukamatwa karibu wiki mbili zilizopita ambapo walirudishwa rumande hadi jana. Chanzo gazeti la Mwananchi.

Sunday, June 5, 2011

MBOWE AKAMATWA: KUFIKISHWA KORTINI.


kiongozi Mkuu wa upinzani Bungeni
Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Tanzania, Dkt. Freeman Mbowe, anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama moja ya Mkoa wa Arusha, Kaskazini mwa nchi hiyo.Bw. Mbowe alikamatwa na polisi majuzi  kwa madai ya kukiuka sheria za dhamana.

Kukamatwa kwa Bw. Mbowe kunakuja siku chache baada ya mahakama moja mjini Arusha kuamuru akamatwe baada ya kukiuka dhamana.Anashutumiwa kwa kutojitokeza kortini wakati wa kesi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake wa Chama Cha Demokrasia (CHADEMA), ya madai ya kuandaa mkutano na kuandamana kinyume cha sheria, Januari 2011. 

Hata hivyo kukamatwa kwa Dkt Mbowe kumevutia hisia kali. Mbunge wa CHADEMA John Munyika, ametaja kukamatwa kwake kama udhalalishaji. ''Ni shambulio dhidi ya bunge na shambulio dhidi ya wabunge'', Bw Munyika amesema.

Naye mwenyekiti wa cha chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, anadai kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani bungeni ni njama ya kudhoofisha kambi ya upinzani bungeni, katika kipindi hiki cha kutayarisha bajeti ya nchi.

Friday, June 3, 2011

KESI YA MGOMBEA BINAFSI YAFUKUTA TENA.


Mchungaji Christopher Mtikila

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wameishtaki Serikali ya Tanzania katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu iliyopo mkoani Arusha, ikidai kusikilizwa na kutoa uamuzi wa suala la mgombea binafsi.TLS na LHRC wamedai kuwa suala la kuwapo mgombea binafsi ambalo liliwahi kuzua mjadala na gumzo nchini, ni haki ya msingi ya kikatiba.Hatua hiyo ya TLS na LHRC imekuja takribani mwaka mmoja tangu jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, kutoa hukumu iliyokubali rufaa ya serikali iliyopinga ruhusa ya kuwapo kwa mgombea binafsi nchini.

Juni 17, 2010, majaji saba wa Mahakama ya Rufani wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani walitengua hukumu ya kuruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kusema suala hilo litaamuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Lakini jana akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Rais wa TLS, Francis Stolla alisema kesi hiyo tayari imesajiliwa na kupewa namba 009/ 2011.Stola alisema kwamba kesi hiyo ni ya kwanza kutoka Tanzania, kwenda katika Mahakama hiyo, lakini pia kesi hiyo ina uwezekano mkubwa wa kushinda kwa kuleta mabadiliko na maendeleo  ya demokrasia, haki za kiraia na za kisiasa nchini.

Alisema kesi hiyo ya kikatiba inapinga Ibara ya 39,67 na 77 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1994.Stolla alisema kwamba mabadiliko hayo yanaondoa kabisa haki ya Watanzania wa kawaida kuchaguliwa katika nafasi  ya urais, ubunge na udiwani kama wagombea binafsi.


Alisema kuwa hawakubaliani na utaratibu huo kwa sababu inawezekana wapo watu hawakubaliani na ilani ya chama, sera na utaratibu wa chama chochote cha siasa kilichopo, lakini sababu ya katiba, wanakosa haki yao ya kuwa viongozi na kuutumikia umma.

Alisema ibara hizo za Katiba ya Tanzania ilivyobadilishwa, inaenda kinyume na Ibara ya 13 inayoeleza haki ya mtu kushiriki katika serikali yake na ibara ya 2 inayoelezea haki ya kulindwa dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu.

“Pia zinaenda kinyume na ibara ya 3 na 25 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa ya mwaka 1966 (ICCPR-1966),"alisema Stolla Alisema hilo ni tatizo lililopo katika nchi ya Tanzania pekee, tofauti na nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), kwa sababu nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi ambazo pia ni wanachama wa EAC zinaruhusu mgombea binafsi na tayari Uganda iliwahi kuwa na mgombea binafsi kwa nafasi ya urais, licha ya nchi hiyo kuwa na migogoro ya kisiasa.

Historia ya mgombea binafsi
Oktoba 24 mwaka 1994, Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila alishinda kesi dhidi ya Serikali katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ambayo iliruhusu kuwapo kwa wagombea binafsi.

Hata hivyo, baada ya kushinda, Serikali ilifanya marekebisho ya Katiba, badala ya kukata rufaa, ili mgombea binafsi asiwepo nchini.Mei 5, 2006 jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, lilitoa hukumu nyingine iliyompa ushindi Mtikila kwa kukubali kuwapo kwa wagombea binafsi, uamuzi ambao Serikali iliupinga kwa kukata rufaa.

Rufaa hiyo ndiyo iliyozaa hukumu iliyotolewa na majaji saba wakiongozwa na Jaji Ramadhani, ambayo ilibatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu na kuzuia uwapo wa wagombea binafsi nchini.

Hukumu hiyo ilipondwa na wanataaluma wengi wa sheria akiwamo mtangulizi wa Jaji Ramadhani, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta ambaye alisema kuwa mahakama ilikwepa wajibu na kwamba hukumu hiyo ni ishara kwamba siasa zilikuwa zimeanza kuuyumbisha mhimili wa mahakama. Habari hii chanzo chake ni Gazeti la Mwananchi.